Mkude Atajwa Namba Sita Bora 2017/18

KIUNGO mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ametajwa kuwa ndiye kiungo bora mkabaji msimu huu kuliko wote.

Hali hiyo inatokana na uwezo wake mkubwa ambao amekuwa akiuonyesha uwanjani wakati akiitumikia timu yake hiyo katika Ligi Kuu Bara.

Wakizungumza na Championi Ijumaa kwa nyakati tofauti baadhi ya wachezaji wa timu mbalimbali za ligi kuu wamemtaja Mkude kuwa ndiye kiungo bora msimu huu.

Beki wa kati wa Mwadui FC, Idd Mobby amesema Mkude ni bora zaidi kuliko msimu uliopita na amekuwa na msaada mkubwa kwa timu yake jambo ambalo linamfanya awe vizuri.

Naye beki wa Prisons, Salum Kimenya, amesema: “Simba wanapaswa kujivunia mchezaji huyo, kawafanyia kazi kubwa, ukiangalia mechi nyingi ambazo hajacheza mabeki wao walipata shida sana tofauti na anapokuwepo uwanjani, binafsi naona anastahili kuwa namba sita bora msimu huu

Comments

Popular posts from this blog