Makonda Kujenga Vituo 20 Vya Kisasa Vya Polisi Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi Kituo cha Polisi cha Tandika, Dar.
Makonda akizungumza na mmoja wa mahabusu alipotembelea vituo vya polisi.
Kituo cha Polisi Kigogo, Dar.
Muonekano wa Kituo cha Polisi Traffic Mwenge, Dar.
Tangu kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi
na taarifa za changamoto zifuatazo kuhusu hali ya huduma za kipolisi
mkoani kwake;-
1. Wananchi kutokupatiwa huduma kwa saa 24 kutokana na vituo hivyo kufungwa usiku.
2. Mazingira mabovu na yasiyoridhisha ya vituo vya polisi.
3. Polisi kutofika kwenye matukio kwa wakati pindi wapigiwapo simu na wananchi.
4. Polisi kushindwa kutoa huduma kutokana na upungufu wa askari polisi.
5. Majambazi kuvamia vituo vya polisi wakiwa na lengo la kuchukua silaha.
1. Wananchi kutokupatiwa huduma kwa saa 24 kutokana na vituo hivyo kufungwa usiku.
2. Mazingira mabovu na yasiyoridhisha ya vituo vya polisi.
3. Polisi kutofika kwenye matukio kwa wakati pindi wapigiwapo simu na wananchi.
4. Polisi kushindwa kutoa huduma kutokana na upungufu wa askari polisi.
5. Majambazi kuvamia vituo vya polisi wakiwa na lengo la kuchukua silaha.
Changamoto hizi za msingi na ambazo
zinahatarisha uhakika wa usalama wa raia wa Dar es Salaam na mali zao
ndizo hasa zimemsukuma Makonda jana kufanya ziara maalum ya kutembelea
baadhi ya vituo vya polisi ili kujionea hali halisi, ambapo baada ya
ziara hiyo pamoja na mengineyo amebaini kuwa kuna ulazima wa kujenga
vituo vikubwa zaidi vya kisasa, vinavyoweza kuhudumia wananchi wengi
zaidi na kwa wakati, vilivyounganishwa na huduma za kisasa za
mawasiliano na utunzaji kumbukumbu na vinavyoweza kutumiwa na idadi
kubwa zaidi ya polisi akiamini kuwa ujenzi huu una maana kubwa katika
kuzalisha majawabu ya sehemu kubwa ya changamoto zilizotajwa.
Kwa sababu hiyo, Makonda ametangaza
kuanza mchakato wa ujenzi wa vituo 20 vya polisi vitakavyogharimu jumla
ya Shilingi Bilioni 10 ikimaanisha ya kwamba kwa kila kituo zitatumika
shilingi milioni 500 pesa ambazo mkuu wa mkoa anapanga kufanya
mazungumzo maalum na wadau wa maendeleo wa mkoa wake ili wamchangie sawa
kabisa na namna alivyopambana kupata pesa za kutekeleza miradi mikubwa
inayoendelea kutekelezwa mkoani kwake, ikiwemo ujenzi wa wodi tatu za
kisasa, Makao Makuu ya BAKWATA na majengo ya emergencies hospitalini,
miradi ambayo inagharimu zaidi ya shilingi bilioni 25 za Kitanzania,
fedha ambazo hazitoki kwenye mfuko wa serikali bali kwa wadau wanaounga
mkono utendaji wa Makonda unaoyapa kipaumbele maslahi ya wananchi wa Dar
kwa ukubwa wake.
Kwa kuwa Mkoa wa Dar es Salaam
umegawanyika katika wilaya tano, kwa kila wilaya vitajengwa vituo 4 na
kila kituo kitakuwa na ofisi za kisasa, vyumba vitatu vya mahabusu
(kimoja cha wanaume, kingine cha wanawake na cha tatu ni kwa ajili ya
wale wenye mahitaji maalum), chumba cha mahojiano, vyumba vya silaha,
idara ya usalama barabarani (traffic), mapokezi, dawati la jinsia na
ofisi za teknolojia ya mawasiliano (ICT sections), kwa ukubwa wake kituo
kimoja kitatumiwa na idadi ya askari wasiopungua 100.
Makonda amezitaka Kamati za Ulinzi na
Usalama za Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam wapeleke mchanganuo wa maeneo
ambayo vituo hivyo vitajengwa ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma
za ulinzi na usalama za uhakika na kwa wakati wote kwa lengo la
kudumisha amani na utulivu katika mkoa wetu wa Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment