BABU TALE ARUDISHWA MAHABUSU KISA MIL 250
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam, Hamis Taletale.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam
na Meneja wa mwanamuziki Naseeb Abadul ‘Diamond’, Hamis Taletale ‘Babu
Tale’, jana alikamatwa kwa amri ya mahakama na kufikishwa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu ambako baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata
kutokuwepo, alirudishwa mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es
Salaam ili kufikishwa tena katika mahakama hiyo leo.Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi hicho baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.
Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi, katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.
Comments
Post a Comment