ALIYEGEUZWA MTUMWA WA NGONO AANIKA 'UCHAFU' WA KANALI GADDAFI
Kanali Muammar Gaddafi aliamuru kutekwa kwa wasichana wa shule ambao baadaye walishikiliwa kama watumwa wa ngono kwenye eneo lake, kwa mujibu wa kitabu kuhusiana na dikteta huyo. Msichana mmoja, aliyetajwa kama Soraya, alitekwa nyara wakati akiwa na umri wa miaka 15 na kushikiliwa kwa miaka mitano katika sehemu ya chini kwenye ngome yake yenye urefu wa maili sita nje kidogo ya mji wa Tripoli. Anasema alibakwa ovyo-ovyo, kupigwa na kudhalilishwa kwa utaratibu wa takribani kila siku na kushuhudia udhalilishaji unaofanana na huo kwa wasichana na wavulana wengine. Stori yake na nyingine za wengine ambao wanasema walibakwa na dikteta huyo zinasimuliwa kwenye kitabu cha "Gaddafi's Harem: The Story Of A Young Woman And The Abuses Of Power In Libya" kilichoandikwa na mwandishi wa kimataifa wa Ufaransa Annick Cojean. Kitabu hicho kimeshauza zaidi ya nakala 100,000 tangu kilipochapishwa nchini Ufaransa mwaka jana na tafsiri ya Kiingereza itaku...