Siwema amuumbua Nay
NA MUSA MATEJA, RISASI MCHANGANYIKO
SIKU chache baada ya mzazi
mwenzake na msanii Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego,’ Siwema Edison
kutoka gerezani na kutakiwa atumikie kifungo cha nje, amefunguka ya
moyoni huku akimuumbua ‘zilipendwa’ wake huyo aliyekuwa akidai
alipambana kumsaidia.
Chanzo makini cha habari hii kilitutonya
hivi karibuni kuwa, mbwembwe zote alizokuwa akizitoa Nay kuwa yeye
ndiye kila kitu mpaka Siwema akarejea uraiani, si za kweli na
zimemuumiza msichana huyo, kwani hakufanya chochote kumsaidia kwenye
janga hilo.
“Siwema analalamika sana, anaumizwa na
majigambo ya Nay kuwa jitihada zake ndiyo zimemrejesha uraiani kitu
ambacho si cha kweli. Ndugu wa Siwema walikuwa ndiyo kila kitu
kufanikisha mtoto wao anaondoka kwenye majanga hayo, sasa hata
haieleweki kwa nini Nay ameamua kuongea uongo kiasi hicho kwenye
‘midia’,” kilifu-nguka chanzo hicho.
Baada ya gazeti hili kunasa ‘ubuyu’ huo,
lilimtafuta Siwema aliyehukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la
kujipatia pesa kwa njia ya vitisho kutoka kwa kigogo mmoja,
alipopatikana alifunguka kama ifuatavyo:
“Dah! Kweli hivi vitu vinaniumiza sana.
In short (kwa kifupi) sitaki kumzungumzia sana Nay maana ni mzazi
mwenzangu tayari ila nashangaa anavyozungumza kuwa amenisaidia wakati si
kweli.
“Kiukweli walionisaidia na kunipigania
ni ndugu zangu na mpaka leo nipo hapa. Ninachokumbuka kuhusu Nay najua
alikutanaga na rafiki yangu, akampa laki tatu kwa ajili ya kunisaidia
nikiwa gerezani, basi.”
Msikie Nay
Alipotafutwa Nay kuzungumzia habari hiyo
alisema: “Kwa namna moja ama nyingine, sitaki kuzungumzia chochote,
Mungu ndiye anayejua ukweli wote na kama wanasema mimi sikushiriki
kumsaidia basi naomba radhi kwa hilo. Nisamehewe!”
Siwema yuko huru kabisa?
Risasi Mchanganyiko lilichimba
zaidi kuhusiana na kutoka gerezani kwa Siwema ambapo ilibainika kuwa,
yuko kifungo cha nje huku akifanya shughuli za kijamii kwenye kituo
kimoja cha afya kilichopo Mwanza.
“Siyo kwamba nipo huru kabisa, hapana.
Huku Mwanza kuna sehemu naweza kusema ni kituo cha afya huwa nahudhuria
kwa ajili ya kuripoti na kutimiza masharti ya kutumikia kifungo cha nje,
naweza kukwambia hivyo kwa sasa,” alisema Siwema.
Comments
Post a Comment