Posts

Wakali Wanne wa Kimataifa Waitwa Taifa Stars

Image
KOCHA wa Timu ya Taifa ya Soka Tanzania (Taifa Stars), Salum Mayanga, leo Machi 8, ametaja majina ya wachezaji 23 watakaoingia kambini kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki mwezi huu. Katika orodha hiyo aliyoitaja asubuhi hii kwenye makao makuu ya shirikisho la soka nchini TFF Karume Ilala, Mayanga amewajumuisha kikosini nyota wanne wa kimataifa akiwemo nahodha Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu anayechezea klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden, Mlinzi wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda na Faridi Mussa anayechezea Club Deportivo Tenerife ya Hispania. Katika majina hayo 23, Simba imechangia wachezaji 6, Yanga ikitoa wachezaji 5 huku nahodha wa Singida United, Mudathir Yahya naye akijumuishwa kikosini. Taifa Stars inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki ikianzia ugenini nchini Algeria, Machi 22 dhidi ya wenyeji, The Greens kabla ya kurejea nyumbani, Dar es Salaam kuwakaribisha DR Congo, Machi 27, katika Uwanja wa Taifa.

Naibu Wazri Ikupa atekeleza ahadi yake

Image
Naibu Waziri wa sera, Bunge, Kazi, vijana, ajira na walemavu, Mh. Stella Ikupa leo amefanya ziara ya ya kutembelea shule ya Sekondari Jangwani, Uhuru Mchanganyiko na Pugu jiji Dar es salaam na kukabidhi  vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu  . Katika ziara hiyo Mh, Ikupa ametoa Magongo ya kutembelea, viti mwendo, fimbo nyeupe kwa wasiona, miwani ya jua, kofia, lenzi za kusomea kwa watu wenye uono hafifu, na ualubino ili kutatua changamoto kwa kundi hilo maalumu. Naibu Waziri wa sera, Bunge, Kazi, vijana, ajira na walemavu Mh Stella Ikupa akimkabidhi baiskeli mwendo mwanafunzi wa Pugu Sekondari Naibu Waziri  Ikupa amesema kama Serikali tunatambua changamoto hizi hivyo tunajitahidi kukabiliana nazo na kidogo kinachopatikana tunakigawa kwa kila mmoja ili kupunguza matatizo haya kidogokidogo na mwisho wa siku yataisha. Pia serikali hii inayoongozwa na Rais Magufuli itaendelea kutennga fedha kwa ajili ya kuendeleza kuwahudumia watoto weny

Manyara: Mbunge CCM Ahojiwa Sentro kwa Amri ya DC

Image
MBUNGE wa Jimbo la Hangang kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Mary Nagu amehojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Sara Ali,  kwa kile kinachodaiwa kukaidi amri halali ya DC ya kuzuia mikutano ya mbunge huyo. Inadaiwa Nagu na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Mathew Darema, waliwekwa ndani kwa saa kadhaa juzi kabla ya kuhojiwa. Ikumbukwe kuwa, hii ni mara ya pili sasa kwa tukio kama hili kujitokeza kwa  Nagu wilayani humo ambapo Mara ya kwanza DC Sara aliwafikisha polisi Katibu wa CCM Wilaya na Mbunge wake kwa madai kuwa walifanya fujo katiika Kikao cha Kamati ya Siasa cha Wilaya. CREDIT: JF

AJIRA SERIKALINI: MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)- INTERNAL AUDITOR II

Image
INTERNAL AUDITOR II – 2 POST Employer:  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Date Published:  2018-03-05 Application Deadline:  2018-03-19 JOB SUMMARY: N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES: i. Participates in audit assignments of the Fund, including pre auditing of providers’ claims and Board claims/payments; ii. Assists to inspect validity of vouchers, receipts, payments, cheque registers and their respective source documents; iii. Assists to check bank reconciliation statements; iv. Assists in auditing journals and other accounting entries; v. Participates in inspection of goods/stocks received and verifies stock records in the store; vi. Assists in performing all his day to day duties as stipulated and specified in the job description of that position; vii. Assists to review imprests retired, checking adherence to imprests regulations, validity of receipts (if any) and performing any other related clerical works; and viii. Performs any other related duties a

