Posts

MAAMUZI YA RAIS KUUPANDISHA HADHI MJI WA DODOMA KUWA JIJI NI SAHIHI-MAJALIWA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni Jijini Dodoma Mei 3, 2018. WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema maamuzi ya  Rais Dkt John Magufuli ya kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji ni sahihi na ameyafanya kwa wakati muafaka na hakuna sheria iliyokiukwa. Aprili 26, 2018 Rais Dkt Magufuli aliupandisha hadhi mji wa Dodoma kutoka Halmashauri ya Manispaa na kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma pamoja na kumteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 3, 2018) wakati akijibu swali la Bibi Felista Bura (Viti Maalumu) katika kipindi cha Maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma. Bibi Felista alitaka kupata kauli ya Serikali juu ya baadhi ya watu wanaobeza maamuzi ya Rais Dkt. Magufuli ya kuupandisha hadhi mji wa Dodoma. Amesema kuwa Rais Dkt Magufuli hakukiuka sheria kwa sababu ana mamlaka kwa

BREAKING NEWS: YONDANI ASIMAMISHWA KUITUMIKIA YANGA

Image
Beki wa Yanga, Kelvin Yondani (kushoto). Bodi ya Ligi Tanzania, imetangaza kumsimamisha beki wa Yanga, Kelvin Yondani kutokana na kuonekana katika video akimtemea mate beki, Asante Kwasi. Mtendani wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amezungumza hivi punde na kusema suala lake limepelekwa Kamati ya nidhamu baada ya kuonekana haliwezi kusikilizwa na Kamati ya Saa 72 iliyokaa. “Kwa hiyo sasa tunamsimamisha hadi hapo kamati itakapokaa na kuamua kuhusiana na suala lake,” alisema Wambura. Katika picha ya video ilimuonyesha Yondani akimtemea Kwasi raia wa Ghana katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyowakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba ambao walishinda kwa bao 1-0. Suala hilo lilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau, wakiwemo waliomtetea Yondani na walioona haikuwa sahihi.

MLINGA ‘KUMCHOMA’ MWANAFUNZI SINDANO, WAZIRI UMMY: SI SAHIHI

Image
KUFUATIA picha zilizosambaa mitandaoni zikimuonyesha Mbunge wa Ulanga, Morogoro (CCM), Goodluck Mlinga, kuonekana ameshika sindano kama anamchoma mwanafunzi chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi, jambo hilo limeibua hisia tofauti miongoni mwa wadau huku wakihoji kuhusu mtu asiye na taaluma ya afya anapata wapi mamlaka ya kutoa chanjo hiyo. “Siasa imeingia sehemu mbaya sana, tiba si eneo la mzaha kiasi hiki, hili ni eneo hatari, na mchezo huu kwa afya za watu unaweza kusababisha maumivu hata ulemavu, si kila mtu anaweza kutoa chanjo,” alitoa maoni mmoja wa wadau kupitia mtanda wa Twitter. Akijibu hoja hiyo kupitia akaunti ya Twitter, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema jambo hilo si sahihi kwani wanaotakiwa kutoa huduma za afya ni watu wataalamu wa tiba na si mtu mwingine huku akimuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kutoa maelekezo kwa waganga.

AJISALIMISHA POLISI BAADA YA MAHINDI ALIYOIBA KUNASA MABEGANI

Image
KIJANA Frank Japhet (23), mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, amelazimika kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Mlandizi, Kibaha, Pwani, baada ya mzigo wa mahindi unaokadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu 20, anaodaiwa kuuiba kung’ang’ania mabegani. Wakati akihojiwa kituoni hapo, mtuhumuwa huyo amesema mzigo huo, uliofungwa kwenye kiroba aliuiba kwa mama mmoja eneo la Mtaa wa Nyambwiro, Mlandizi, Kibaha, mkoani Pwani majira ya saa 7.00 usiku wa kuamkia leo Mei 3, 2018, akaongeza kwamba aliondoka na mzigo huo hadi eneo la Stendi ya Mlandizi alipokuwa auache kwa mwenzake ili arudie mzigo mwingine, ambapo mzigo huo uling’ang’ania kichwani. Ameendelea kusema kwamba alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini aliponyanyuka, alinyanyuka nao kichwani! Baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu, alidai alichoka hivyo akalazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini

Vijana wa CCM wanatamani sana nionyeshe naiunga mkono serikali ya awamu ya tano!

