RIPOTI MPYA AFYA YA MZEE MAJUTO INDIA
ZIKIWA zimepita siku 19 tangu mkongwe wa vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ apelekwe nchini India kwa matibabu, ripoti mpya ya afya yake imetoka, Risasi Mchanganyiko linayo.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Ashraf ambaye alijitambulisha kuwa ni mtoto wa Mzee Majuto alieleza kwamba, kwa sasa afya ya Mzee Majuto inaendelea vizuri, tofauti na alivyokuwa hapa nchini licha ya kwamba bado anaendelea na matibabu.
“Kwa sasa baba anaendelea vizuri kwa kweli, tumewasiliana na waliopo naye kule hospitalini India, wanasema hali yake imeanza kutengemaa tofauti na alivyokuwa hapa Bongo. Kwa sasa ni hayo tu, mengine familia itazungumza zaidi baadaye,” alisema Ashraf.
MKE WA MAJUTO AFANYA SIRI
Risasi Mchanganyiko liliwasiliana na mke wa Mzee Majuto, Aisha Yusuf ambaye yupo hospitalini na mumewe huko India na kumuuliza kuhusu maendeleo ya mgonjwa ambapo mahojiano yalikuwa hivi;
Risasi Mchanganyiko: Habari mama, vipi Mzee Majuto anaendeleaje?
Mama: Hajambo…
Risasi Mchanganyiko: Vipi mapokezi huko yalikuwaje na je, mzee ameshaanza matibabu?
Mama: Mpaka sasa sina majibu kamili, baadaye tutawafahamisha.
Risasi Mchanganyiko: Mashabiki wa mzee wangependa kuona hata picha mkiwa hospitalini huko India, tunaomba ututumie kama hutajali.
Mama: Haturuhusiwi kupiga picha, zikiwa tayari mtazipata.
Risasi Mchanganyiko: Ni kwa nini mmekuwa mkifanya siri sana baada ya kufika huko wakati mashabiki wana kiu ya kumuona na kujua hali ya staa wao?
Mama: Huo ni utaratibu wa hospitalini siyo sisi.
Risasi Mchanganyiko: Je, mtaruhusiwa lini kupiga picha na kuelezea hali kamili ya mgonjwa?
Mama: Sijui.
Baada ya mahojiano hayo, gazeti hili lilimtafuta Afisa Habari wa Chama cha Waigizaji Kinondoni, Masoud Kaftany ambaye alikiri kwamba, hali ya Mzee Majuto kwa sasa inaendelea vizuri.
“Unajua kwa sasa hatutoi taarifa na picha akiwa anafanyiwa matibabu India kwa sababu familia imetoa agizo tusitoe badala yake tuwasubiri mpaka watakaporuhusu hivyo tunawasubiri ila kuhusu afya ya Mzee Majuto, anaendelea vizuri tu,” alisema Kaftany.
Kwa muda mrefu Mzee Majuto alilalamika kusumbuliwa na ugonjwa wa ngiri kabla ya baadaye kubainika kusumbuliwa na tezidume ambapo baada ya operesheni hapa nchini alianza kusumbuliwa na tatizo lingine la nyonga hivyo kupelekwa India kwa matibabu zai
STORI: Gladness Mallya, Risasi Mchanganyiko.
Comments
Post a Comment