Wenye Vyeti FEKI Kulipwa Mafao Yao

Watumishi waliobainika na vyeti feki, watalazimika kusubiri mafao yao hadi utaratibu wa kuwalipa utakapofanyika.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Amina Mollel.

Amina alitaka kujua ni hatua gani zitachukuliwa ili kuwalipa mafao yao wafanyakazi waliobainika na vyeti feki.

Waziri Kairuki alisema, ofisi yake itaandaa utaratibu wa mafao ya wafanyakazi hao na pindi utakapokamilika, watajulishwa na kulipwa haki zao.

Aidha,  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu, Anthony Mavunde, alisema kwamba seeikali inaendelea na mchakato wa kuunganisha mifuko ya jamii.

Mavunde alisema hayo alipojibu swali la msingi la Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Almas Maige, aliyetaka kujua mchakato wa kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii, umefikia hatua gani.

Mavunde alisema, serikali kwa sasa inafanya tathmini ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo imetoa mapendekezo kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatiwa katika mchakato wa kuunganisha mifuko hiyo.

Alisema, wadau vikiwemo vyama vya waajiri, vimeshirikishwa ili kutoa maoni na mapendekezo kwa serikali na kutoa maamuzi.W

Comments

Popular posts from this blog