Rais Magufuli: Bora Kula Sumu Kuliko Fedha za Serikali

Rais Magufuli leo Ijumaa ameweka jiwe la msingi la Barabara ya Kidatu – Ifakara. Sherehe hizo zimehudhuriwa na Wabunge wote wa Chadema na CCM mkoani Morogoro.
Moja ya kauli ambazo Rais amezungumza leo; “Kuna maeneo ambayo wakandarasi wamekula hela za miradi, wamekula sumu. Hela ya Serikali ya awamu ya tano hailiwi bora ule sumu kali. Waliokula fedha waanze kujiandaa, kurudisha fedha na kutekeleza miradi au kukumbana na sheria ya mwaka 97.”

“Haiwezekani mimi nitafute hela halafu wewe uzile tu nikwambie umeula wa chuya. Kama makandarasi watakuwa wamekimbia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, polisi na Takukuru wawatafute popote. Watazitapika hizo fedha wanazozitafuna,” amesisitiza Rais.
Amesema hatojali fisadi ametoka CCM, Chadema wala CUF au nje ya nchi, atawashughulikia.

Mbunge wa Kilombero, Lijualikali(CHADEMA)
“Ukiniambia leo uwape zawadi gani watu wa Morogoro maana kuna mengi lakini naomba watu wote ambao wamechukua ardhi yetu na hawaifanyii kazi basi naomba leo uondoke nao kwa sababu watu hao wanahujumu rasilimali yetu na hii barabara kama tutaacha hivi basi kwetu itakuwa haina faida na mimi kama Mbunge nilikuwa nawaambia wananchi wangu msiuze ardhi hovyo kwani ardhi ndiyo rasilimali yetu”
“Wananchi wana shida ya kujua wingi wa sukari, wanashida ya kujua ni namna gani uzito wa mua unapatikana kwani kiwanda ndiyo kinapima chenyewe uzito, kiwanda kinapima chenyewe wingi wa sukari wananchi wanapewa tu hesabu sasa hatuwezi kujua tunaibiwa au tuko sahihi”

Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule(Prof. Jay)

Profesa Jay amemuomba Rais Magufuli amsadie shilingi bilioni mbili ili kukamilisha mradi mkubwa wa maji uliopo katika Kata ya Ruaha.
Pia amemuomba Rais kutatua changamoto nyingi zinalolikabili jimbo lake ikiwemo uboreshaji wa miundombinu.

Comments

Popular posts from this blog