John Stephen Akhwari Mwanariadha Shujaa Wa Tanzania

John Stephen Akhwari akikimbia.

MCHEZO wa ri­adha ni mchezo wa tatu unaopendwa zaidi na Watanza­nia, ukiondoa soka na ndondi bila shaka riadha ndiyo nam­ba tatu.

Ukifungua ukurasa wa Google au YouTube kisha ukaandika John Stephen Akhwari hakika kile am­bacho utakiona kitakufanya utamani kutazama mpaka mwisho.

Jina la mtu huyo litajitokeza mara nyingi kwenye kurasa hizo na k a m a u n ­amfa­hamu b a s i itaku­fanya utamani kumtazama na kuona historia yake kwa mara nyingine, kama ni mara yako ya kwanza bila shaka kuna kitu utajifunza hata kama siyo cha kimichezo basi kimaisha.

Historia ya tukio lake lililotokea mwaka 1968 nchini Mexico bado ina­kumbukwa hadi leo, taswira ya kile
wakati akikimbia kiliwa­fanya Wazungu wengi wakitambue kama ‘The Greatest Last- Place Fin­ish Ever in the Olympic games’.

Maana isiyo ras­mi ya sen­tensi hiyo ni kuwa ni mtu wa mwisho bora ku­wahi kumaliza katika michezo ya Olimpiki, yaani alikuwa wa mwisho lakini ni bora kuwahi kutokea na hadi leo kila anayetazama video yake au picha yake wakati an­apokuwa anamaliza kukimbia ataji­funza kuwa katika maisha hutakiwi kukata tamaa.

Miaka ya 1968, 1974 hadi 1980, Tanzania ilikuwa ni miongoni mwa nchi am­bazo zilikuwa zinasifika kwa riadha, wengi walifanya vi­zuri mfano katika mita 1,500 mashindano ya Madola mwaka 1974, Filbert Bay na mshindi wa mita 5,000 Ol­impiki ya Urusi mwaka 1980, Sulei­man Nyambui wote wali­fanya vizuri.

KWA NINI JOHN AKHWARI?
Licha ya kina Bayi na Nyambui kufanya vizuri, lakini alichofanya Akhwari ndani ya ardhi ya Mexico kwa kumaliza mbio ndefu akiwa anachechemea baada ya kuumia, ali­ifanya Tanzania ijivunie ujasiri wake.

Wakati ulimwengu mzima ukimshangaa kwa kitendo chake cha kutokata tamaa licha ya wenzake kumaliza takti­bani saa moja zaidi huku yeye akijivuta, alitamka:

“My country did not send me to Mexico City to start the race. They sent me to finish.” (Nchi yangu haikunituma Mexico City kuanza mbio bali kumaliza mbio). Gazeti la Cham­p i o n i I j u ­m a a l i l i ­funga
safari hadi nyumbani kwa Akhwari wilayani Mbulu mkoani Manyara kuzungumza naye kiundani kuhusu mchezo huo:

HISTORIA YAKE
Alizaliwa Machi 27, 1938 Kijiji cha Khaday, Kata ya Sanu, Tarafa ya Endagikot wilayani Mbulu Mkoa wa Manyara. Alianza riadha mwaka 1958 baada ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 1962, mwaka 1976 ndiyo ambao aliachana rasmi na mchezo huo.

KWA NINI RIADHA?
“ T a n g u enzi za ukoloni kulikuwa na mashindano ya sherehe ya malkia, sasa tulikuwa t u n a p e l e ­kwa umbali mrefu kisha tunarudi kwa miguu, lazima ukimbie, hiyo ikachangia nianze ku­penda riad­ha, pia waka­ti ule ilikuwa fahari kush­iriki mchezo huo.

ULIPOSHINDA ULIPEWA NINI?
“Hakukuwa na medali, tulikuwa tukipe­wa jani la heshima lisilokauka, baadaye ika­ja vikombe kisha ndiyo medali ya dhahabu, ya fedha na medali ya fedha nyekundu.

CHANGAMOTO ULIZOKU­TANA NAZO
“Enzi zetu viongozi hawakuwa na elimu ya kutosha juu ya riadha, mimi ndiyo nili­fungua mlango wa kwenda nje, kwa hiyo nilipata matatizo makubwa sana lakini nili­vumilia.

ULISHINDA MBIO ZIPI?
“Mwaka 1962 nilishinda mashindano ya taifa ya km 3 na 6 Dar, pia Marathon ya Af­rika Mashariki iliyofanyika Nairobi, nafasi ya 6 mbio za Jumuiya ya Madola km 42 iliyo­fanyika West Australia na mbio za Sri Lanka km 3 nafasi 2.
“Mwaka 1963 nafasi ya 2 km 42 nchini Ugiriki, 1967 mshindi wa kwanza km 42 Afrika mashariki ilifanyika Kampala nchini Uganda, 1970 mshindi wa 5 km 42 kati ya watu 56 mashindano ya Jumuiya ya Madola.

