Posts

Breaking: Ripoti ya TRA Kuhusu Utajiri wa Kakobe, Amuomba Radhi JPM

Image
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema wakati wakiendelea kumchunguza Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel, Zachary Kakobe , mnamo Januari 24, 2018, Askofu huyo alimuandikia barua Rais Dkt. John Magufuli kumuomba radhi kutokana na kauli yake ya kebehi na matamshi ya dharau kuwa ‘ana pesa nyingi kuliko Serikali’. Hayo yamesemwa leo na Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere , wakati akizunumza na wanahabari jijini dar es Salaam akitoa ripoti ya uchunguzi huo. Akihubiri wakati wa mkesha wa sikukuu ya Krismasi, Desemba 24, mwaka jana, askofu huyo alisema yeye ni tajiri zaidi ya serikali ya Tanzania na baadaye kusema kuwa utajiri anaomiliki kwa sasa ni zaidi ya serikali nyingi duniani jambo ambalo liliwafanya TRA wamchunguze.

RATIBA KUAGWA MWILI WAMAREHEMU AKWILINA DAR

Image
BAADA ya maridhiano ya kuuchukua mwili katika Hospitali ya Taifa Mhimbili, familia ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi imetoa ratiba ya kuagwa kwa mwili w binti huyo. Akizungumza baada ya kupokea ripoti ya mwili wa marehemu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kaka wa marehemu, Moi Kiyeyeu alisema kuwa mdogo wake ataagwa Alhamisi hii Februari 22, katika viwanja vya Chuo cha NIT kilichopo Mabibo jijini Dar na baadaye atasafirishwa kwenda nyumbani kwao Rombo-Mashati mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi. Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, ripoti ya uchunguzi waliyopewa na madaktari wa Muhimbili inaonesha kuwa marehemu alipigwa risasi kichwani iliyoingia upande wa kushoto na kutokea upande wa kulia. “Ripoti tuliyopewa inaonesha kichwa cha marehemu kilipasuliwa na risasi ambayo iliingia upande wa kushoto na kutokea upande wa kulia ambao umefumuliwa vibaya,” shemeji wa Akwilina, Festo Kavis...

Mbowe, Mashinji, Mnyika na Wengine 4 Waitwa kwa DCI Kuhojiwa

Image
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na viongozi wengine 6 wa chama hicho wameitwa rasmi Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa. Viongozi hao wanatuhumiwa kwa kufanya maandamano kinyume cha sheria kwa mujibu wa barua hiyo ya wito kutoka kwa Jeshi la Polisi. Viongozi wengine 6 walioitwa ni; – Dkt Mashinji(Katibu Mkuu wa CHADEMA) John J. Mnyika(Mbunge na Naibu Katibu Mkuu Bara) Salum Mwalim(Naibu Katibu Mkuu ZNZ) Halima Mdee(Mbunge na M/Kiti wa BAWACHA) John Heche(Mbunge) Ester N. Matiko(Mhazini wa BAWACHA).

ZARI KUMPIGA KIBUTI DIAMOND KWAIBUA MAMBO MAPYA,KWANINI ZARI KAUMIZWA UJEREO WA WEMA SEPETU NA SI HAMISA MOBETO

Image
SIKU chache baada ya Zarinah Hassan ‘Zari Boss Lady’ kuweka wazi kuwa ameachana na baba watoto wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, swali linakuja ni kwa nini Zari anaweza kuwa ameumizwa sana na Wema Abraham Sepetu na si Hamisa Mobeto ambaye hivi karibuni amempa msongo wa mawazo baada ya kuzaa na baba watoto wake? Twende taratibu! Kwanza nauliza swali hilo ambalo nitaliweka wazi baadaye kidogo na kadiri unavyoendelea kusoma makala haya, utanielewa. Baada ya matukio yote ya Diamond na Mobeto, bado Zari alionekana kuwa ‘jiwe’ na kutetea penzi lake lakini lilipokuja suala la shoo ya Mboso ambayo Diamond alionekana wazi kuwa na mahaba na Wema kwa video yao ya ‘kupapasana’ kuwekwa mitandaoni, siku chache baadaye Zari aliamua kutangaza rasmi kummwaga Diamond. Sababu ya wadau na mashabiki wa Baba Tiffah na Mama Tiffah kuona kuwa hiyo itakuwa imemuudhi Zari ni jinsi wapendanao hao walivyopotezeana hata kabla ya Zari kutangaza kuachia ngazi na muda mwingi akaonekana kuu...

