JPM: Mtoto Wangu na wa Lukuvi, Hawawezi Kupata Mkopo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuna vigezo muhimu ambavyo huzingatiwa katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, ikiwa ni pamoja na kuangalia hali ya kiuchumi ya familia ya mwombaji wa mkopo huo ambapo familia ambazo zinao uwezo hasa viongozi, hawana sifa za kupata mkopo hata kama angekua ni mtoto wake.

Rais Magufuli amesema hayo leo Mei 02, alipokua akihutubia wanafunzi na uongozi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa;
“Kwa mwaka unatoa bilioni 427, kwa nchi masikini kama Tanzania na unapotoa mkopo ni lazima pawepo na taratibu zinazoendeshwa na watu, mtoto wangu mimi hawezi kupata mkopo, mtoto wa Lukuvi (Waziri wa Ardhi),  mtoto wa Profesa, hata mtoto wa mkuu wa mkoa hatakiwi kupata mkopo,” alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais amesema wanafunzi wa elimu ya juu wanaonufaika na mkopo kwa sasa ni zaidi ya 130,000 ambapo serikali imetoa bilioni 427 licha ya kukumbwa na changamoto ya kubaini wanafunzi hewa  wa elimu ya juu zaidi ya 3500 katika orodha ya wanufaika na mikopo.

Comments

Popular posts from this blog