Posts

BREAKING: SANGA ATANGAZA RASMI KUACHIA NGAZI YANGA

Image
Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake katika klabu hiyo. Sanga amejiuzulu wadhifa huo kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri baina yake na viongozi wenzake ndani ya klabu hiyo ikiwemo wale wa Kamati ya Utendaji kueleza hana ushirikiano mzuri. Kiongozi huyo aliyekuwa akikaimu nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, alikuwa akitupiwa lawama na viongozi wa Kamati ya Utendaji akiwemo Khalfan Hamis ambaye amejiuzulu juzi akidai Sanga amekuwa si mweledi wa mambo. Mbali na kukosa maelewano, Sanga ameeleza kuwa kuna CLIP ameiona mitandaoni inayohamasisha watu kumvamia kwa mapanga ni moja ya sababu zilizopelekea kufanya uamuzi wa kuachia ngazi. Aidha,wiki kadhaa zilizopita Mjumbe mwingine kutoka kamati hiyo, Salum Mkemi naye aling’atuka kuendelea na wadhifa huo ndani ya Yanga na akisalia kuwa mwanachama pekee kutokana na kutokuwa na kukosa maelewano mazuri baina yake na wanachama wa klabu. Ukiachana na Sanga, Kati...

Rais Magufulia atoa agizo kwa Mkandarasi Daraja la Salender

Image
Rais John Magufuli amemuagiza Mkandarasi aliyepewa kazi wa kujenga daraja kubwa la Selander Bridge kutoka Coco Beach mpaka Agha Khan litakalogharimu shilingi bilioni 250 kwa ufadhili wa Serikali ya Korea kusini kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ndani ya miezi 36 aliyopangiwa  kufanya kazi. Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kushuhudia mkataba wa utiaji saini ujenzi wa darala hilo ambalo litakuwa na urefu wa kilomita 6.23 mbele ya Waziri Mkuu wa Korea Kusini Mh.0 Lee Nak-Y eon Ikulu jijini Dar es Salaam na kusema kukamilika kwa daraja hilo kutaendelea kubadilisha taswira mpya ya Jiji la Dar es Salaam katika miundombinu ya barabara. Katika tukio jingine, hivi sasa Rais Magufuli anapokea gawio la kipindi cha mwaka 2017/18 kutoka Wakala, Kampuni, Taasisi na Mashirika ya Umma 47 ambayo Serikali inamiliki hisa.

Tanga: Diwani wa CUF Avuliwa Udiwani kwa Kutofika Vikaoni

Image
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imemuondoa kwenye nafasi yake, Diwani wa Kata ya Ngamiani Kusini, Mussa Mbarouk,  ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, baada ya kupoteza sifa kwa kutohudhuria vikao sita mfululizo. Kata hiyo sasa imetangazwa kuwa wazi. You May Like

Madiwani wapita bila kupingwa Uchaguzi mdogo wa Udiwani- Mbulu.

Image
  Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbulu ndugu Hudson S. Kamoga akisoma taarifa ya maamuzi ya rufaa za Wagombea Udiwani katika kata za Tumati na Hayderer . Akiongea na vyombo vya habari hii leo ofisini kwake Msimamizi wa Uchaguzi   jimbo la Mbulu, ndugu Hudson Stanley Kamoga amewatangaza Madiwani wawili wa kata ya Tumati ndugu Paulo Emanuel Axwesso (CCM) na ndugu Justine Sidamuy Masuja Hayderer(CCM),wamepita bila kupingwa   baada ya Wapinzani wao kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kushindwa rufaa waliokata Tume ya Taifa ya Uchaguzi dhidi ya Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi.   Msimamizi msaidi wa jimbo la Mbulu ndugu Michael Faraay(wa kwanza kushoto) akiwa na mratibu wa uchaguzi ndugu Stedvant Kileo wakimsikiliza kwa makini msimamizi wa uchaguzi (hayupo pichani)wakati wakusoma maamuzi ya rufaa Akitoa taarifa juu ya maamuzi ya rufaa hiyo iliyotolewa na tume ya taifa ya Uchaguzi,msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ame...