Mke na Mme Waliokamatwa na Madawa China, Familia Yaanika A-Z

Image
Baraka Malali na mkewe pamoja na mtoto wao. Sakata la Watanzania wawili ambao ni mke na mume kukamatwa na dawa za kulevya ‘unga’ nchini China na mtoto wao kurudishwa Bongo , limeingia sura mpya, baada ya familia za pande zote mbili kuzungumza na siri ya safari yao kufichuka, Ijumaa Wikienda lina ukweli wa tukio hilo. Wakazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam , Baraka Malali na mkewe Ashura Musa walikamatwa Januari 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Baiyun jijini Guangzhou, China wakiwa wamemeza jumla ya pipi 129 za dawa za kulevya zilizosadikika kuwa ni heroin. Mume alipakia pipi 47 na mkewe pipi 82. Taarifa zilieleza kuwa, mamlaka nchini humo ziliamua kumrudisha nyumbani mtoto wao ambaye aliwasili Bongo wikiendi iliyopita kukabidhiwa kwa Ustawi wa Jamii, wakati mipango ya kumkabidhi mtoto huyo kwa ndugu wa wazazi wake ikiendelea. Baada ya kujiri kwa tukio hilo, Ijumaa Wikienda lilizungumza na wazazi wa watuhumiwa hao na Idara ya Ustawi wa Jamii kujua kw...

Breaking News: Salum Mwalimu Akamatwa na Polisi

Image
Mgombea ubunge wa Chadema Kinondoni, Salum Mwalimu. MGOMBEA  ubunge wa Chadema Kinondoni, Salum Mwalimu amekamatwa na polisi kituo cha kupigia kura cha Idrisa Kata ya Magomeni. Akizungumza na Global TV Online mchana huu Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene amethibitisha kukamatwa kwa mgombea huyo.

Diamond Platnumz ateswa na maamuzi ya Zari

Image
 Leo February 16,2018 Diamond Platnumz ameonekana kuonyesha hisia zake juu ya maamuzi  ya Zari kuachana nae, kupitia instagram account yake Diamond amekuwa akipost video clips mbalimbali za nyimbo za mapenzi. Kupitia instagram ya Diamond Platnumz amepost kipande cha wimbo wake wa Sikomi na kuandika “Unajua Nyimbo zingine Unaziimba ila Hata we mwenyewe zinakuingia Baadae😟…. Anyways 28 Days Before the Reveal of #AboyFromTandaleAlbum!🔥 #SikoMi Bonus Track on #AboyFromTandale Available on All Digital Platforms now!”

Wananchi Wamkataa Mkuu Wa Wilaya Mbele Ya Waziri Mkuu

Image
WANANCHI wa wilaya ya Kwimba wamemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aondoke na mkuu wa wilaya hiyo Bw. Mtemi Msafiri baada ya kutoridhishwa na utendaji wake. Wametoa ombi hilo jana (Ijumaa, Februari 16, 2018) walipozuia msafara wa Waziri Mkuu alipowasili katika Ofisi za Halmashauri ya wilaya Kwimba zilizopo Ngudu kwa ajili ya kuzungumza na watumishi akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. Wananchi hao walimkataa mkuu wao wa wilaya Bw. Msafiri kupitia ujumbe wa mabango 17, ambapo Waziri Mkuu amewataka wananchi hao wawe watulivu wakati Serikali inafanyia kazi malalamiko yao. Wananchi hao wanadai kwamba Mkuu huyo wa Wilaya anatabia ya kuamrisha polisi wawakamate kwa kisingizio cha uzururaji na kisha wanawekwa mahabusu, ambapo baada ya muda wanatolewa na kwenda kulima kwenye shamba lake. Waziri Mkuu amesema Serikali inahitaji kila mtumishi atambue majukumu yake na ayatekeleze. “Hakuna atakayeonewa, haki zenu zote tunazitekeleza nanyi mnataki...

