Posts

MTV EMA Wampokonya Tuzo Wizkid na Kumpa Alikiba

Image
IKIWA ni siku chache baada ya waandaaji wa Tuzo za MTV EMA 2016 kutoa tuzo hizo na kumtangaza msanii wa Nigeria Wizkid kuwa ndiye mshindi wa Best African Act na Worldwide Act ambapo katika kipengele hicho alikuwa akichuana na msanii wa Tanzania, Ali Kiba. Waandaaji hao wamempokonya Wizkid tuzo hiyo kwa madai kuwa hakustahili na kumpa Ali Kiba ambaye wamesema alistahili kushinda. Siku chache zilizopita baada ya Wizkid kushinda tuzo hiyo, kulitokea sintofahamu huku mashabiki wa kiba wakiponda mchakato mzima wa utoaji tuzo huo ambapo website ya MTV EMA ilionesha kura zilionesha kuwa ni Alikiba ndiye aliyeshinda. MTV EMA kupitia akaunti yao ya twitter wamethibitisha kumpa ushindi huo Alikiba ambapo yeye ameupokea kwa furaha sambamba na mashabiki wake. Amesema baada ya mashabiki wake kulalamika kuhusiana na mkanganyiko huo, MTV EMA walifuatilia na kukiri kuwa na makosa na kuutumia ujumbe uongozi wake kuwa Alikiba ndiye mshindi halali, na sio Wizkid. “Sasa ndio nim

Rais Obama Amualika Donald Trump Ikulu Leo

Image
  Rais Barack Obama wa Marekani  amempongeza Rais Mteule wa taifa hilo, Donald Trump na kumualika Ikulu kujadiliana juu makabidhiano ya ofisi. Maelfu waandamana kupinga ushindi wa Trump Kumekuwa na maandamano ya kupinga ushindi wa Donald Trump kutoka katika miji mbalimbali nchini Marekani. Maelfu ya raia kwa sasa wamekusanyika nje ya mnara maarufu kama Trump Tower mjini New york wakipaza sauti zao kuhusu sera za uhamiaji,mapenzi ya jinsia moja na haki ya uzazi yanayopingwa na Donald Trump. Wanasema hata dunia ina wasiwasi juu ya ushindi wa urais.

MAJALIWA APOKEA MSAADA WA MAAFA YA TETEMEKO LA KAGERA KUTOKA KWA BALOZI WA KUWAIT NCHINI

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Novemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya dola za Marekani 33,000 kutoka kwa balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyka ofisini kwa Waziri Mkuum bungeni mjini Dodoma Novemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Novemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya dola za Marekani 33,000 kutoka kwa balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem ukiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyka ofisini kwa Waziri Mkuum bungeni mjini Dodoma Novemba 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Jaji Mutungi Avifutia Usajili Vyama Vitatu vya Siasa Nchini

Image
DAR ES SALAAM: Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi leo amevifutia usajili wa kudumu vyama vitatu vya siasa kwa makosa mbalimbali.  Vyama hivyo vilivyofutwa ni pamoja na Chama cha Haki na Ustawi wa Jamii (CHAUSTA) kinachoongozwa na  James Mapalala, Chama cha The African Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo)  kinachoongozwa na Peter Kuga Mziray na Chama cha Jahazi Asilia kilichokuwa kinaongozwa na Kassim Bakari Ally. Akiongea na wanahabari leo, Jaji Mutungi amesema amevifuta vyama hivyo kwa kutumia kifungu cha 19 cha sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992.    Jaji Mtungi ameongeza kuwa, mchakato wa kufuta usajili wa vyama hivyo unatokana na zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa mengine ya sheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu lililofanyika kuanzia Juni 26  hadi Julai 2016. Katika zoezi hilo la uhakiki ilibainika kuwa vyama tajwa hapo juu vimepoteza sifa za usajili wa kudumu kwa kuki

Rais Magufuli, Nkurunzinza Wampongeza Donald Trump kwa Kushinda Urais wa Marekani

Image
  Leo November 9, 2016 Marekani imeweka historia nyingine baada Donald Trump wa Chama cha Republican kutangazwa mshindi wa kiti cha Urais, na tayari ameanza kupokea pongezi kutoka kwa viongozi wa nchi mbalimbali ikiwemo Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ni miongoni mwa viongozi waliompongeza Donald Trump kupitia Twitter.   Rais Magufuli ametoa pongezi zake kwa Rais Donald Trump kupitia ukurasa wake Twitter Congratulation President-Elect and people of America for a democratic election,I assure and people of Tanzania for a continued friendship. — Dr John Magufuli (@MagufuliJP) November 9, 2016 Nkurunziza ampongeza Trump Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema ushindi wa Trump ni ushindi wa Wamarekani wote. Mr. @realDonaldTrump , on behalf of the people of Burundi, we warmly congratulate you. Your Victory is the Victory of all Americans. — Pierre Nkurunziza (@pnkurunziza) November 9, 2016 Tupia