AJIRA SERIKALINI: Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)- ACCOUNTANT II

Image
ACCOUNTANT II – 1 POST Employer:  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Date Published:  2018-03-05 Application Deadline:  2018-03-19 JOB SUMMARY: N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES: Accountant II– Expenditure i. Ensures that all payments are made in accordance with financial regulations and approved budget; ii. Maintains Zonal administrative imprest accounts and ensures timely refunds and replenishments; iii. Oversees the management of the petty cash account; iv. Oversees maintenance of the non-current assets register; v.  Prepares financial statements; vi. Prepares periodic reports on the status of expenditure; vii. Administers and maintains non-current assets register; viii. Maintains subsidiary legers for staff loans; ix. Monitors imprest returns from Zonal offices and takes corrective actions whenever necessary; x. Maintains ledgers for imprest; xi. Monitor and control of salary advances; xii. Deals with all issues pertaining to replenishing funds at

Breaking News:Abdul Nondo apatikana Mafinga mkoani Iringa

Image
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliyekuwa hajulikani alipo tangu usiku wa kuamkia jana na kuacha ujumbe usemao “I AM AT HIGH RISK”, amepatikana Mafinga mkoani Iringa. Mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Paul Kisabo amesema  kwamba Abdul Nondo amepatikana mkoani Iringa katika wilaya ya Mafinga jana jioni baada ya kuzinduka na kujikuta ametupwa barabarani. “Nondo amepatikana Mafinga katika Kituo cha Polisi hivi punde, amezinduka na kujikuta akiwa ametupwa, akauliza watu eneo alipo ndipo wakamwambia yupo Mafinga, amejikokota na kuelekea kituo cha polisi kuripoti. “Kilichomsaidia alikuwa anakumbuka namba mojaya dada yake ambayo alikuwa ameikariri kichwani, ikabidi aombe simu polisi, kumpigia dada yake ambaye naye alijulisha baba yake mdogo aliyepo Dar es Salaam kuwa ndugu yao amepatikana. “Nondo ameongea na baba yake mdogo kupitia simu ya polis

Kikosi cha Simba dhidi ya Waarabu Leo

Image
KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre, tayari ameshakipanga kikosi chake ambacho kitaanza leo Jumatano kwenye mchezo wao dhidi ya Al Masry ya Misri, huku akiwapa jukumu zito la kufunga mabao washambuliaji wake, Emmanuel Okwi na John Bocco. Mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa ni wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika na utaanza majira ya saa 12 jioni, ingawa Lechantre hakufura­hishwa na muda huo uliopangwa na viongozi. Katika mazoezi ya juzi Jumatatu yaliyoanza majira ya saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Boko uliopo jijini Dar, Championi lilimshuhudia Lechantre akipanga kikosi chake kilichoonekana ndicho cha maan­gamizi ambacho kitatumika kum­maliza Mwarabu leo. Katika kikosi hicho ambacho golini yupo Aishi Manula, walinzi wake ni Shomary Kapombe, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Yusuf Mlipili na James Kotei. Kwenye kiungo wapo; Jonas Mkude, Nicholaus Gyan, Shiza Kichuya, Bocco na Okwi. Katika ma­zoezi hayo yaliyomalizika saa 1:30 usiku, kocha huyo

Mwenyekiti Mtandao wa Wanafunzi Hajulikani Alipo

Image
TAARIFA zilizoenea mchana huu zinadai kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na hajulikani alipo tangu jana saa sita usiku. Marafiki za Nondo wamedai alituma ujumbe kwa viongozi wenzake wa TSNP kuwa yuko katika hatari na baada ya kutuma ujumbe huo simu yake ilikuwa ikipokelewa lakini hakuwa akiongea chochote, na baada ya muda alianza kujiondoa kwenye magroup ya WhatsApp. Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa TSNP kuhusu Nondo inasema hajulikani alipo wakiwemo wazazi wake.   Viongozi wa TSNP wamefika Kituo cha Polisi kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na  kutoa taarifa za kupotea kwake. Feb 18, 2018, Nondo alijitokeza na kuikosoa mienendo ya Jeshi la Polisi na Waziri wa Mambo ya Ndani, na mara ya mwisho kuongea na wanahabari, alishinikiza Waziri  Mwigulu Nchemba ajiuzulu. Hivi karibuni pia akizungumza na