Nafasi za Kazi 17 Mamlaka ya Maji Musoma

Image
Musoma Water Supply and Sanitation Authority (MUWASA) is a utility established under section 9 of the Water Supply and Sanitation Act No. 12 of 2009 with the objective of provision of Water Supply and Sanitation services in Musoma Municipality. In this respect, the activities of MUWASA have specifically expanded and the authority now invites application from suitably qualified and skilled individuals who are dynamic and result oriented to fill the following posts:- 1:0 Position: Assistant Technician II 6 Post 1:1 Reporting to: Production Engineer 1:2 Duties and Responsibilities 1) Customer Plumbers i. To repair all water leakages. ii. To assist in connecting new water customers as scheduled. iii. To report on unauthorized water connection. iv. To report of sewerage pipe faults to responsible officers. v. To assist in carrying out water disconnections and re-connections. vi. To reconnect water debtors as assigned timely. 2) Technical Plumbers i. To attend to cust...

Mama Afungwa Jela kwa Kuruhusu Wanaume Kumbaka Mwanaye

Image
MWANAMKE Azzie Watson (25) wa Independence, Kansas City, Marekani, ameshitakiwa kwa kuuruhusu wanaume kumbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka miwili. Mahakama iliambiwa kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa kila mara anasema alimpeleka mtoto wake huyo kwenye nyumba fulani ambako alibakwa mara tano.  Maneno hayo yanadaiwa yalinaswa na rafiki yake wa kiume kwenye kinasa sauti. Watson alikana madai hayo, lakini pia akasema hajui ni kwa nini mtoto wake huyo aliambukizwa ugonjwa wa zinaa. Mtoto huyo wa mtuhumiwa na mdogo wake wa kiume walichukuliwa na kwenda kulelewa na watu maalum wakati kesi ilipoanza kuunguruma. Wakiwa huko, Juni 29, mwaka huu, mama anayemlea alimsikia binti huyo, wakati anamvua nepi, akimlalamikia mwanamme ambaye mlezi huyo hakumjua. “Baba inaumiza.  Baba, usiwe katili.  Baba, inaumiza,” alikuwa akilalamika mtoto huyo. Polisi wamemkata mwanamme mmoja Charles Green (43) kwa mashitaka mawili ya kuhatarisha maisha ya mtoto.  Mt...

JPM ATOA POLE KWA KIKWETE KUFIWA NA BABA MKEWE

Image
Rais John Magufuli akilakiwa na rais mstaafu Jakaya Kikwete alipofika kutoa pole kwa kufiwa na baba mzazi wa mkewe Mama Salma Kikwete, marehemu Rashid Mkwachu, nyumbani kwa wafiwa Msasani jijini Dar es Salaam leo Julai 21, 2018. Mke wa Rais Magufuli, Mama Janeth Magufuli, akilakiwa na Kikwete kwenye msiba huo. Magufuli akimpa pole mke wa Kikwete,  Mama Salma Kikwete.  Magufuli  na Kikwete wakati wa dua.  …Dua ya familia kwa ajili ya marehemu. Rais na mkewe wakiagana na wafiwa. …Akiendelea kuagana na waliofika msibani. Magufuli na mkewe wakisindikizwa.  RAIS  John Magufuli na  mkewe Mama Janeth Magufuli , wamefika nyumbani kwa rais mstaafu, Jakaya Kikwete,   kutoa pole kwa kufiwa na baba mzazi wa mkewe Mama Salma Kikwete, marehemu Rashid Mkwachu, nyumbani Msasani jijini Dar es Salaam leo Julai 21, 2018. Picha na IKULU

