MTV EMA Wampokonya Tuzo Wizkid na Kumpa Alikiba
MTV EMA kupitia akaunti yao ya twitter
wamethibitisha kumpa ushindi huo Alikiba ambapo yeye ameupokea kwa
furaha sambamba na mashabiki wake.
Amesema baada ya mashabiki wake
kulalamika kuhusiana na mkanganyiko huo, MTV EMA walifuatilia na kukiri
kuwa na makosa na kuutumia ujumbe uongozi wake kuwa Alikiba ndiye
mshindi halali, na sio Wizkid.
“Sasa ndio nimepata confirmation kwamba
ni kweli tuzo inakuja Tanzania na vile vile mimi siwezi kuzungumzia,
nitasubiri mpaka nizishike,” amesema Kiba.
Muimbaji huyo amedai kuwa habari hizo
amezipokea kwa furaha kubwa na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha
kushinda na kuwa nyuma yake.
Wakati hup huo Kiba amempongeza Wizkid
kwa ushindi wa tuzo nyingine ya Afrima. Kwa upande wa Wizkid, tayari
amefuta post zote za Instagram alizokuwa ameweka kushangilia ushindi
huo.
WALICHOKIANDIKA MTV EMAUSHINDI WA WIZKID
Comments
Post a Comment