Jinsi ya kuepuka matatizo ya nguvu za kiume
MATATIZO haya ya nguvu za kiume humuathiri mwanaume na mwanamke kwa ujumla.Tatizo hili hulalamikiwa aidha na mwanaume mwenyewe au mwanamke kwa kutofurahia tendo la ndoa, hasa kwa wale walio katika mahusiano. Zipo sababu nyingi kama tutakavyokuja kuona lakini matatizo haya humuathiri mtu zaidi kisaikolojia anapohisi anashindwa kutimiza wajibu wake au mwanamke kujihisi hapati haki yake ya kufurahia tendo.
Mtu anaweza kuwa na tatizo dogo ambalo kama ni mshtuko na anapopata mshituko huo hujikuta tatizo linazidi hivyo kujikuta mgonjwa, yaani ana tatizo. Kwa hiyo ni vema unapotokewa na tatizo hili usikimbilie kutumia dawa hasa za asili na hata za madukani bali waone madaktari wakufanyie uchunguzi katika hospitali kubwa.
AINA ZA MATATIZO YA NGUVU ZA KIUME
Tatizo la nguvu za kiume limegawanyika katika makundi mawili; Kwanza ni tatizo la kuzidi kwa nguvu za kiume. Watu wengi wamezoea ukisema tatizo la nguvu za kiume ni upungufu, lakini lipo hili la kuzidi isivyo kawaida na kujikuta mtu anashidwa kufikia mwisho au mshindo. Hali hii tutakuja kuiona kwa undani.
Tatizo la pili ni upungufu wa nguvu, hili ndilo tatizo lililozoeleka sana miongoni mwa wanaume wengi. Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kuwa mdogo au mkubwa, nao una sababu zake tutakuja kuziona.
KUONGEZEKA NGUVU ZA KIUME ISIVYO KAWAIDA
Hali hii kitaalamu inaitwa ‘Painful Abnormal Erection of The Penis’. Mwanaume mwenye hali hii hulalamika maumivu makali ya uume pale unaposimama na hushindwa kumaliza tendo. Hali hii inaweza kuwa ya muda tu au ikatokea mara mojamoja na wakati mwingine inaweza kuendelea kwa muda mrefu.
Chanzo cha tatizo hili ni matatizo au magonjwa ya mfumo wa fahamu, kulazimisha uume usimame kwa kutumia madawa au njia yoyote ile, uwepo wa mawe katika kibofu cha mkojo, maambukizi katika njia ya mkojo, maambukizi ya tezi dume kuziba kwa mishipa ya damu ya vena inayotoa damu kwenye uume kurudisha mwilini na hii huwatokea zaidi wagonjwa wa siko seli, matatizo ya mfumo wa damu hasa yanayoambatana na kansa ya damu au magonjwa yanayoathiri mfumo wa damu.
MATIBABU
Tiba sahihi ya tatizo hili ni kutafuta chanzo cha tatizo la uume kusimama kwa muda mrefu hadi mtu anapata maumivu.
Endapo hali kama hii inatokea, basi epuka kuvaa nguo za kubana au nguo za ndani, jifunge tu shuka au msuli na endapo utavaa nguo kama suruali au bukta basi hakikisha uume unauzungushia pamba ya kutosha usikwaruze kwenye nguo ngumu na ikaleta kikwazo kitachoongeza maumivu.
Mgonjwa apelekwe haraka hospitali ambapo atapatiwa matibabu. Wengi hutokewa na hali hii kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume bila ya ushauri wa daktari.
Comments
Post a Comment