Mwanamume aliyejibadilisha jinsia 'amnyonyesha mtoto'

Image
Mwanamume aliyejibadilisha jinis na kuwa mwanamke amefanikiwa kumyonyesha mtoto katika kisa cha kwanza cha iana yake kuwahi kushuhudiwa, watafiti wanasema. Mwanmke huyo mwenye umri wa miaka 30 alitaka kumnyonyesha mtoto baada ya mpenzi wake aliyejifungua kusema hataki kumnyonyesha mtoto huyo, hayoni kwa mujibu wa wa jarida la afya la watu waliojibadili jinsia. Alifanikiwa kunyonyesha baada ya kumeza dawa na kukamua maziwa, ripotihiyo inasema kutoka nchini Marekani. Mtaalamu wa Marekani anasema utafiti huo huenda ukachangia visa zaidi vya wanaume walijibadilisha jinsia kuwa wanawake kunyonyesha watoto. Mwanamke huyo aliyekuwa anapokea matibabu ya kubadili homoni zake mwilini kwa muda wa miaka 6, lakini hajafanyiwa upasuaji kubadili sehemu zake za siri, wakati alipowaomba madaktari wamsaidie atimize lengo lake la kumnyonyesha mtoto. Kabla ya mtoto huyo kuzaliwa, madakatari walimpadawa za miezi mitatu unusu kumsaidia kupata maziwa, kwa kawaida dawa hizo hupewa ...

DIAMOND PLATINUMZ NA RUGE TENA,WATAJWA NA MGOMBEA UBUNGE KINONDONI

Image
Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM, Maulid Mtulia ameahidi kuwatumia Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba kunyanyua vipaji katika jimbo hilo ili kuongeza fursa ya ajira.    Mhe. Mtulia amesema hayo leo Ijumaa Februari 16, 2018 katika viwanja vya Biafra wakati akijinadi kwenye kilele cha kampeni ya uchaguzi mdogo wa jimbo hilo. Hata hivyo, Mtulia amewahakikishia wapenzi wote wa soka jimboni humo kuwa ataisaidia timu ya KMC FC iliyopanda daraja kwenda Ligi Kuu kwa hali na mali ifanye vizuri ili kukuza kwa urahisi vijana wengine wenye vipaji. Kwa upande mwingine Mtulia amesema wakazi wa Kinondoni wasihadaike kwa lolote kuchagua viongozi wa vyama vingine kwani yeye anajua matatizo ya vyama hivyo ndio maana aliamua kuhamia CCM akitokea CUF.

Mgombea Ubunge Maulid Mtulia apiga kura yake

Image
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Maulid Mtulia, amepiga kura asubuhi hii ya Feb. 17, 2018 katika kituo cha Friends Corner huko Kata ya Ndugumbi jijini Dar es Salaam.

Makamuzi Ya Mapacha Watatu Si Mchezo

Image
Jose Mara akiwajibika jukwaani. Mpiga besi gitaa wa Mapacha Watatu Vincent Munisi akiwajibika jukwaani. Chaz Baba Kingunge naye akiwajibika. Wanenguaji wakifanya yao. Bendi ya Mapacha Watatu Music Band chini ya Jose Mara usiku wa kuamkia leo ilifanya makamuzi kwenye ukumbi wa Safari Pub, Mtoni Kijichi jijini Dar. Katika onesho hilo Bendi hiyo ilifanya makamuzi ya nguvu ambapo leo Jumamosi itafanya makamuzi Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Mori jijini Dar.

