ZARI KUMPIGA KIBUTI DIAMOND KWAIBUA MAMBO MAPYA,KWANINI ZARI KAUMIZWA UJEREO WA WEMA SEPETU NA SI HAMISA MOBETO
SIKU chache baada ya Zarinah Hassan ‘Zari Boss Lady’ kuweka wazi kuwa ameachana na baba watoto wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, swali linakuja ni kwa nini Zari anaweza kuwa ameumizwa sana na Wema Abraham Sepetu na si Hamisa Mobeto ambaye hivi karibuni amempa msongo wa mawazo baada ya kuzaa na baba watoto wake? Twende taratibu! Kwanza nauliza swali hilo ambalo nitaliweka wazi baadaye kidogo na kadiri unavyoendelea kusoma makala haya, utanielewa. Baada ya matukio yote ya Diamond na Mobeto, bado Zari alionekana kuwa ‘jiwe’ na kutetea penzi lake lakini lilipokuja suala la shoo ya Mboso ambayo Diamond alionekana wazi kuwa na mahaba na Wema kwa video yao ya ‘kupapasana’ kuwekwa mitandaoni, siku chache baadaye Zari aliamua kutangaza rasmi kummwaga Diamond. Sababu ya wadau na mashabiki wa Baba Tiffah na Mama Tiffah kuona kuwa hiyo itakuwa imemuudhi Zari ni jinsi wapendanao hao walivyopotezeana hata kabla ya Zari kutangaza kuachia ngazi na muda mwingi akaonekana kuu