Mambo 8 Usiyoyajua Ndoa ya Kifalme ya Meghan na Prince Harry

Prince Harry Akiwa na Mkewe Rachel Meghan Markle

SI kipindi kirefu kimepita tangu watu wengi duniani wajiulize itakuwaje siku ya ndoa ya mwanadada ambaye ni muigizaji maarufu Marekani, Rachel Meghan Markle na mtoto wa Mfalme wa Wales, ambaye pia ni mjukuu wa Malkia Elizabeth II, aitwaye Prince Harry.

Wengi walijiuliza ukubwa wa harusi hiyo, mastaa watakaohudhuria watakuwa wamevaa vipi, maharusi watakuwa kwenye muonekano upi, vituko gani vitatokea na mengine mengi! Lakini hayawihayawi hatimaye yamekuwa! Kila kitu kimejulikana baada ya Jumamosi iliyopita, watu kutoka sehemu mbalimbali duniani kusimamisha shughuli zao kushuhudia tukio hilo la kihistoria, ambapo ndoa ilifungwa kwenye Kanisa la Kifalme la St. George la Anglican na kuhudhuriwa na watu wengi mashuhuri


Kama yalivyokuwa mategemeo ya wengi, yapo mambo mengi yaliyojiri kwenye ndoa hiyo. Inawezekana umeyasikia tu lakini huyafahamu kiundani au hujayasikia kabisa.
Basi usijali, Risasi Vibes inakumegea kwa haja yako kuhusu harusi hiyo, lakini anza kumfahamu kwanza mrembo huyu aliyevunja rekodi ya kuwa Mmarekani wa kwanza kuingia kwenye familia ya kifalme na ya Malkia Elizabeth II, bila kipingamizi chochote!
Mama yake aliteswa, alinyanyasa na kuachwa na mumewe
Meghan ni Mmarekani, aliyezaliwa Agosti 4, 1981 (36), huko Los Angeles, California. Baba yake mwenye asili ya Kizungu anaitwa Thomas Markle Sr. ambaye kwa sasa anaishi Rosarito, Mexico na mama yake mwenye asili ya Kizungu na Kiafrika, anaitwa Doria Ragland.
Mwanadada huyu ana ndugu zake wawili wa damu, Thomas Markle Jr. na Samantha Grant. Hata hivyo Meghan alilelewa zaidi na mama yake mzazi Doria baada ya kuachika yeye akiwa na miaka 6, tu! Hiyo ilitokana na mama yake kunyanyaswa na kuteswa kwenye ndoa yake kisa kuwa na asili ya Kiafrika.


Kuhusu uigizaji vipi?
Meghan alianza masuala ya kuigiza baada ya kumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Nothwestern, mwaka 2003 alikokuwa akichukua digrii kwenye masomo yanayohusu Michezo ya Kuigiza na Mafunzo ya Kimataifa ‘Theatre and International Studies’.
Ameonekana kwenye Filamu za Deal or No Deal, Remember Me, Horrible Bosses, A Lot Like Love, Get Him to The Greek na Candidate. Lakini miongoni mwa kazi nzuri za uigizaji amefanya pia kupitia ‘series’ za Fringe, The War of Home, Knight Rider, Without a Trace na series aliyoiandaa mwenyewe iitwayo Rachel Zone.

2
Ni Mkatoliki
Ingawa Meghan amefunga ndoa na mumewe, Prince Harry kupitia Kanisa la Anglican, lakini alikuwa akiabudu kupitia Dhehebu la Roman Catholic, alikolelewa na kukulia kwani ndiko wazazi wake huabudu.
Aliwahi kuolewa na kuachika!
Septemba 10, 2011, huko Ocho Rios, Jamaica, mwanadada Meghan alifunga ndoa na muandaaji wa muziki na filamu, Trevor Engelson. Hata hivyo baada ya muda mfupi tu wa ndoa yao, Meghan alipaa na ndege mpaka Toronto, Canada kwa ajili ya kushuti series iitwayo Suits na kumuacha mumewe kwenye nyumba yao huko Los Angeles, akiendelea kushuti filamu zake.
Uhusiano wao wa mbali baadaye ulionekana kuwa mgumu, baada ya Trevor kulazimika kusafiri kila mara kwa takribani saa tano, kumfuata mkewe Canada. Ndipo alipoamua kumpa talaka mapema mwaka 2013.
Penzi lao lilizaliwa Afrika
Kwa familia ya Kifalme na Malkia Elizabeth II, anayotoka Prince Harry pengine isingekuwa kazi kupata mwanamke wa kuwa naye kwenye uhusiano, si ndiyo?
Lakini amini kwamba ilikuwa ni kazi ngumu kwake kumpata mwanamke sahihi wa kuoa kiasi kwamba, aliona suala hilo lisiwe siri hata kuamua kumweleza rafiki wa familia hiyo ya Malkia aitwaye Violet von Westenholz, juu ya wakati mgumu anaopata kutafuta mwanamke sahihi wa kuoa! Violet ambaye ukaribu wake pamoja na Prince Harry na kaka yake William, ulitokana na baba wa mwanadada huyo kumfanyia kazi Mfalme wa Wales, Charles hakupenda kumua-ngusha rafiki yake.
Inaelezwa kwamba, mwaka 2016, Violet alimuonesha Prince Harry ‘clip ya video’ ya mrembo wa Kimarekani, Meghan ambaye alikuwa anatarajia kwenda London kwa ajili ya uzinduzi wa Tamthiliya ya Suits na brand ya mavazi inayomilikiwa na Kampuni ya Ralph Lauren ambayo Violet anafanya kazi.
Prince Harry baada ya kumuoa Meghan inaelezwa kwamba, alivutiwa naye na kumtumia ‘sms’ kwenye mtandao

Comments

Popular posts from this blog