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Aapishwa

Image
Rais John Magufuli amemuapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed. Luteni Jenerali Mohamed ameteuliwa jana Februari 14, 2018 kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ na kupandishwa cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali. Luteni Jenerali Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali, James Mwakibolwa ambaye amestaafu. Mbali na uteuzi huo, Rais Magufuli pia amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali J.G. Kingu, M.S. Busungu, R.R. Mrangira, B.K. Masanja, G.T. Msongole, A.F. Kapinga, K.P. Njelekela, A.S. Bahati, M.E. Mkingule na S.S. Makona. Taarifa ilitotolewa Ikulu jana imesema mabrigedia jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye. Kabla ya kuapishwa kwa Luteni Jenerali Mohamed, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Venance Mabeyo aliwavalisha vyeo mameja jenerali waliopandishwa vyeo na Rais Magufuli.

NAFASI ZA KAZI PRECISION AIR SERVICES PLC

Image
Precision Air Services Plc is a fast growing private Tanzanian airline which operates in partnership with Kenya Airways, with its strategies to expand wings beyond East Africa and Africa. In order to keep our services at a higher level and meet our customers’ maximum satisfaction, we wish to invite applications from suitably qualified candidates to fill in this challenging positions. POSITION: PILOT IN COMAND ATR 42/72   REPORTS TO: FLEET CAPTAIN DUTY STATION: DAR ES SALAAM ROLE PURPOSE STATEMENT: To plan, supervise and execute company flights in accordance with legal and company policies and procedures for safe, efficient and economic conduct of flights. Duties and Responsibilities It is the responsibility of the PIC to ensure the safe and efficient operation of the aircraft in all stages of ground and flight operations. Plan, and supervise the execution of company flights in accordance with legal and company policies and procedures, authoriz...

Nafasi za Kazi Medical Stores Department (MSD), February 2018

Image
Ref.No.EA.7 /96/01 /J/83  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PRESIDENT’S OFFICE  February 12, 2018 PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT  VACANCIES ANNOUNCEMENT President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat on behalf of the Medical Stores Department (MSD), invites qualified Tanzanians to fill one (1) vacant post as mentioned below; 1.0 BACKGROUND  1.1 MEDICAL STORES DEPARTMENT ( MSD )  Medical Stores Department (MSD) is a semi-autonomous Department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children, established by Act of Parliament No.13 of 1993 with an objective of developing and maintaining an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of health commodities required for use by the public and accredited faith based health facilities. MSD is at a very exciting stage of reforming its operations, systems and processes with the aim of becoming a highly effectiv...

Ajira: Wildlife Biologist/Ecologist Jobs, (WWF), February 2018

Image
JOB VACANCY  Wildlife Biologist/Ecologist  WWF (The World Wide Fund for Nature) is an international non-governmental organization that deals with conservation of nature through a number of environmental management programmes. Our mission is to stop the degradation of the Planet’s natural environment and to build a future in which human live in harmony with nature. WWF-Tanzania Country Office (WWF-TCO) is seeking to hire the ‘Wildlife Biologist/Ecologist” to be based in Tunduru.  I. Major Functions:  This is a field based position and responsible for studying the life processes of animals and their environment as well as wildlife population dynamics. Monitoring plant and animal habitats, determines which animals are affecting nature in a detrimental way, and helps restore and conserve animal habitats within the WMAs, buffer areas of Selous Game Reserve and the Selous-Niassa Wildlife Corridor. The officer will be the lead person for designin...

ESMA: SIPENDI KUMTEGEMEA DIAMOND

Image
D ADA wa mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Khan amesema hapendi kumtegemea mdogo wake huyo katika shughuli zake licha ya kuwa anaamini anaweza kumsaidia sana. Akizun-gumza na Amani, Esma alisema siku zote anataka ajivunie mafa-nikio yake, atembee mwen-yewe na ndiyo maana hata alipofungua duka la nguo, hakutaka kumsumbua Diamond wala wifi yake, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’. “Najua kabisa kaka yangu na wifi yangu wana watu wengi kwenye mitandao yao lakini nilitamani sana kwenye mafanikio yangu nisimame mwenyewe ili nijue changamoto zake, kweli nimeweza,” alisema Esma. Esma na Diamond ‘wanashea’ mama, kila mmoja ana baba yake.

