Madiwani watatu Chadema wahamia CCM
Chadema katika Halmashauri ya Tunduma, wilaya ya Momba mkoani Mbeya kimepata pigo baada ya madiwani wake watatu kuhamia CCM. Madiwani hao na kata zao katika mabano ni Ayub Mlimba (Mwaka Kati), Simon Mbukwa (Kaloleni) na Amos Nzunda (Mpemba) na walitambulishwa jana mchana katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Jumaa Irando. Wakizungumza na Mwananchi madiwani hao waliohamia CCM wamesema wamechukua uamuzi huo baada ya kuona Chadema kimepoteza mwelekeo Tunduma, huku viongozi wake wakitoa amri za kibabe wakitaka wanachama kutozungumza chochote. “Unajua baraza la madiwani Tunduma linaundwa na Chadema, sasa tunapewa maagizo ya nini cha kuzungumza na kusimamia hata kama hayaendani na mahitaji ya wananchi wetu kwa lengo tu la watu wachache ndani ya chama,” alisema Nzunda. Mlimba alisema sababu ya kuhamia CCM ni kufurahishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli huku Mbukwa akieleza sababu yake kuondoa Chadema kuwa ni mvutano na mtafar...