TUZO ZA RAIS KWA WAZALISHAJI BORA WA VIWANDA ZATIKISA JIJINI DAR

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,(kulia) akizungumza jambo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka uliopita wa 2017.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo.
…Mwijage (katikati) akikabidhi tuzo kwa baadhi ya wamiliki wa viwanda.
Mwijage (kushoto) akikabidhi tuzo kwa Zephania Shaidi kutoka Shirikisho la  Viwanda Tanzania (CTI) ambaye alipokea kwa niaba ya baadhi ya viwanda vilivyofanya vizuri ambavyo wawakilishi wake hawakuwepo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mwijage (katikati).

SHIRIKISHO  la Viwanda Tanzania (CTI) leo limetoa tuzo kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka uliopita wa 2017 ambazo zimekabidhiwa na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage.
Tuzo hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tuzo za Rais za Mzalishaji bora wa Viwandani (PMAYA)  2017.

Akisoma taarifa yake kwa niaba ya rais, Mwijage amesema kuwa sekta ya Viwanda ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi yetu na kuboresha maisha ya Watanzania na kwamba Duniani kote sekta hiyo ndiyo chimbuko la maendeleo ya haraka ya nchi mbalimbali na ni mhimili mkuu wa kutegemewa katika kuongeza thamani ya mali ghafi tulizonazo, kutoa ajira kwa wananchi, kuongeza mapato ya Serikali pamoja na fedha za kigeni, kuongeza na kuboresha sayansi na teknolojia na hivyo kukuza uchumi,na kuondoa umaskini nchini.

Tuzo hizo ziliandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) ambapo hutoa tuzo hizo kwa viwanda vilivyofanya vizuri katika mwaka uliopita zikiwahusisha wanachama wa CTI na wasio wanachama.

Na Denis Mtima/Gpl.

Comments

Popular posts from this blog