BIBI HARUSI APEWA TALAKA SAA CHACHE BAADA YA NDOA

Mwanaume
mmoja ameamua kumtalakisha mkewe saa chache baada ya kufunga ndoa,
kwasababu mkewe huyo mpya alitumia usiku wao wote wa ‘fungate’ kuchat na
rafiki zake.
Kwa
mujibu wa gazeti la Al Watan la Saudi Arabia, bibi harusi huyo alikuwa
busy akipokea salamu za pongezi kutoka kwa rafiki yake akimsahau mumewe
aliyenaye chumbani muda huo.“Bwana harusi alijaribu kusogea karibu naye
na kimahusiano, lakini alishitushwa kuona mkewe anampotezea, hajibu
anachoulizwa au hata kuonesha vitendo,” ndugu wa Bwana harusi aliiambia
Al Watan.
“Mwanaume
alipomuuliza kama rafiki zake ni muhimu kuliko yeye, alimjibu ndio,”
walisimulia mkasa walioelezwa na bwana harusi.Mahakama ya mwanzo katika
eneo hilo imejaribu kuwasuluhisha ili waendelee na ndoa yao, lakini
mwanaume ameendelea kushikilia msimamo wake wa talaka.
Comments
Post a Comment