Posts

HEKO RAIS JPM TUKO NYUMA YAKO

Image

Wanaowania Tuzo za Ligi Kuu Bara Msimu wa 2017/18 Yaanikwa

Image
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeanika majina ya wachezaji wanao wania tuzo za Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) msimu wa mwaka 2017/18 ambazo zitatolewa Juni 23, 2018 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. TFF imesema kuwa mwaka huu wameongeza tuzo ya mwamuzi bora msaidizi ambayo haikuwepo hapo awali ikiwa na lengo la kuthamini nafasi na mchango wa waamuzi wasaidizi katika mchezo wa soka hapa nchini. Tuzo zitakazotolewa ni za Timu Bingwa, Mshindi wa Pili, Mshindi Tatu, Wanne, Mfungaji Bora, Timu yenye nidhamu, ‘ Under Twenty Player ’, mchezaji bora chipukizi, Mwamuzi bora msaidizi, Mwamuzi bora, Kipa bora na kocha bora, Goli Bora, ‘VPL Best Eleven’, Mchezaji wa heshima huku zawadi zikitarajiwa kutangazwa siku za huvi karibuni. Kamati ya tuzo ya TFF imekamilisha orodha ya wachezaji 30 watakao wania tuzo hizomsimu huu wa mwaka 2017/18. Kwenye majina ya wachezaji 30 waliyo orodheshwa kuwania tuzo hizo watachujwa mpaka kufikia 10 kisha watatu na kuta

Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kulawiti watoto watatu mtwara

Image
Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Mohamedi Kaisi Hamisi mwenye miaka 47 mkazi wa kijiji cha Kawawa mkoani Mtwara, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za ulawiti. Akizungumza na www.eatv.tv, Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara Lucas Mkondya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba mwanaume huyo anatuhumiwa kulawiti watoto watatu wenye miaka 13, 14 na 15, wa shule ya msingi Kawawa, walipokuwa wanatafuta Nazi kwenye minazi iliyopo vichakani baada ya kutoka Kamanda Mkondya amesema kwamba baada ya kuwakuta watoto hao mtuhumiwa aliwatishia maisha kabla ya kufanya kitendo hicho cha kinyama katika eneo la Nambonde. Hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwepo baada ya mtuhumiwa kukamatwa (Nassoro Abdala Nyoya, Sharifa Hassani na Julieta Athanas) kwa masikitiko makubwa wameiomba serikali ichukue hatua kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

BREAKING NEWS: KESI YA BABU TALE YAAHIRISHWA, ARUDISHWA MAHABUSU

Image
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam na Meneja wa mwanamuziki Naseeb Abadul ‘Diamond’, Hamis Taletale ‘Babu Tale’, leo amefikishwa katika Mahakama Kuu jijini Dar ambako baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo kesi imeharishwa na Babu Tale atarudishwa mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam. Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi hicho baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi, katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.

Mambo 8 Usiyoyajua Ndoa ya Kifalme ya Meghan na Prince Harry

Image
Prince Harry Akiwa na Mkewe Rachel Meghan Markle SI kipindi kirefu kimepita tangu watu wengi duniani wajiulize itakuwaje siku ya ndoa ya mwanadada ambaye ni muigizaji maarufu Marekani, Rachel Meghan Markle na mtoto wa Mfalme wa Wales, ambaye pia ni mjukuu wa Malkia Elizabeth II, aitwaye Prince Harry. Wengi walijiuliza ukubwa wa harusi hiyo, mastaa watakaohudhuria watakuwa wamevaa vipi, maharusi watakuwa kwenye muonekano upi, vituko gani vitatokea na mengine mengi! Lakini hayawihayawi hatimaye yamekuwa! Kila kitu kimejulikana baada ya Jumamosi iliyopita, watu kutoka sehemu mbalimbali duniani kusimamisha shughuli zao kushuhudia tukio hilo la kihistoria, ambapo ndoa ilifungwa kwenye Kanisa la Kifalme la St. George la Anglican na kuhudhuriwa na watu wengi mashuhuri Kama yalivyokuwa mategemeo ya wengi, yapo mambo mengi yaliyojiri kwenye ndoa hiyo. Inawezekana umeyasikia tu lakini huyafahamu kiundani au hujayasikia kabisa. Basi usijali, Risasi Vibes inakumegea kwa

