Wanaowania Tuzo za Ligi Kuu Bara Msimu wa 2017/18 Yaanikwa

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeanika majina ya wachezaji wanao wania tuzo za Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) msimu wa mwaka 2017/18 ambazo zitatolewa Juni 23, 2018 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

TFF imesema kuwa mwaka huu wameongeza tuzo ya mwamuzi bora msaidizi ambayo haikuwepo hapo awali ikiwa na lengo la kuthamini nafasi na mchango wa waamuzi wasaidizi katika mchezo wa soka hapa nchini.
Tuzo zitakazotolewa ni za Timu Bingwa, Mshindi wa Pili, Mshindi Tatu, Wanne, Mfungaji Bora, Timu yenye nidhamu, ‘Under Twenty Player’, mchezaji bora chipukizi, Mwamuzi bora msaidizi, Mwamuzi bora, Kipa bora na kocha bora, Goli Bora, ‘VPL Best Eleven’, Mchezaji wa heshima huku zawadi zikitarajiwa kutangazwa siku za huvi karibuni.
Kamati ya tuzo ya TFF imekamilisha orodha ya wachezaji 30 watakao wania tuzo hizomsimu huu wa mwaka 2017/18.
Kwenye majina ya wachezaji 30 waliyo orodheshwa kuwania tuzo hizo watachujwa mpaka kufikia 10 kisha watatu na kutafuta mshindi.
1. Habibu Kyombo (Mbao)
2. Khamis Mcha- Ruvu Shooting
3. Yahya Zayd-Azam
4. Razack Abalora-Azam
5. Bruce  Kangwa-Azam
6. Aggrey Morris -Azam
7. Himid Mao –Azam FC
8. Awesu Awesu –Mwadui
9. Adam Salamba-Lipuli
10. Mohammed Rashid-Prisons
11. Shafiq Batambuze-Singida
12. Mudathir Yahya-Singida United
13. Marcel Kaheza- Majimaji
14. Ditram Nchimbi-Njombe Mji
15. Eliud Ambokile- Mbeya City
16. Shaaban Nditi-Mtibwa
17. Tafadzwa Kutinyu-Singida
18. Ibrahim Ajibu- Yanga
19. Gadiel Michael-Yanga
20. Papy Tshishimbi-Yanga
21. Kelvin Yondani-Yanga
22. Obrey Chirwa-Yanga
23. Aishi Manula-Simba
24. Emmanuel Okwi-Simba
25. John Bocco-Simba
26. Jonas Mkude-Simba
27. Erasto Nyoni-Simba
28. Shiza Kichuya-Simba
29. Asante Kwasi –Simba
30. Hassan Dilunga-Mtibwa

Comments

Popular posts from this blog