Trump Ashinda Urais wa Marekani, Clinton Akubali Matokeo

Image
MAREKANI: Mgombea Urais wa Chama cha Republican, Donald Trump ameshinda kiti hicho. Trumpa ambaye mpaka sasa ana kura 288 huku Hillary Clinton akiwa na kura 218 za wajumbe kati ya kura zote 538. Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Mshindi wa urais alitakiwa kushinda angalau kura 270 kati ya hizo 538 lakini Bw. Trump amevuka na kufikisha kura 279 mpaka sasa. Clinton akubali kushindwa CNN na NBC wameripoti kwamba mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton amempigia simu Donald Trump na kukubali kushindwa. Shangwe kambi ya Trump Shangwe, nderemo na vifijo zimetanda miongoni mwa wafuasi wa Donald Trump. Trump: Asanteni sana Trump amepanda jukwaani Manhattan, New York. Amewashukuru wafuasi wake na kusema amepigiwa simu na Hillary Clinton “kuwapongeza”. Akizungumza na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi, Trump amewataka raia wote wa Marekani, waliomchagua na ambao hawakumchagua kuungana na kuanza kuijenga nchi yao kwani muda wa kampeni na siasa za kugawan

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA BODI YA TANAPA JENERALI GEORGE WAITARA NA MKUU WA JKT BRIGEDIA JENERALI MICHAEL ISAMUHYO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANAPA  ambaye pia Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara alipokutana naye kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Oktoba 8, 2016. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Michael Isamuhyo alipokutana naye kwa mazungumzo   Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Oktoba 8, 2016. Picha na IKULU

BREAKIN NEWZZ!!:- MSIBA MWNGINE MZITO WA TAIFA HUU HAPA WAZIRI WA ZAMANI AFARIKI DUNIA MUDA MCHACHE ULIOPITA GHAFLA!!

Image
Aliyewahi kuwa Waziri mwandamizi katika wizara mbalimbali, ikiwemo Wizara ya Elimu, Ndg.Joseph Mungai, amefariki dunia jioni ya leo, katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokua akipatiwa matibabu. Mungu ampumzishe kwa amani.! Posted by BONGO YETU at Tuesday, November 08, 2016 Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Pinterest

Wezi Watokomea na Mashine ya ATM Ikiwa na Pesa

Image
NAIROBI: Polisi jijini Nairobi nchini Kenya wamemkamata mlinzi wa Benki ya Equity kuhusiana na tukio la wizi lililotokea Jumamosi iliyopita ambapo watu wanaoaminika kuwa ni wezi waliiba mashine ya kielektroniki ya kutolea pesa, Automatic Teller Machine (ATM) pamoja na pesa taslim ambazo hazijafahamika kiasi chake. Wezi hao walichimba ukuta wa nyuma wa Benki hiyo na kutoweka na sanduku la uhifadhi wa pesa pamoja na mtambo wa ATM, pesa zikiwa ndani. Wakati wakitekeleza tukio hilo, washukiwa waliweza kuzima kamera za CCTV na pia kengele ya usalama kabla ya kutekeleza adhma yao ya kuiba mashine na pesa hizo. Akizungumza na wanahabari, Kamanda wa Polisi wa Jimbo la Nairobi, Japheth Koome amesema kwamba polisi waliweza kupata mitungi ya gesi na vifaa vingine ambavyo hutumuka kukata chuma. Alipoulizwa kama wezi siku hizi wamepata maarifa na mbinu nyingi kama wacheza filamu, alisema kwamba kwa siku za hivi karibuni matukio ya wizi kwenye mabenki yanazidi kuongezeka na

SAKATA LA DIVA NA JOKATE KIDOTI KWA ALI KIBA,MAPYA YAIBUKA,GIGY MONEY AFUNGUKA

Image
Mwanadada Diva aliweza ku tweet kuhusiana na uwezo wa alikiba katika kuimba na kumalizia kuwa “Girlfriend anakutia gundu” kitu ambacho wengi walijiuliza inamaana Jokate (Kama inavyo julikana kuwa ndiye wa Kiba) kuwa anamtia gundu? Leo Mrembo Gigy_Money amejitokeaza na kupost picha hii hapa chini na kuandika maneno ya kumtetea Jokate: "Honestly jojo wangu mtoto classic uyu 😍wache waseme unagundu ila mwisho wa siku watakuelewa tu kwa mafanikio yako hadi unafikia umri wao yani we utakua Michael Jackson wa kike unajituma mwaya #USIFORCETUFANANE #HATUFANANI" Gigy Mone y