Image
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatamani sana yeye aonekane anaiunga mkono serikali ya awamu ya tano na kusema kuwa watasubiri sana kwa jambo hilo. Msigwa amesema hayo leo Mei 3, 2018 baada ya moja ya video yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuoonyesha akimsifia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa katika kipindi chake amekuwa hajali vyama kwani hata wao watu wa CHADEMA wamekuwa wakipokea fedha ambazo zimewawezeshja kujenga barabara kutoka Mlandege mpaka kwa Mkuu wa wilaya ambayo imegharimu zaidi ya bilioni tatu, wana stendi ya Ipogolo ambayo nayo imegharimu zaidi ya bilioni tatu na kudai kuwa Rais hapendelei. Baada ya video hiyo kusambazwa sana Mchungaji Msigwa amesema kuwa "Vijana wa CCM wanatamani sana nionyeshe naiunga mkono serikali ya awamu ya tano! (Dying for my endorsement ) Mtasubiri sana"`

KANISA LAPIGA MARUFUKU SHELA KWA WAJAWAZITO WAKATI WA NDOA

Image
KANISA Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, limewapiga marufuku wanawake wajawazito kuvaa shela wakati wa kufunga ndoa kwa madai vazi hilo ni alama ya ubikira kwa mwanamke na sio vinginevyo.   Hayo yamesemwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresa, Padre Festus Mangwangi  wakati akiweka mkazo juu ya tamko lililotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Isaack Amani , wakati akiadhimisha misa ya shukrani iliyofanyika Jumapili iliyopita, baada ya kuteuliwa kwake na Baba Mtakatifu Francis kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo. Kabla ya uteuzi huo uliotangazwa Desemba 27 mwaka 2017 , Askofu Mkuu Amani alikuwa Askofu wa Jimbo la Moshi na kusema haitakiwi kwa mwanamke yeyote ambaye anajijua ni mjamzito kuvaa shela kipindi anafunga ndoa kwa kuwa vazi hilo linavaliwa na mwanamke asiyemjua mwanaume ( bikra ).   Aidha, Padre Festus Mangwangi amewataka wazazi kuwafundisha watoto wao wa kike kutunza miili yao na kuishi maisha ya kimaadili hadi watakapopata wenza wa kufung

Ngorongoro Heroes kucheza na Mali Mei 13

Image
Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) itacheza na timu ya Taifa ya Mali U20 Jumapili ya Mei 13,2018 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Katika mchezo huo utakaochezwa saa 10 jioni kiingilio cha kuingia Uwanjani kutazama mechi hiyo VIP zote shilingi 3,000 Mzunguko shilingi 1,000. Ngorongoro Heroes wapo kambini wakiendelea kujiandaa na mchezo huo, ampabo wapo kwenye ratiba ya kufanya mazoezi ya gym asubuhi na jioni kabla ya kuwa na mazoezi ya uwanjani kesho na Ijumaa ambapo. Alhamisi watakuwa na kipindi kimoja cha Uwanjani saa 10 kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Ijumaa watafanya vipindi viwili asubuhi na jioni saa 10. Kikosi hicho hakina majeruhi vijana wana morali kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa kwanza wa raundi ya pili ya kufuzu fainali za vijana Africa.

DKT. MWAKYEMBE AFANYA UTEUZI TASNIA YA FILAMU

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe ametua Bodi Mpya ya Filamu Tanzania. Bodi hiyo itaongozwa na Prof. Frowin Paul Nyoni kama Mwenyekiti. Kwa mujibu wa sheria za Filamu na Michezo ya kuigiza Namba. 4 ya mwaka 1976.

JPM: Mtoto Wangu na wa Lukuvi, Hawawezi Kupata Mkopo

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuna vigezo muhimu ambavyo huzingatiwa katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, ikiwa ni pamoja na kuangalia hali ya kiuchumi ya familia ya mwombaji wa mkopo huo ambapo familia ambazo zinao uwezo hasa viongozi, hawana sifa za kupata mkopo hata kama angekua ni mtoto wake. Rais Magufuli amesema hayo leo Mei 02, alipokua akihutubia wanafunzi na uongozi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa; “Kwa mwaka unatoa bilioni 427, kwa nchi masikini kama Tanzania na unapotoa mkopo ni lazima pawepo na taratibu zinazoendeshwa na watu, mtoto wangu mimi hawezi kupata mkopo, mtoto wa Lukuvi (Waziri wa Ardhi),  mtoto wa Profesa, hata mtoto wa mkuu wa mkoa hatakiwi kupata mkopo,” alisema Rais Magufuli. Aidha, Rais amesema wanafunzi wa elimu ya juu wanaonufaika na mkopo kwa sasa ni zaidi ya 130,000 ambapo serikali imetoa bilioni 427 licha ya kukumbwa na changamoto ya kubaini wanafunzi hewa  wa el

