ESMA: SIPENDI KUMTEGEMEA DIAMOND

DADA wa mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Khan amesema hapendi kumtegemea mdogo wake huyo katika shughuli zake licha ya kuwa anaamini anaweza kumsaidia sana. Akizun-gumza na Amani, Esma alisema siku zote anataka ajivunie mafa-nikio yake, atembee mwen-yewe na ndiyo maana hata alipofungua duka la nguo, hakutaka kumsumbua Diamond wala wifi yake, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
“Najua kabisa kaka yangu na wifi yangu wana watu wengi kwenye mitandao yao lakini nilitamani sana kwenye mafanikio yangu nisimame mwenyewe ili nijue changamoto zake, kweli nimeweza,” alisema Esma.
Esma na Diamond ‘wanashea’ mama, kila mmoja ana baba yake.

Comments

Popular posts from this blog