Baada ya Ney wa Mitego kumchana, Madam Ritta ampa big up na kumkaribisha ku-perfom kwenye fainali za BSS

Madam Rita: Usiruhusu mtu akuamulie maisha yako!
Kupitia U Heard na Gossip Cop leo, madam Ritta aongea juu ya tetesi kuwa yupo katika mipango ya kumfungulia mashtaki Ney na kumdai shilingi millioni 500 pamoja na ku-record album nzima kwa kumsafisha jina lake baada ya kumchafulia.

Madam Ritta: nani amesema hivyo, sio kweli na wala sina mda huo na sidhani hata kama ningefanya hivyo anaweza aka, mia tani kidogo ,kwahiyo i dont have time kwa vitu ambavyo havina faida na mimi, ingekuwa anazo na uwezo huo labda  ningefanya hivyo kwasababu time is money, kwahiyo muda wangu kwenda kushtakiana kwa vitu ambavyo haviwezi kunifikisha popote , sina mda huo na sijafanya hivyo kwanza nashangaa nani amesema hiyo, sia mda huo sijaenda polisi , sina hata, hata simjui, hata simfikirii yaani.
Gossip Cop: aaaaaah hivi lile songi umelisikiliza Ney wa mitego alivyokuchana .
Madam Ritta: huto wimbo naufaham hata kabla hajarecord
Gossip Cop: Duuh madam we nomaaa, ehe ilikuaje kuaje ukaijua kabla haijatoka??
Madam Ritta: nipo kwenye industry ya entertainment remember? kuna mtu ambae hanijui mimi hapa Tanzania hii
Gossip: na kweli, lakini Madam Ritta ile samansi kwa Ney alipelekewa lini ile, naskia alikataa kuipokea??
Madam Ritta: ha ha hahaa, nimeshakwambia sina muda wa vitu ambavyo sina faida navyo, kwanza hiyo kwenda kufanya ni gharama pia ni muda, kwahiyo muda kwangu ni very very imporyant, angekuwa anaweza kuwa na hizo hela ningeacha vitu vingine nikaifanyia kazi, lakini  hawezi kunilipa na uwezo huo hana, kwahiyo amejipatia fursa ya kujipandisha, labda kutumia kuandika hivyo na kuimba hiyo nyimbo anaweza kubadilisha maisha yake, yote kheri, ameona furasa atumie kuwaongelewa watu hivyo labda itaweza kumsogeza mbele, na kama haita msogeza mbele mi nitapata thawabu.
Gossip: na kweli, ila Ney wa mitego hivi alifaham faham vipi kwamba washindi wa BSS hawapatagi mitonyo yao ya millioni 50
Madam Ritta: Sikiliza mimi hata huu mda nilioongelea hicho kitu ni wast of time, kwahiyo mi naomba tumalizie hapo kwasabau he is not worth my time, hata mimi kumtaja jina lake mimi nakua nimemuongezea nanii, kwahiyo basically nimeongea hivyo ulivyoniuliza na staki kupoteza muda wangu kumuongelea mtu ambae hana faida na mimi 
Gossip: Madam samahani lakini hivi anaitwa nani yule jamaa?
Madam Ritta: mimi simjui hahahahahahaaaaaaaa
Gossip: nani wa mitego??
Madam Rittah: hahahaaaaaa simjui hahahaaaa kusema ukweli mimi simjui nikwambie ukweli, simjui mtu anaitwa nini sijui nini  ndo hivyo unaona, lakini ukizangatia sasa nimeshamjua, amefanya na mimi nimjue pia sooo yaaah he is creative, big up to him big up, he is creative young man.
Gossip: Unaonaje akija ku-perfome kwenye fainaliza BSS
Madam Rittah: aje ata-perfome, tena a-perfom wimbo huo huo, kwenye fainali nimesham-book ye ndio ata-perfom wa kwanza kabisa, unaona eeeh, yaani anakaribiswa kuperfom kabisa, sisi tupo hapa kubadilisha maisha ya vijana

Comments

Popular posts from this blog