Makonda Kujenga Vituo 20 Vya Kisasa Vya Polisi Dar

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi Kituo cha Polisi cha Tandika, Dar. ..Maongezi yakiendelea katika Kituo cha Polisi cha Tandika. Makonda akizungumza na mmoja wa mahabusu alipotembelea vituo vya polisi.   Kituo cha Polisi Kigogo, Dar. Muonekano wa Kituo cha Polisi Traffic Mwenge, Dar. Tangu kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi na taarifa za changamoto zifuatazo kuhusu hali ya huduma za kipolisi mkoani kwake;- 1. Wananchi kutokupatiwa huduma kwa saa 24 kutokana na vituo hivyo kufungwa usiku. 2. Mazingira mabovu na yasiyoridhisha ya vituo vya polisi. 3. Polisi kutofika kwenye matukio kwa wakati pindi wapigiwapo simu na wananchi. 4. Polisi kushindwa kutoa huduma kutokana na upungufu wa askari polisi. 5. Majambazi kuvamia vituo vya polisi wakiwa na lengo la kuchukua silaha. Changamoto hizi za msingi na ambazo zinahatarisha uhakika wa usalama wa raia wa Dar es

ALICHO ANDIKA MBUNGE TUNDU LISSU KUHUSU KIFO CHA SAMMUEL SITTA

Image

YANAYOENDELEA KUJIRI NYUMBANI KWA MAREHEMU SAMUEL SITTA

Image
 Mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akisaini kitabu cha maombolezo, wakati alipofika nyumbani kwa Marehemu Mh. Samuel Sitta aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani. Msiba upo Nyumbani kwa Marehemu, Masaki jijini Dar es salaam.  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akiwa katika mazungumzo na baadhi ya viongozi pamoja ndugu wa Marehemu Mh. Samuel Sitta aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akisaini kitabu cha Maombolezo cha aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani. Sehemu ya ndugu wa Marehemu wakiwa nyumbani hapo.

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Samwel Sitta samwel-sittaaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Spika Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo lililopo Mkoani Tabora Mhe. Samwel Sitta. Mhe. Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita. Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Samwel Sitta na kwamba Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo. “Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na Serikali. “Kupitia kwako Mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa Marehemu Mhe. Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Urambo na familia nzima ya marehemu, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi wa Urambo Mkoani Tabora na watu wote walioguswa na msiba huu” amesema Rais Magufuli katika salamu hizo. Dkt. Magufuli amesema anaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na amewaombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu. “Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Ameni” Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam 07 Novemba, 2016

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Spika Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo lililopo Mkoani Tabora Mhe. Samwel Sitta.   Mhe. Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.   Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Samwel Sitta na kwamba Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.   “Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na Serikali.   “Kupitia kwako Mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa Marehemu Mhe. Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Jimb

Tanzia: Spika Samwel Sitta Afariki Dunia

Image
  DAR ES SALAAM : Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu, Samuel Sitta (74) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani. Mtoto wa marehemu, Benjamin Sitta amesema baba yake amefariki saa 10:00 usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani. ‘’Nikweli mzee amefariki nchini Ujerumani akiwa anapatiwa matibabu, alipelekwa Alhamisi iliyopita na alikuwa anasumbulia na saratani ya tezi dume ambayo ilisambaa na kuathiri miguu na mwili mzima. Benjamin amesema kuwa taarifa za mipango ya kusafirisha mwili zitatolewa baadaye. Sitta aliyezaliwa Desemba 18, 1942, alikuwa Spika wa Bunge tangu mwaka 2005 baada ya kustaafu kwa aliyekuwa spika wa Bunge hilo, Pius Msekwa, hadi mwaka 2010 na pia Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, Tabora. Mwaka 2010, aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki cheo alichokitumikia hadi hadi mwaka 201

Afrima Awards: Diamond Platnumz Anyakua Tuzo 3

Image
Lagos, Nigeria: Diamond Platnumz ameibuka na ushindi wa nguvu kwenye tuzo za Afrima 2016 zilizotolewa Jumapili hii jijini Lagos, Nigeria. Muimbaji huyo ameshinda tuzo tatu, Song of The Year – Utanipenda, Best Artist/Duo/Song Of The Year Utanipenda na Best Male Artist in Eastern Africa. Pamoja na ushindi huo, Diamond pia alitumbuiza wimbo alioimba na Papa Wemba, msanii aliyetunukiwa tuzo ya heshima. Wasanii wengine waliotumbuiza ni pamoja na Patoranking, P-Square, Falz, Eddy Kenzo, Avril, Simi, Darey, Phyno, Seyi Shay na wengine. Chini ni orodha ya washindi kwenye tuzo hizo pamoja na picha za ndani ya ukumbi na red carpet: Artist of the Year  Wizkid Song of The Year Utanipenda – Diamond Album of the Year Ahmed Soultan Revelation of the year Falz Video of the Year Dogo Yaro – Vvip Best African Collaboration Eddy Kenzo ft Niniola – Mbilo Mbilo (Remix) Best African Group VVip Best African Jazz Jimmy Dludlu Best Artist/Duo/Song Of The Year  Diamond –