Aina 7 Za Juisi Zenye Kuondoa Sumu Mwilini

Image
Sumu mwilini hutokana na vile vitu au vyakula ambavyo binadamu hutumia huenda kwa kujua au kutokujua. Sumu hizo pia huweza kuchangiwa na matumizi ya yasiyosahihi ya dawa mbalimbali. Miongoni mwa mbinu bora na nzuri ya kuondoasumu hizo ndani ya mwili ni pamoja na kutumia vyakula halisi mara kwa mara. Hapa nanayo orodha ya vinywaji ambavyo huweza kuondoa sumu ndani ya mwili:- 1. Juisi ya mchanaganyiko wa tango na spinachi. 2.Jusi ya mchanganyiko wa tangawizi na spinachi. 3. Juisi ya mchanganyiko wa chungwa na tango. 4. Juisi ya komamanga pamoja na mapera 5. Juisi ya changanyiko wa passion na tango 6. Juisi ya mchanganyiko wa apple na parachichi 7. Juisi ya mchanganyiko wa mbegu za maboga na strawberry

Breaking News: Mahakama Yaamuru Hans Pope na Lauwo Wakamatwe

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo April 30, 2018 imetoa amri kwamba Mwenyekiti wa Usajili wa Klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani ili kuunganishwa katika kesi inayomkabili Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’. Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao. Wakili Swai amedai amewatafuta washtakiwa hao tangu Machi mwaka huu bila mafanikio hivyo akaomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani. Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, nyaraka na kutakatisha fedha kiasi cha Dola za Marekani 300,000.

Chadema Wakanusha Lissu Kuerejea Nchini

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimekanusha taarifa zinazoendelea mitandaoni kuhusu uwezekano wa kurejea nchini kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu kutokea Ubelgiji alipokuwa akipatiwa matibabu tangu mapema Januari mwaka huu. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Tumaini Makene amesema; Kupitia mitandaoni mapema leo kumekuwa na taarifa za kwamba Lissu anatarajiwa kutua nchini wakati wowote kuanzia juzi na kwamba amemaliza matibabu yake kitu ambacho si cha kweli na kimezua taharuki. Makene amesema, Lissu hajazungumza na mwandishi wa habari yeyote kuhusu kurejea kwake hapa chini kwa sababu  hajapona na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine mwishoni wiki hii au wiki ijayo. Chadema kimetoa wito kwa na wanachama na Watanzania wote wenye mapenzi mema kutokana na kuguswa na uzito wa masahibu yaliyompata Lissu wameendelea kuguswa na kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya matibabu na hali ya afya yake kupuuza taarifa hizo. Lissu yupo nchini Ubelgi

Makonda Ampokea Ahmed Aliyepooza Akitokea China

Image
Ahmed alikwenda nchini China miezi miwili iliyopita ambapo hali yake inaendelea vizuri  baada ya kupatiwa matibabu. Kijana huyo alipata tatizo hilo la kupooza baada ya kuumia wakati akifanya mazoezi ya kuogelea. Ahmed Albaiti akiwasili uwanja wa ndege Dar es Salaam akitoka katika matibabu nchini China leo. Picha na Denis Mtima | GPL

RAIS MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA IRINGA-DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma wa pili kutoka kulia wakivuta utepe kwenye jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Sherehe hizo za ufunguzi zilifanyika katika kijiji cha Ndolela kilichopo Isimani nje kidogo ya mji wa Iringa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma, Balozi wa Japan Masaharu Yoshida wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa , Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wa Serikali na wageni k

Serengeti Boys wanyakua ubingwa wa CECAFA U- 17

Image
Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imeibuka na ubingwa wa CECAFA U-17 baada ya kuifunga timu ya vijana ya Somalia mabao 2-0 katika fainali iliyopigwa huko Burundi. Serengeti Boys imecheza vizuri mchezo huo wa fainali na kufanikiwa kuongoza kwa bao moja hadi mapumziko kabla ya kuongeza bao la pili kipindi cha pili na kujihakikishia ubingwa huo. Mabingwa hao wapya wa Afrika Mashariki na Kati, wamekabidhiwa kombe hilo na mgeni rasmi wa fainali hiyo ambaye ni Rais wa shirikisho la soka barani Africa Ahmed Ahmed. Vijana hao wametinga fainali hiyo baada ya kuwatoa timu ya Taifa ya Kenya U17 kwa jumla ya mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa Alhamisi. Wakati Somalia imeingia fainali kwa kuifunga Uganda 1-0. Moja ya timu zilizofungwa na vijana hao katika hatua ya makundi ni pamoja na Sudan na Uganda. Katika michuano hii timu ya taifa ya vijana ya Zanzibar (Karume Boys) iliondolewa kutoka na kuwa na wachezaji we

ALIKIBA NA MKEWE AMINA WALIVYOINGIA UKUMBINI

Image
STAA wa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ na mkewe, Amina raia wa Kenya wameingia katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena uliyopo Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusherehekea harusi yao usiku huu wa Aprili 29, 2018. Katika sherehe hizo ambazo pia zinahusisha harusi ya mdogo wake Alikiba, Abdu Kiba na mkewe, Ruwayda imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde. Tazama picha hizi. Picha na Azam TV.