RIPOTI MPYA AFYA YA MZEE MAJUTO INDIA

Image
Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ ZIKIWA zimepita siku 19 tangu mkongwe wa vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ apelekwe nchini India kwa matibabu, ripoti mpya ya afya yake imetoka, Risasi Mchanganyiko linayo. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko , Ashraf ambaye alijitambulisha kuwa ni mtoto wa Mzee Majuto alieleza kwamba, kwa sasa afya ya Mzee Majuto inaendelea vizuri, tofauti na alivyokuwa hapa nchini licha ya kwamba bado anaendelea na matibabu. “Kwa sasa baba anaendelea vizuri kwa kweli, tumewasiliana na waliopo naye kule hospitalini India, wanasema hali yake imeanza kutengemaa tofauti na alivyokuwa hapa Bongo. Kwa sasa ni hayo tu, mengine familia itazungumza zaidi baadaye,” alisema Ashraf. MKE WA MAJUTO AFANYA SIRI Risasi Mchanganyiko liliwasiliana na mke wa Mzee Majuto, Aisha Yusuf ambaye yupo hospitalini na mumewe huko India na kumuuliza kuhusu maendeleo ya mgonjwa ambapo mahojiano yalikuwa hivi; Risasi Mchanganyiko: Habari mama, vipi Mzee Majuto

Mkuu wa Wilaya amwaga machozi kwa kipigo walichopata Wananchi wake

Image
Mkuu wa Wilaya ya Rombo Agnes Hokororo ametoa machozi baada ya kukuta wananchi wa eneo la Samanga katika eneo la Useri kulalamikia jeshi la polisi kushirikiana na majambazi katika kuwapiga pamoja na kuwadai rushwa ili waweze kuachiwa pale wanapokamatwa. DC Hokororo amelaani pia kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mikononi na kumuua jambazi anayetuhumiwa kuwaibia wananchi kijijini hapo.

BABU TALE ARUDISHWA MAHABUSU KISA MIL 250

Image
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam, Hamis Taletale. Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam na Meneja wa mwanamuziki Naseeb Abadul ‘Diamond’,  Hamis Taletale ‘Babu Tale’,  jana alikamatwa kwa amri ya mahakama na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambako baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo, alirudishwa mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam ili kufikishwa tena katika mahakama hiyo leo. Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi hicho baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki. Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi,  katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutu

DAWA ZAVUSHWA KUPITIA MTO WENYE MAMBA MKOANI RUVUMA

Image
  Wakazi wa vijiji vilivyopo kandokando ya mto Ruvuma wilayani Nyasa mkoani Ruvuma na wafanyakazi wa Bobari ya Dawa (MSD), wakisaidia kushusha maboksi yenye dawa na kuyaingiza kwenye mtumbwi baada ya kupelekewa na MSD Kanda ya Iringa leo na baadae kuyapeleka katika Zahanati ya Kijiji cha  Mitomoni .   Maboksi ya dawa yakiingizwa kwenye mtumbwi.   Wakazi wa Kijiji cha Mitomoni wakisubiri mtumbwi ili kuwavusha upande wa pili wa mto Ruvuma.   Dawa zikipelekwa Zahanati ya Mitomoni   Maboksi ya dawa kutoka MSD yakishushwa   Wananchi wakishusha maboksi hayo kutoka katika mtumbwi.   Mkazi wa Kijiji cha Mitomoni Khadija Salum, akizungumzia upatikanaji wa dawa kutoka MSD.   Mkazi wa kijiji hicho, Mbwana Koloma, akizungumzia changamoto ya miundombinu ya barabara na jinsi wanavyopokea dawa kutoka MSD.   Mwenyekiti wa kamati ya Afya wa Kijiji cha Mitomoni Omar Hassan akizungumza wakati wa kupokea dawa hizo. Mmoja wa viongozi wa Kiji

