MALI ZA VIGOGO HAWA WA MADAWA YA KULEVYA ZAKAMATWA


VIGOGO 111 wanaosadikiwa kujihusisha na biashara yharamu ya madawa ya kulevya nchini wameanza kuonja 'joto ya jiwe' kufuatia Jeshi la Polisi Tanzania Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kukamata mali zao, .

 
Kamanda Nzowa.

Kwa mujibu wa vyanzo makini ndani ya jeshi hilo, pia vigogo wengi wanaojihusisha na biashara hiyo  walikamatwa na kiasi kikubwa cha ‘unga’ ndani ya kipindi cha miaka minne iliyopita.
Kuhusu mali ambazo ni magari, ilidaiwa kuwa kufuatia taarifa zilizowataja wauza unga, jeshi la polisi liliamua kushikilia magari hayo na kufanya uchunguzi wa uhalali wake.
“Kuna watu walitajwa majina, wakafuatiliwa, magari yao yakakamatwa na kufanyiwa uchunguzi, lakini cha kushangaza baadhi yao  wameingia mitini na kutelekeza magari yao,” kilisema chanzo.
Chanzo kilisema baadhi ya magari hayo ni Mercedes Benz, Jeep, Toyota Spacio, Toyota Galsira, Toyota Mark II, Nissan Patrol 4x4 GL, Toyota Land Cruiser na Toyota Prado. 
Uwazi lilifanikiwa kunasa majina ya vigogo waliokamatwa wakiwa na unga  na kiasi walichokamatwa nacho.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika mahakama mbalimbali nchini na ndani ya jeshi la polisi umebaini kuwa, kesi za watuhumiwa hao zinaendelea kuunguruma kortini  japokuwa kasi yake si ya kuridhisha.
source: global

Comments

Popular posts from this blog