Naibu Meya, Madiwani CHADEMA Wajiuzulu Mbeya

Image
IKIWA ni saa chache baada ya uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Mbeya kupendekeza kuwavua uanachama madiwani watatu wa chama hicho mkoani humo kwa utovu wa nidhamu waliouonyesha, madiwani hao wamejiuzulu nyadhifa zao hizo. Madiwani hao na kata zao katika mabano ni Geofrey Kajigili (Sisimba), Newton Mwatuboje (Manga)na Hamphrey Ngalawa (Iwambi). Madiwani hao wamejiuzulu leo Jumamosi  Julai 21, 2018 baada ya Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, Obadia Mwaipalu,  kutangaza uamuzi huo  katika mkutano wake na waandishi wa habari na kubainisha kuwa  vikao halali vya chama vilivyoketi mara kadhaa kujadili hatua stahiki dhidi ya madiwani vimefikia uamuzi huo. Amesema kutokana na utovu wa nidhamu, kukiuka katiba ya Chadema na kukaidi utekelezaji wa maazimio ya uongozi, wamepeleka mapendekezo yao kwa uongozi wa chama hicho Kanda ya Nyasa ili  hatua zichukuliwe. Aliyekuwa Naibu Meya na Diwani wa Kata ya Nsalaga Mjini Mbeya, ...

Simba Kufikia Kambi ya Kishua Uturuki

Image
JUMLA ya wachezaji 26 wa kikosi cha Simba, wanatarajiwa kuondoka kesho Alfajiri kuelekea Uturuki kuweka kambi ya takribani wiki mbili kabla ya kurejea hapa nchini Agosti 5, mwaka huu. Wachezaji wa Simba ambao watakuwa kwenye safari hiyo jana Ijumaa walikuwa na zoezi la upimwaji wa afya kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar. Katika nyota hao 26 watakaosafiri, kiungo mkongwe, Mwinyi Kazimoto, hatakuwepo kwenye msafara huo ambao utaongozwa na kocha mpya wa kikosi hicho, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji. Msafara mzima wa Simba unaotarajiwa kwenda Uturuki kwenye kambi hiyo, utakuwa na jumla ya watu 35. Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba, kimelidokeza Championi kuwa, mbali na Kazimoto, pia Mosses Kitandu, Jamal Mwambeleko, Ally Shomary na Said Mohammed ‘Nduda’ nao watabaki hapa nchini. “Kama ambavyo imepangwa, kikosi kitaondoka Jumapili alfajiri ambapo baada ya kocha mpya kutangazwa jana (juzi Alhamisi), yeye ndiye atakuwa anawaongoza vijana ...

Nafasi Ya Kazi Kwa IT Kutoka Car & General Trading Limited

Image
Car & General Trading Limited is looking for well qualified and competent candidates for the following post: IT Person Qualifications: • Minimum 2 yrs experience in IT • Web graphic and animation design • Knowledge in database programming • Knowledge of Web and Mobile Applications • Good communication skills • Excellent diagnostic and problem solving • Knowledge in Software development • Technical Support Skills/IT Support Education Qualification: Degree in computer Science, Engineering or relevant field Persons with proven experience in IT are encouraged to apply before 20/712018. Package: An attractive salary to be offered to experience candidate. Apply to: HR Manager, Car & General Trading / Tanzania Limited. P.O. Box: 1552, Dar Es Salaam. Tanzania. Source: The Guardian July 11, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Eng. Isack Kamwelwe kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kangi Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Jacob Kingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kailima Ramadhani kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Thomas Mihayo kuwa Kamishn...