Vyakula Kumi 10 Vya Kuongeza Kinga Ya Mwili

Image
Watu wengi tumekuwa tukijali kazi zetu za kila siku bila kujali hali ya afya zetu matokeo yake kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya ghafla. Suala la kula pengine ndilo nguzo ya kwanza ya afya ya binadamu Mwili ukiwa sawia bila shaka utaweza kufanya mambo yako yote, na usipokuwa sawa basi hutaweza kutimiza lengo lako lolote! Hivi ni yakula kadhaa vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga ya Mwili wako 1.Yogurt ( Maziwa mtindi ) Hutengenezwa kwa kutumia maziwa ya ng’ombe na kimea, hupatikana kwa ladha mbalimbali kulingana na matakwa yako, yogati pengine ndio chakula kinachoongoza kwa kuogeza Kinga ya mwili wako. 2. Matunda Yanapatikana sehemu yoyote duniani kwa bei unazozimudu, katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, matunda asiyekula matunda anahatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda. 3. Vitunguu saumu Hupatikana Kila soko Tanzania! Japokuwa vitunguu saumu vimekuwa ...

Breaking News: Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini Ajiuzulu

Image
HATIMAYE Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ametangaza kujiuzulu urais wa nchi hiyo usiku huu ikiwa ni siku chache baada ya chama chake cha ANC kuanzisha vuguvugu la kumng’oa madarakani. Akitangaza uamuzi huo, Zuma amesema asingependa damu imwagike na chama(ANC) kimeguke kwa sababu yake. ANC kikiongozwa na Cyril Ramaphosa, siku chache zilizopit kilituma ujumbe maalum kumtaka rais huyo kuachia madaraka, kutokana na harakati nyingi za kumtaka afanye hivyo tangu mwaka jana. Jacob Zuma anakabiliwa na tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya madaraka ambapo Bunge la nchi hiyo kujaribu kupiga kura za maoni ili kumuondoa lakini ilishindikana, ndipo chama kikafanya mkutano na kuchukua uamuzi huo mgumu wa kumtaka afanye hivyo, la sivyo kitamtoa kwa nguvu. Zuma amefuata nyayo alizopita rafiki yake mkubwa Robert Mugabe ambaye alikuwa Rais wa Zimbabwe, aliyetakiwa kufanya hivyo mwishoni mwa mwaka 2017 na jeshi la nchi hiyo, la sivyo lingetumia nguvu kumng’oa, na hatimaye kuac...

Zari Atangaza Rasmi Kuachana na Diamond

Image
IKIWA ni siku ya wapendanao,  leo Februari 14, 2018, Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari the Boss Lady ametangaza kuvunja rasmi mahusiano yake ya kimapenzi na Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Kupitia ukurasa wake wa Instagaram, Zari amefunguka kuwa kilichompelekea kufanya hivyo ni kutokana na Diamond kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano yao huku akibainisha kuwa kuachana katika mahusiano ya kimapenzi hakutaathiri uhusiano wao kama wazazi. Diamond ambaye alianza mahusiano na Zari takribani miaka mitano iliyopita baada ya kuachana na staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu, amezaa na Zari watoto wawili ambao ni Tiffah na Nilan huku pia akitajwa kuchepuka jambo ambalo limepelekea akazaa mtoto mwingine na mwanamitindo Hamissa Mobeto. Mbali na Mobeto, Diamond amekuwa akihusishwa kurudiana na Wema ambapo hivi karibuni walionekana kugandana kwenye hafla ya kutambulishwa kwa msanii Mbosso kwenye lebo ya WCB Wasa...