Naibu Wazri Ikupa atekeleza ahadi yake

Naibu Waziri wa sera, Bunge, Kazi, vijana, ajira na walemavu, Mh. Stella Ikupa leo amefanya ziara ya ya kutembelea shule ya Sekondari Jangwani, Uhuru Mchanganyiko na Pugu jiji Dar es salaam na kukabidhi  vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu  .

Katika ziara hiyo Mh, Ikupa ametoa Magongo ya kutembelea, viti mwendo, fimbo nyeupe kwa wasiona, miwani ya jua, kofia, lenzi za kusomea kwa watu wenye uono hafifu, na ualubino ili kutatua changamoto kwa kundi hilo maalumu.

Naibu Waziri wa sera, Bunge, Kazi, vijana, ajira na walemavu Mh Stella Ikupa akimkabidhi baiskeli mwendo mwanafunzi wa Pugu Sekondari
Naibu Waziri  Ikupa amesema kama Serikali tunatambua changamoto hizi hivyo tunajitahidi kukabiliana nazo na kidogo kinachopatikana tunakigawa kwa kila mmoja ili kupunguza matatizo haya kidogokidogo na mwisho wa siku yataisha.

Pia serikali hii inayoongozwa na Rais Magufuli itaendelea kutennga fedha kwa ajili ya kuendeleza kuwahudumia watoto wenye ulemavu hivyo kikubwa tuendelee kushirikiana ili kwa pamoja tutatue changamoto hizi kwa kundi lenye lenye mahitaji maalumu kwa kadri iwezekanavyo


Hata hivyo ametoa wito kwa wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu kujikita kwenye elimu ndio mkombozi wa maisha yao kwani pasipo na  elimu au ujuzi wowote wanaweza kurudi mtaani na kuwa ombaomba, pia kutokana na serikali hii kuwa sikivu tunaendelea kuboresha miundombinu kwa kukarabati kadri siku zinavyoenda na isiwe tena kuwa kikwazo cha kukosa elimu.

Aidha Makamu mkuu wa shule ya Jangwani Eunsta Siara akisoma taarifa mbele ya  Mh. Ikupa amesema kuwa kundi hilo lina changamoto mbalimbali ikiwa pamoja sehemu ya maabara sehemu za kulala walemavu, majengo hivyo kama serikali isaidia kukamilisha vitu hivyo ili pasiwe na kikwazo cha kukwamisha elimu kwa kundi hilo maalum.

Naibu Waziri wa sera, Bunge, Kazi, vijana, ajira na walemavu Mh Stella Ikupa akikabidhi baadhi ya vifaa shule ya Sekondari Jangwani
Cosmas Antony ambae ni mwanafunzi wa Kidato cha tatu  Pugu sekondari amefurahi na kumpongeza Mh. Ikupa kwa kutekeleza ahadi yake kwani mwaka jana aliahidi kuleta vifaa ambavyo vitatusaidia kurahisishia mazingira ya kupata elimu bora na amefanya hivyo.

Comments

Popular posts from this blog