Huu ndio umri sahihi wa kufunga ndoa

Image
Kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Utah kilichopo nchini Marekani imebainisha kwamba watu ambao wamefunga ndoa kati ya umri wa miaka 28 mpaka 32 wamekuwa na ndoa yenye mafanikio zaidi. Utafiti huo umebainisha kwamba ndoa ambazo zipo katika hatari ya kuvunjika ni zile ambazo mmoja wa wanandoa ana umri wa chini ya miaka 20 na wale waliofunga ndoa wakiwa na umri wa miaka zaidi ya 45 na kuongeza kuwa ndoa hizo hazijadumu zaidi ya miaka mitano. Taarifa za utafiti huo umeongeza kuwa kwa watu ambao wanasubiri kufika umri wa miaka 30 ili kufunga ndoa wanahatari ya kupata shida sana katika miaka mitano ya mwanzo ya ndoa yao Awali ilijulikana kwamba watu wanaofunga ndoa katika umri mkubwa ndiyo wananafasi ndogo ya kuachana, lakini utafiti huu umeonesha kwamba watu wanaofunga ndoa katika umri wa miaka 45 uwezekano wa kupeana taraka unaongezeka kwa asilimia 5 kila baada ya mwaka mmoja. Sababu kubwa inayosababisha watu walio katika umri mkubwa kupeana taraka ni histori

Binti Aliyedai Kutelekezwa na Lowassa Zengwe Jipya Laibuka!

Image
  U KISEMA unatafuta maisha usisahau kwamba kuna wakati nayo yanakutafuta ili mcheze ngoma moja; tuhuma za Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kudaiwa kutelekeza mtoto zina funzo ndani yake. Siku chache baada ya msichana aitwaye Fatuma Lowassa kujitokeza ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kutoa madai ya kutelekezwa na Lowassa na hatimaye ishu hiyo ‘kupotelea hewani’, Uwazi limenasa zegwe jipya. “Kama ni kujitokeza na madai hayo ya kutelekezwa na Lowassa hii si mara ya kwanza kwa msichana huyo, sikumbuki ni lini lakini miaka ya nyuma aliwahi kufanya hivyo. “Mi nawaamini mkifanya uchunguzi wenu mtapata jambo hili, kuna watu wanayo video ya mahojiano ya msichana huyo pamoja na mama yake wakilalamika kutelekezwa. “Mimi nimejaribu kuipata nimeshindwa ila nasikia inaandaliwa itolewe ili kufufua upya tuhuma,” chanzo makini kililidokeza Uwazi na kulifanya lipange kikosi kazi kwa lengo la kufuatilia uwepo wa video hiyo .     Fatuma Lowassa  

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AWATEMBELEA WANANCHI JAMII YA WAHADZABE NA WATATOGA KATA YA ESHKESH WILAYANI MBULU MKOA WA MANYARA

Image
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza na wananchi wa jamii za Wahdzabe Watatoga na Wasukuma wakati alipotembelea Kata ya Eshkesh  kijiji cha Dumanga Yaeda Chini wilayani Mbulu mkoa wa Manyara wakati alipozitembelea jamii hizo ili kuzungumza nao kuhusu maisha yao pamoja na uhifazi wa tamaduni na mila zao ambao unaweza kuwa Kivutio cha Utalii pia lakini pia kujua mahitaji yao ya muhimu katika maisha ya jamii hizo.   Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza na wananchi wa jamii za Wahdzabe Watatoga na Wasukuma wakati alipotembelea Kata ya Eshkesh  kijiji cha Dumanga kutoka kulia ni Gesso Bajuta diwani wa kata ya Endamilay wilayani Mbulu., Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduzi Wizara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Beleko na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga.  Wananchi wa Eshkesh Jamii ya Watatoga wakiwa katika mkutano huo.

