MKUTANO WA USHIRIKIANO WA VYOMBO VYA HABARI KATI YA NCHI ZA AFRIKA NA CHINA UNAOFANYIKA MJINI BEIJING CHINA
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akieleza jinsi Tanzania ilivyofanikiwa kuhama kutoka mfumo wa urushaji wa matangazo ya Televisheni kutoka Analogia kwenda Digitali katika mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (Kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel wakiwa katika ukumbi wa mikutano leo kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Star Media Tanzania Liao Lanfang wakibadilishana mawazo leo kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
Mkutano wa Ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya nchi za Afrika na China ukiendelea mjini Beijing nchini China.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Zamaradi Kawawa wakibadilishana mawazo leo kabla ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
Picha na Mpigapicha wetu
Comments
Post a Comment