MAANDAMANO YA MAADHIMISHO YA TAMASHA LA 11 LA TGNP JIJINI DAR ES SALAAM YAFANA


Tamasha la 11 la mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) limeanza kwa maandamano katika ofisi za TGNP eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam.
Maandamano hayo yameanzia lango kuu la ofisi za TGNP na kuhitimishwa katika viwanja vya tamasha eneo hilo la TGNP.
E84A0808 8e258
Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha hilo mkurugenzi wa TGNP Usu Mallya alisema wakati TGNP inaazimisha tamasha hilo bado inajivunia mapambano makubwa yaliyodumu kwa miaka 16 katika kupigania jengo hilo ambalo lilikuwa na kesi mahakamani hadi wanaposhinda kesi hiyo.
Hivyo alisema ushindi wa kesi hiyo dhidi ya jengo hilo utawafanya sasa kuendelea kuboresha zaidi jengop hilo na kulifanya kuwa la kisasa zaidi na kuendeleza mafunzo mbali mbali.
Chanzo:Francisgodwinblog

Comments

Popular posts from this blog