WANARIADHA WA SASA KU­TUMIA DAWA ZA KUONGEA NGUVU
“Zamani hayo mambo hayakuwepo ulikuwa unatumia nguvu ya kuzaliwa, wa­naoendelea na tabia hiyo hawatafika mbali, hizo zinaumiza na zinakufanya usidumu kwenye michezo.
“Tangu naanza kushiriki hadi nastaafu sikuwahi kutumia.
TUKIO LA MEXICO CITY MWAKA 1968
“Olimpiki ya mwaka 1968, nia yangu ilikuwa ni kushinda tatizo kwetu Tanzania, viongozi wa chama cha Riadha Taifa (Tanganyika Africa Athlet­ics Association-TAA) chini ya mwenyekiti wa wakati huo, Mustapha Nyang’anyi badala ya kutupeleka kufanya mazoezi kwenye ukan­da wa juu ya bahari wakatupeleka kwenye usawa wa bahari.
“Unaambiwa ukitaka kuzoea hali ya huko lazima ukafanye mazoezi miezi sita ndiyo uzoee, matokeo yake niliumia misuli na ni­kawa wa mwisho.

“Nilipoanza kukimbia sikuwa na hofu yoyote, nilikuwa naongoza, ghafla nikaanza kuhisi kizunguzungu, nikapoteza fahamu. Nilipozinduka nikakuta watu wa huduma ya kwanza wananihudumia, wakanitaka niingie katika ambulance, nikakataa, nikasi­mama na kuanza kukimbia tena.
“Nilikuwa nahisi maumivu makali sana, na nikawa natokwa na damu, niliumia ma­goti yote lakini sikujali hilo kwa kuwa lengo langu ilikuwa ni kumaliza. Nilitimiza hilo kwa saa 3:25:27. Baada ya hapo nilitumia wiki mbili nikitibiwa kisha ndiyo nikarejea Tanzania.

“Lengo lilikuwa kutimiza uzalendo wangu wa kile ambacho nchi ilinituma na ninashukuru nilitimiza ahadi niliyojiwekea.”
Wakati wanaanza mbio hizo walikuwa washiriki 75, lakini mwisho wakamaliza 57 huku 18 wakiishia njiani, Mtanzania huyo
akawa mtu wa 57 am­bapo mshindi wa kwanza alikuwa ni Mamo Wolde wa Ethiopia aliyetumia sa 2:20:26.
Hiyo inamaana kuwa Akhwari alimal­iza mbio ikiwa ni saa moja na dakika 5 tangu mshindi alipopatikana, mashabiki na waandishi wakiwa wameshasahau kama kulikuwa na mshiriki mwingine ambaye alikuwa hajamaliza kukimbia.
Alipofuatwa na kuulizwa sababu za kuendelea kukimbia wakati alikuwa hoi kwa maumivu ndipo akasema: “My country did not send me to Mexi­co City to start the race. They sent me to finish.” Kauli ambayo imetumika katika matukio mengi ya kuhamasi­sha jamii mbalimbali.
VIPI KUHUSU TUZO ZA HESHIMA?
“Mwaka 1995 nilitunukiwa nis­hani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Ali Hassan Mwinyi, 2008 nil­ipe­wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Af­rika wa Ri­adha, tuzo ambayo ilitolewa Af­rika Kusini, mwaka huohuo ni­likwenda Beijing, China ku­fungua mashinda­no ya Ol­impiki na kukimbiza Mwenge wa Olimpiki, 2012 nili­tunukiwa Nishani ya Sanaa na Michezo iliyotolewa na Rais Jakaya Kik­wete.

KUNA MBIO ZIME­ANZISHWA KWA JINA LA AKHWARI
“Nazijua na nil­ishirikishwa, nafura­hi kuona vijana wanaen­delea kuthamini mchango wangu katika riadha, kwangu ni jambo la pe­kee kuona mashindano ya riadha yanaitwa jina langu, natamani kuo­na wanariadha wetu wa sasa wanafanya makubwa kuliko mimi na kuiletea heshima Tanzania,” anasema.
TUZO YA HES­HIMA MARE­KANI
Watanzania waish­io Marekani wam­etambua mchango wa mkongwe huyu na kuamua kumpa­tia Tuzo ya Heshima (Tunu Adimu) ambazo zilitolewa Aprili 29, 2018 jijini Dallas, Texas.
Lengo kubwa ya tuzo hizo ni kwa watu waliotoa mchango mkubwa kwa taifa la Tanzania.
MAKALA NA KENNEDY LUCAS

Comments

Popular posts from this blog