NICK MBISHI ATANGAZA RASIMI KUWA YEYE NI MUATHIRIKA WA UKIMWI
Tumekuwa tukishuhudiwa vituko mbalimbali vya wasanii wetu ambao wamekuwa wakihangaika usiku na mchana kuusaka umaarufu....
Wapo ambao wamekuwa wakivua nguo zao jukwaani, wapo ambao wamekuwa wakipiga picha za uchi na kuzitupia mitandaoni.Yote hiyo ni kutafuta Jina au umaarufu ambao mimi binafsi nauita ni umaarufu wa kishamba.....
Leo Nick Mbishi ametoa kituko ambacho kimenifanya niamini kuwa wasanii wetu wana njia mpya kwa sasa za kutaka kujulikana ( kuwa maarufu).
Katika account yake ya Twitter, Nick Mbishi alitoa post moja ikielezea kuwa yeye ni muathirika wa ukimwi.
Post hiyo ilikuwa na taswira mbili za mafumbo . Fumbo la kwanza linamaanisha kuwa Yeye NI mwathirika wa UKIMWI huku fumbo la pili likimaanisha kinyume chacke.
Baada ya post hiyo, mijadala kadhaa ya watu iliibuka kwenye mitanado ya jamii.Wapo waliompa pole na wapo waliompongeza kwa ujasiri wake...
Cha kushangaza ni kwamba, baada ya Nick kuona kuwa issue imekuwa serious kuhusu madai ya yeye kuwa na UKIMWI, alirudi tena Twitter na kuanza kuilaumu mitandao ya kijamii....
Kinachonishangaza ni kwamba, Nick anakaumu nini wakati alitamka mwenyewe??.Hizo ni sifa za kishamba za kutaka jamii ikuongelee na kukujadili...
Kama umeamua kujitangaza, basi kuwa serious ili watu wajue moja.
Hii ndo post yake.
Comments
Post a Comment