ABDU KIBA NA MKEWE WALIVYOINGIA UKUMBINI

Image
MKALI wa Bongo Fleva, Abdu Kiba na mkewe, Ruwayda tayari wameshaingia katika Ukumbi wa Serena Hotel uliyopo Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusherehekea harusi yao usiku huu. Katika sherehe hizo ambazo pia zinahusisha harusi ya Alikiba na mkewe, Amina imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde. Tazama picha hizi. Picha na Azam TV.

MAMA KIKWETE, UMMY MWALIMU WATINGA HARUSI YA KIBA

Image
MKE wa Rais wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepata fursa ya kuhudhuria katika harusi ya staa wa Bongo Fleva, Alikiba na mkewe, Amina katika ukumbi wa Serena Hotel uliyopo Posta jijini Dar es Salaam usiku huu wa Aprili 29, 2018. Mama Salma ambaye pia ni mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameambatana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Watoto, Wanawake, Jinsia na Wazee, Dkt. Ummy Mwalimu katika seherehe hiyo. Katika sherehe hiyo pia inahusisha harusi ya mdogo wa Alikiba, Abdu Kiba na mkewe, Ruwayda ambao walifunga ndoa Jumapili iliyopita. Viongozi wengine waliopata fursa ya kuhudhuria sherehe hiyo ni Naibu Waziri wa Kazi ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde (kulia), na Mwenyekiti wa UVCCM, Khery James (kushoto). Picha na Azama TV.

WAMILIKI SOBA HOUSE WAWAJIBU WABUNGE TUHUMA ZA KUWACHOMA SINDANO WAATHIRIKA DAWA ZA KULEVYA

Image
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wamiliki wa Sober House Tanzania, Pili Missanah (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Baadhi ya viongozi wa  Sober House Tanzania walioshiriki mkutano huo na waandishi wa habari. WAMILIKI wa nyumba zinazosaidia waathirika kujinusuru na dawa za kulevya nchini maarufu kama Soba house wamejibu tuhuma za kuwachoma vijana sindano pindi wapatapo nafuu. Akiongea na waandishi wa habari leo Jiji Dar es Salaam Katibu wa Umoja wa Soba house nchini, Pili Missanah ambaye ni mmoja wa wamiliki wa vituo hivyo ameeleza kuwa, April 25 mwaka huu katika mjadala wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baadhi ya wabunge walieleza kuhusu tabia chafu  za baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo kuwachoma sindano za dawa za kulevya baadhi ya waathirika pindi wanapokaribia kupona ili wazazi au walezi waendelee kuchangia fedha kwenye nyumba hizo. Pili ameeleza kuwa lengo la nyumba hizo sio baya bali ni kuwasaidia waathirika wa dawa za k

FT: SIMBA 1-0 YANGA, KUTOKA UWANJA WA TAIFA (KADI NYEKUNDU KESSY)

Image
MPIRA UMEKWISHA DAKIKA 4 ZA NYONGEZA Dk 90 Yanga wanaingia lakini Simba wamejaa nyum SUB Dk 83, Simba wanamtoa Gyan nafasi yake inachukuliwa na Paul  Bukaba Dk 82, Mahadhi anaingia na kujaribu kupiga krosi, Mkude ameunawa ni faulo si mbali na lango la Simba Dk 76, krosi maridadi katika lango la Simba, Chirwa anaruka na kupiga kichwa lakini ni goal kick Dk 70 Kichuya anapangua watu wawili, anatoa pasi kwa Bocco, naye anampa Kapombe kona ya saba ya Simba, Yanga hawana kona hata moja Dk 70 sasa, bado inaonekana Yanga wanafanya mashambulizi ya kufunga, lakini Simba wanapoteza nafasi nyingi na lazima wazitumie mapema maana Yanga bado nao wana uwezo wa kufunga Dk 67, Kichuya anamtoka Makapu, anaingia na kupiga krosi safi kabisa, Dante anapiga kichwa na kuokoa Dk 65 Yanga wanaonekana wanaanza kufunguka lakini Mlipili yuko makini, anaokoa unakuwa wa kurushwa Dk 63 mpira wa Okwi unaokolewa na kuwa kona ya sita ya SImba, inachongwa na kuokolewa SUB Dk 62, Yanga inafanya sub