SHIDA YA UMEME KUSINI IMEKWISHA – MAJALIWA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Mradi wa Upanuzi wa Kituo cha Kufua Umeme kwa  Gesi Asilia Mtwara, Mei 21, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na  kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Mradi wa Upanuzi wa Kituo  cha Kufua Umeme kwa Gesi Asilia Mtwara, Mei 21, 2018. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo litakalotumika kupakuwa mafuta kutoka  kwenye meli hadi kwenye matangi ya kuhifadhi mafuta katika bandari ya Mtwara, Mei 21, 2018. Majenereta mawili ya kuzalisha umeme yaliyonunuliwa serikali na kufungwa kwenye eneo la  TANESCO lenye mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi asilia katika Manispaa ya Mtwara ili  kupanua uzalishaji umeme wa gesi asilia Mtwara .  Majenereta hayo yalizinduliwa na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mei 21, 2018 . WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema shida ya umeme iliyokuwa inaikabili mikoa ya Lindi na Mtwar

Polisi Waibua Balaa Ishu ya Wanawake Wenye Makalio Makubwa!

Image
D AR ES SALAAM: Huu mchezo wa baadhi ya wanaume kuona wanawake wenye makalio makubwa na kujifanya kurukwa na akili kwa kuwapigia miruzi, kujikohoza au kuzomeazomea umefikia mwisho. Jeshi la polisi na hasa Visiwani Zanzibar liko ‘siriazi’ na ishu hii ambapo hivi karibuni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Magharibi ‘RPC’, Hassan Nassir (pichani), alitoa tamko ambalo limeibua balaa mitaani. SIKIA TAMKO LA RPC Hebu kabla ya kuelezea balaa lilolopo kuhusu tamko hilo ni bora kujipa muda wa kumsikiliza RPC Nassir kile alichosema alipozungumza katika semina ya kulinda utu wa mwanamke na mtoto iliyofanyika hivi karibuni mkoani humo. “Naomba wananchi wajue mwanamke kupita pengine maumbile yake yamejazajaza ukaanza kukohoa, mmh, mmmh, hilo ni shambulio la aibu tutakukamata tukupeleke mahakamani. “Maana wengine wanafikiri ni mchezo tu ina maana mama zetu, dada zetu, watoto wetu wenye maumbile makubwa wasitembee mitaani; maana wakitembea watu wanaanza kukohoa mmh, kama una kihozi nen

IGP Simon Sirro Akutana na Rais wa TLS

Image
MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro leo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume aliyefika makao makuu ya Jeshi la Polisi kwa lengo la kujitambulisha tangu alipochaguliwa kuongoza chama hicho ambapo pia walijadiliana masuala kadhaa ya kisheria. MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro (kushoto) akiongea na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Fatma Karume aliyefika  makao makuu ya Jeshi la Polisi. Mazunguzo yakiendelea.

Tende, Maji Zinavyofaa Wakati wa Mfungo wa Ramadhani

Image
V YAKULA vinavyofaa kuliwa wakati huu wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni vingi, leo tutaanza kuchambua kimoja baada ya kingine, Mbali na Waislamu, uchambuzi huu unawafaa pia wale ambao siyo Waislamu. Chakula kilichozoeleka zaidi kwa futari ni tende. Baada ya kushinda kutwa nzima na Swaumu, kiwango cha sukari ya mwili hupungua na hivyo, kuhitaji kujazilizwa tena. Aina ya kwanza ya sukari itumikayo mwilini na hasahasa ubongoni ni glukosi. Mshuko wa sukari walioupata wale ambao hawakula au kunywa kwa kipindi kirefu, unaweza kusababisha ulegevu wa mwili. Pindi sukari inapoliwa kwa njia ya chakula au kinywaji, viwango vya glukosi ya mwili hujisawazisha vyenyewe na kumfanya mtu aliyefunga asijihisi kuchoka sana na huwa na nuru zaidi ya macho. Ingawaje tende, mara nyingi, si chakula kinachopendelewa sana na watu wenye njaa, lakini ndicho chakula kisicho na mafuta, na ni chanzo madhubuti cha sukari. Nusu ya sukari zitolewazo na tende ni kwa ajili ya glukosi pek