Ukiwa na sifa hizi, kila mwanaume atatamani kukuoa!
KUOLEWA ni heshima kwa mwanamke. Heshima hiyo inaenda mbali zaidi hadi kuwagusa wazazi wa binti ambaye ataolewa. Wazazi wanatembea kifua mbele pindi binti yao anapoolewa, tena wanafurahia zaidi binti huyo anapoolewa akiwa angali bado hajazaa. Wanamshukuru Mungu kwa binti yao kujitunza. Wanamshukuru binti kwa kuwapa heshima katika familia yao na ndiyo maana siku ya sherehe ya kuagwa (send off) wazazi wanafurahi sana kuagana na binti yao kwa heshima. Hali hiyo huwa inaleta shauku kubwa kwa warembo wengi kutamani kuingia kwenye ndoa. Wengi wanaguswa na rekodi za wanawake wenzao ambao wamejitunza na hatimaye kuwaletea heshima wazazi wao. Kinyume chake, wengi wamejikuta wakijilaumu kwa kushindwa kuleta heshima katika familia zao. Binti umri unaenda, anatamani kuingia kwenye ndoa lakini hapati wa kumuoa. Au mwingine inatokea, anatamani kuolewa lakini anaishia kupigwa mimba na kuachwa. Badala ya kuleta heshima, analeta aibu katika familia yake kutokana na mila na destu