TFDA kuzuia soseji kutoka Afrika Kusini zenye bakteria

Image
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imesema itazuia uingizaji wa soseji kutoka Afrika Kusini zilizobainika kuwa na bakteria aina ya listeria. Uamuzi wa TFDA unatokana na soseji hizo aina ya Polony kubainika kuwa na aina hiyo ya bakteria wanaosababisha ugonjwa wa listeriosis uliosababisha vifo vya watu 180 nchini Afrika Kusini. Msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwanza akizungumza na Mwananchi jana alisema mamlaka hiyo inalifanyia kazi suala hilo ikiwa ni pamoja na kuzuia uingizwaji wa soseji hizo nchini, “Tunalifanyia kazi kwa kufanya ukaguzi na kujiridhisha kama soseji husika zipo katika soko,” alisema. Soseji hizo kwa mujibu wa habari zilizochapishwa na vyombo kadhaa vya kimataifa zinatengenezwa na kiwanda cha tiger brands unit enterprises na cha RCL foods vyote vya Afrika Kusini. Waziri wa Afya wa Afrika Kusini, Aaron Motsoaledi alikaririwa na mitandao ya kijamii akisema ameagiza kuondolewa sokoni soseji hizo, huku akiwashauri wananchi kuacha kula. Mot

Tanzia:Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma mjini afariki dunia Muhimbili

Image
ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Dkt. Amani Walid Kabourou amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. Dkt. Kabourou ambaye alizaliwa Mei 23, 1949, amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CHADEMA) kabla ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma. Aidha, Dkt. Kabourou amewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki akiiwakilisha Tanzania kuanzia Juni 05, 2007 hadi Juni 04, 2012. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa sasa wa Kigoma Mjini amesema kwao huo ni msiba mkubwa, na umewaacha na majonzi tele. “Tumeamka asubuhi na habari za kusikitisha kuwa Dkt. Amani Walid Kabourou, Mbunge Mstaafu wa Kigoma Mjini ametangulia mbele ya haki. Hakika ni msiba mkubwa kwetu. Mola ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,” ameandika Zitto.

MAGAZETI YA LEO 5/3/2018

Image

Fahamu Madhara Ya Usukaji Wa Nywele Bandia Na Uvaaji Wa Mawigi

Image
Katika karne ya sasa , uvaaji wa wigi umekuwa fasheni katika sekta ya urembo na hutumika hususan na wanawake. Ingawa uvaaji wa wigi huwafanya wanawake hao kuonekana ni walimbwende zaidi. Wigi huvaliwa zaidi na kinamama wenye asili ya Afrika au Wamarekani wa asili ya Afrika. Lakini tukiangalia moja ya chimbuko hasa la uvaaji wigi ni ubaguzi uliokuwepo wakati wa utumwa ambapo wale wenye ngozi nyeupe na nywele shombeshombe walipewa kazi za ndani na wale wasio na ngozi nyeupe  na nywele zisizo shombeshombe walifanyishwa kazi ngumu za mashambani. Watumwa waliopelekwa barani Amerika hawakuweza kuzihudumia nywele zao kutokana na hali ngumu, na mabwenyenye waliwashusha hadhi na kuwavunja moyo kwa kuwaambia hawakuwa na nywele bali ni "manyoya". Lakini sababu nyingine inayodhaniwa kuwaathiri wanawake wa asili ya Afrika ni fikra kuwa mwanamke mwenye nywele ndefu pengine hadi mgongoni ni mrembo zaidi. Pia siku hizi warembo na wanaoshiriki katika mashindano ya urem

Ikulu Yakanusha Taarifa Dhidi Ya Waziri Hamis Kigwangala

Image
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa amekanusha kuwa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala kwa mujibu wa barua inayosambaa kwenye mitandao kuwa ni uzushi na imetengenezwa na wahalifu.        Alichokisema Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa. Barua inayosambaa kwenye mitandao ambayo imetengenezwa na wahalifu.

DIAMOND KULAMBA SHAVU KOMBE LA DUNIA SIRI YAFICHUKA!

