Picha: Treni ya Abiria Yapata Ajali, Morogoro
MOROGORO: Treni ya abiria
iliyokuwa inakwenda Bara imepata ajali usiku wa kumakia leo majira ya
saa 5:25 katika eneo la Stesheni ya Mazimbu mkoani Morogoro.
Katika ajali hiyo ilihusisha mabehewa saba ambapo manne yakiwa yameegama na matatu yameacha reli.
Abiria mmoja, Ashura Mrisho aliyekuwa anasafiri kwenda Tabora amepata maumivu baada ya kuangukiwa na mizigo iliyokuwamo ndani ya moja ya mabehewa hayo.
Mabehewa 13 yamerejeshwa Morogoro kuwapangia usafiri mbadala abiria waliokuwa wakisafiri na treni hiyo.
Aidha Shirika la Reli Tanzania (TRL) linafanya utaratibu wa kuwasafirisha abiria wa bara kwa mabasi hadi Kijiji cha Lukobe Manispaa ya Morogoro ambapo watapanda treni kwenda bara.
Kuhusu wale wa treni ya kuja Dar es Salaam kutoka bara ambayo itasimama Lukobe, watasafirishwa kwa mabasi kurudi Morogoro kuendelea na safari.
Taarifa zaidi zitafuata wakati uongozi wa TRL, mafundi na wahandisi wakishughulikia ajali hiyo.

Comments
Post a Comment