BALOZI DK.MAHIGA AKABIDHIWA MAGARI NA SERIKALI YA KUWAIT
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Dk. Augustine Mahiga amepewa msaada wa magari kutoka serikali ya Kuwait ilikuweza kusaidia katika shughuli mbalimbali za kiutendaji.Balozi Mahiga amesema hayo wakati akipokea msaada wa magari kwa ajili ya wizara yake amesema wizara yake sio yenye tatizo ya usafiri bali ni suala wizara mbalimbali na taasisi zingine za serikali .Amesema serikali ya Kuwait inatoa msaada katika serikali ya Tanzania zaidi ya dola za kimarekani milioni 200 kwa kila mwaka.Balozi Mahiga amesema ubalozi wa Kuwait nchini amekubali kusaidia magari kwa sekta zingeni kwa kutaka kuorodhesha mahitaji ya usafiri ili kuweza kusaidia serikali ya Tanzania Kiutendaji.
Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu kukabidhiwa magari kutoka ubalozi wa Kuwait nchini leo Jijini Dar
es Salaam.
Balozi wa
Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhii magari yenye thamani ya
dola za Kimarekani 100,000 leo jijini Dar es Salaam.picha zote na
Emmauel Massaka,Glob ya Jamii.
Balozi wa
Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi funguo za Magari kwa Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika hafla iliyofanyika leo jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiteta jambo na Balozi wa Kuwait
nchini, Jasem Al-Najem
Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem
Al-Najem wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa wizara hiyo.
Comments
Post a Comment