Image
DAR ES SALAAM: Nyuma ya tukio la Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kulamba shavu la kuimba wimbo wa uzinduzi wa Michuano ya Kombe la Dunia 2018, Ijumaa Wikienda limebaini siri iliyochangia uteuzi wake huo. Katika uchunguzi mdogo uliofanywa na gazeti hili, mambo matatu makubwa ambayo ndiyo sababu kubwa iliyowafanya waandaaji wampe kipaumbele rais huyo wa Wasafi Classic Baby (WCB). Ijumaa Wikienda lilibaini kuwa, jambo la kwanza lililochangia Diamond ateuliwe ni bidii ya uongozi wake chini ya Sallam SK. Sallam ametajwa kuwa miongoni mwa mameneja ambao wana ‘connection’ nyingi za vituo vikubwa vya redio na televisheni ambavyo hucheza nyimbo za Diamond duniani. Ilielezwa kuwa, connection hizo ndizo zilizochangia kuwashawishi waandaaji wa michuano hiyo wakati walipokuwa wanaangalia ni wasanii gani wa Afrika ambao wana uwezo na ushawishi mkubwa, wakampendekeza Diamond. Mbali na hilo, jambo lingine lililochangia Diamond ateuliwe na kushiriki katika uzinduzi wa mashindano

BREAKING NEWS : AJALIMBAYA DALADALA YAGONGANA NA GARI LA TAKA,LASABABISHA VIFO NA MAJERUHI DODOMA

Image
Watu sita wamefariki dunia papo hapo huku wengine sita kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria kugongana na lori mkoani Dodoma. Eneo la ajali ambapo watu sita wamefariki baada Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Gillece Muroto amesema ajali hiyo imetokea leo Jumapili Machi 4, 2018 majira ya mchana ambapo daladala aina ya Toyota Hiace iliyokuwa na abiria kugongana na lori la kubebea taka. Taarifa zaidi nitazitoa baada ya kufuatilia lakini kwa ufupi ajali hiyo ipo na watu sita wamekufa na wengine sita wapo katika hospitali ya rufaa ya mkoa na hali zao sio nzuri,” amesema Muroto kwenye mahohjiano na Gazeti la Mwananchi.

Kilimo Bora Cha Viazi Vitamu

Image
Viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi nchini Tanzania ambalo hulimwa kwa ajili ya chakula. Zao hili ni moja kati ya mazao ya kinga ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame. Zao la viaViazi vitamu, asilia yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Morogoro,Kagera,Arusha na Ruvuma. Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa katika njia mbalimbali kama vichembe, na Matobolwa. Pia Unga wa viazi vitamu hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati na tambi. Majani ya viazi huliwa kama mboga pia hutumika katika kutayarisha mboji. Aina za viazi vitamu Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni. Hapa nchini Tanzania aina zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega, Karoti C, Mwananjemu, Ali mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli, Sinia,Vumilia na Polista. Faida: vina wanga, vitamin, kambalishe, madini ya kalisiuamu, potasiamu, chu

Breaking News: Moto Waunguza Shule ya Wasichana Korogwe

Image
Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe  iliyoko wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga, inaungua moto usiku huu, huku chanzo cha ajali ya moto huo kikiwa hakijajulikana. Inadaiwa watu kadhaa wamejeruhiwa kutokana na moto huo. Hakuna vifo vilivyoripotiwa ama kuthibitishwa hadi sasa. Tunaendelea kufuatilia kwa kina, taarifa zaidi tutakuletea baadaye.

Breaking News: Watano Wafariki Basi la New Force Kugongana na Hiace

Image
WATU watano wamefariki dunia leo asubuhi baada ya basi la New Force lilikokuwa linatokea Msamvu kwenda Mikese kugongana na gari dogo la abiria (Hiace) lililokuwa linatokea Msamvu, mkoani Mogororo. Pia watu kadhaa ambao idadi yao bado haijajulikana, wamejeruhiwa. Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema chanzo ni dereva wa gari hilo la Hiace kutaka kulipita gari la mchanga lililokuwa mbele ambapo lilijikuta likigongana uso kwa uso na basi hilo.