DIAMOND PLATINUMZ NA RUGE TENA,WATAJWA NA MGOMBEA UBUNGE KINONDONI

Mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM, Maulid Mtulia ameahidi kuwatumia Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba kunyanyua vipaji katika jimbo hilo ili kuongeza fursa ya ajira.    Mhe. Mtulia amesema hayo leo Ijumaa Februari 16, 2018 katika viwanja vya Biafra wakati akijinadi kwenye kilele cha kampeni ya uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
Hata hivyo, Mtulia amewahakikishia wapenzi wote wa soka jimboni humo kuwa ataisaidia timu ya KMC FC iliyopanda daraja kwenda Ligi Kuu kwa hali na mali ifanye vizuri ili kukuza kwa urahisi
vijana wengine wenye vipaji.

Kwa upande mwingine Mtulia amesema wakazi wa Kinondoni wasihadaike kwa lolote kuchagua viongozi wa vyama vingine kwani yeye anajua matatizo ya vyama hivyo ndio maana aliamua kuhamia CCM akitokea CUF.

Comments

Popular posts from this blog