SALAMBA,KAGERE WAIPELEKA SIMBA ROBO FAINALI YA KOMBE LA KAGAME CUP 2018

Image
Washambuliaji wapya wa  klabu ya Simba wameisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya APR  ya Rwanda Mchezo wa Michuano ya Kagame inayoendelea jijini Dar Salaam kwenye viwanja vya Chamazi na Taifa. Katika mchezo huo uliokuwa na mashambulizi ya zamu kwa zamu, ulimalizika dakika 45 za kwanza bila timu yoyote kuona bao. Mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, timu zote zilionesha kukamiana zikiwa na lengo la kucheka na nyavu ambapo mnamo dakika ya 66, Kinzingabo aliweza kuiandikia APR bao la kwanza. Ilichukua takribani dakika 6 baadaye Simba kuweza kusawazisha ambapo katika dakika ya 72, mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka Lipuli ya Iringa, Adam Salama alifunga na kuufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-1. Wakati mpira ukiwa katika dakika za nyongeza, straika hatari mpya, Meddie Kagere aliifungia Simba bao la pili na la ushindi kwa njia ya penati baada ya kiungo Said Ndemla kuangushwa katika eneo la hatari. Kwa Matokeo hayo Simba na ...

WIZARA YA AFYA YATANGAZA RASMI KUPOKEA HOSPITALI ZA RUFA ZA MIKOA

Image
WIZARA ya afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imetangaza rasmi kuanzia Juali 1 2018  imepokea Hospitali 28 za Rufaa za Mikoa ambazo zilikuwa chini ya usimamizi wa OR-TAMISEMI . Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala. “Hospitali ambazo tumezipokea zina jumla ya vitanda 7,474 na jumla ya watumishi 8,671 ambao, kati yao Wauguzi ni 3,960, Madaktari 536, Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali ni 182, na waliobakia ni watumishi wa kada zingine mbalimbali za Afya” alisema Waziri Ummy. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo juu ya matangazo yaliyo kwenye mbao mapema leo wakati alipofanya ziara ya kukagua huduma za Afya zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala. Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ambazo Wizara imezipokea ni Ho...

Breaking News: Gari Lateketea kwa Moto Daraja la Kigamboni

Image
MOTO umewaka na kuteketeza gari dogo aina ya Toyota Ractics, leo Jumatatu, Julai 2, 2018 katika Daraja la Nyerere (Kigamboni) jijini Dar es Salaam huku mwenye gari akifanikiwa kutoka nje ya gari na kukimbilia sehem salama. Chanzo cha ajali hiyo imedaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme wa gari hiyo pindi limefika kwenye kukata ticket hitilafu hiyo imetoka na kuanza kuungua, juhudi za kuliokua gari hilo zilifanyika na kufanikiwa kuuzima moto huo hali likiwa limeshaungua mbele. Inadaiwa ajali hiyo imetokea wakati dereva wa gari hilo akilipia fedha ili avuke ng’ambo, lakini pia huku kukiwa hakuna taarifa ya majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa kutokana na ajali hiyo. Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu.

Mshambuliaji wa Croatia atimuliwa Urusi, kisa kukataa kuivaa Nigeria

Image
Mshambuliaji timu ya taifa ya Croatia Nikola Kalinic amerudishwa nyumbani baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu. Kocha wake, Zlatko Dalic alimtaka mshambuliaji huyo kuingia katika dakika za mwisho katika mechi yao dhidi ya Nigeria, akagoma. Kalinic aligoma akidai alikuwa na maumivu ya mgongo. Hivyo akakataa kuinuka na kuingia kama kocha huyo alivyotaka. Pamoja na kwamba aliomba msamaha baada ya Croatia kushinda kwa mabao 2-0 katika mechi hiyo, Dalic alikataa katakata na kusisitiza, arejee nyumbani Croatia.

CHIDI BENZ ANASWA NA MZIGO WA BANGI DODOMA

Image
STAA wa Bongo Fleva, Rashidi Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ amekamtwa na Jeshi la Polisi jijini Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na mzigo wa bangi kiasi cha gramu tano. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema hayo leo Jumatatu, Juni 18, 2018 wakati akizungumza na wanahabari jijini humo baada ya kumtia mbaroni msanii huyo.   Hii ni mara ya pili kwa Chidi kukamatwa na madawa ya kulevya mwaka huu mkoani Dodoma huku akidai kuwa alishaacha kutumia madawa hayo na anaendelea na matibabu Sober House. Hii ni sehemu ya taarifa ya polisi kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa mbaliombali akiwemo Chidi.