AIBU YA MWAKA..! WANASWA LIVE WAKIFANYA UFUSKA KAZINI!

Baada ya kunaswa.

NI aibu kubwa! Tangu kuanza kwa mwaka 2018, yapo yaliyotokea na kusisimua, lakini hili la mrembo kunaswa na mwanaume wakifanya ufuska kwenye eneo la kazi, limeibua hisia za aina yake kuwa huenda maisha hayaendi, Ijumaa Wikienda linaifumua.
Habari kamili, tukio hilo lilijiri kwenye eneo la kazi la mrembo huyo ambalo ni saluni inayojihusisha na vitendo vya ’masaji’ lakini yeye akadaiwa kucheza mchezo wake wa ngono.
Saluni hiyo ipo maeneo ya Sinza-Kwaremy jijini Dar ambapo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikidaiwa kujihusisha na uchafu huo na kusababisha kero kwa wananchi wenye maadili yao.
…Akiwa uchi baada ya kunaswa.

OFM KAZINI
Kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, kikiwa kimetulia ndani ya mjengo wa makao yake makuu, Sinza-Mori jijini Dar, kilipokea simu kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi
 wa saluni hiyo akimshitakia mwenzake kuwa amekuwa akijihusisha na ufuska na wanaume mbalimbali wakiwemo waume za watu na waheshimiwa ambao hufika mahali hapo kutaka huduma halali ya kuchua mwili.
Chanzo: Halooo…., hapo ni Makao Makuu ya OFM?

OFM: Ndiyo dada, tukusaidie nini?
Chanzo: Mna habari jamani?
OFM: Zimejaa tele, ila hata ya kwako inaweza kuwa bora kuliko tulizonazo.
Chanzo: Hapa Sinza (Dar), kuna saluni moja, kuna dada ni mfanyakazi mwenzetu lakini tumemshindwa kwa vitendo vichafu vya ngono.
OFM: Kivipi? Hebu fafanua tafadhali!
Chanzo: Mkija maeneo haya sisi tutawalengesha mfanye uchunguzi wenu.

Eneo la tikio.

OFM MZIGONI
Bila kupoteza sekunde, OFM ilianza uchunguzi wake mara moja ambapo ilifika eneo hilo na kumuulizia dada huyo ambaye tayari chanzo kilishawatajia jina.

UCHUNGUZI
Mmoja wa makamanda wa OFM alijitosa ndani ya saluni hiyo ambapo alipokelewa na mhusika huyo kwa bashasha kisha akapewa utaratibu wa kulipia huduma ikiwemo hiyo ya ngono.
Baada ya kupewa utaratibu huo, OFM aliomba kwenda kujiandaa kwa kuwa hakubeba kiasi cha fedha cha kutosha huku mrembo huyo akihuzunika na kumuomba chondechonde arejee kwa huduma safi ya ngono.
Uchunguzi huo ulibaini kuwa, mrembo huyo hujifanya anatoa huduma ya kuchua mwili (body massage) kama ilivyosajiliwa saluni hiyo kwa Sh. 30,000/= kwa huduma za kawaida.

Ni hatari.


HUDUMA
Katika upelelezi huo, ilibainika kuwa mteja akilipia gharama ana uhuru wa kuchagua kama atapenda kufanyiwa huduma ya uchuaji kwa mikono tu au kwa matiti na wakati mwingine mwili mzima huku mtoa huduma hiyo akiwa amevua nguo zote!
Ikazidi kubainika kuwa, endapo mhudumiwaji atataka huduma hiyo ya mchuaji kuvua nguo zote, atafanyiwa hivyo, lakini kama atazidiwa na kuhitaji huduma ya ngono, atatakiwa kuongeza Sh. 30,000/= kwa msichana huyo wa huduma na kufanya gharama kuwa zaidi ya Sh. 60,000/=.
“Amekuwa akifanya vitendo viovu sana, yaani ngono nje-nje, jamani hii siyo saluni, bali ni danguro la ngono, fuatilieni mtagundua juu ya ukweli huu,” alisema mmoja wa wafanyakazi wenzake aliyevujisha ishu hiyo.
Siku kadhaa baada ya uchunguzi, OFM alirejea na polisi ambao waliweka mtego na kubaini ukweli wa kile kilichokuwa kikisemekana baada ya mtego kufyatuka.
Mmoja wa vijana wa OFM alijifanya anahitaji huduma hiyo ya kufanyiwa masaji mwili mzima ambapo mrembo huyo alichangamkia ‘tenda’ fastafasta bila kujua mteja huyo hakuwa mteja kama walivyo wengine bali alikuwa ‘mteja wa moto’.
Katika mtego huo, OFM na polisi walishirikiana katika oparesheni hiyo maalum.
Baada ya kuweka mazingira sawa, OFM na polisi wa kike na kiume walivamia na kufanikiwa kufuma laivu matukio mengi ya ufuska mkubwa (ukitaka kuona zaidi, unakaribishwa Sinza-Mori ofisini kwetu).

WAUME ZA WATU!
Baada ya zoezi hilo kukamilika, baadhi ya mashuhuda (hasa akina mama) walisikika wakishukuru kufumuliwa kwa saluni hiyo kwa kuwa ndoa zao zilikuwa zimeanza kuota magugu kwani wateja wengi wa saluni hiyo ni waume za watu na vigogo serikalini!
“Jamani tunashukuru sana, waume zetu walikuwa wanakimbilia hapo, ugomvi kidogo tu, mwanaume anakwenda hapo na akirudi nyumbani hana habari kabisa na mkewe, safi sana OFM na polisi kwa jumla,” alisikika mama Inno akishangilia kufumuliwa kwa saluni hiyo.

SOO POLISI
Baada ya ‘sheshe’ hilo, mrembo huyo alichukuliwa na polisi kwa upelelezi maalum ambapo polisi walilieleza Ijumaa Wikienda kuwa, watahakikisha wanaikomesha tabia hiyo hasa katika eneo la Sinza.
“Tumejionea wenyewe, kumbe saluni hizi zimeoza kiasi hiki? Tutahakikisha tunalimaliza hili,” alisema mmoja wa polisi ambaye aliomba hifadhi ya jina kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi hilo.
BOSI ANASEMAJE?
Ijumaa Wikienda lilimtafuta bosi wa saluni hiyo, lakini simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.
Hata hivyo, katika majibu yake, mmoja wa wasimamizi wa saluni hiyo alisema kuwa, wao wana leseni ya kutoa huduma hiyo na kilichotokea kwa mwezao ni tabia ya mtu binafsi na siyo utaratibu wa ofisi yao hiyo.

KAMANDA WA POLISI
Gazeti hili lilifanya jitihada za hali ya juu za kumpata Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Murilo Jumanne ili azungumzie juu ya sakata hilo, lakini hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

KUTOKA IJUMAA WIKIENDA
Timu nzima ya OFM na Dawati la Ijumaa Wikienda kwa jumla, tunalaani vikali kuwepo kwa vitendo viovu kama hivi vinavyokwenda kinyume na maadili na utamaduni wetu kwa sababu vinachochea mmomonyoko wa maadili na ongezeko la maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

source:GPL

Comments

Popular posts from this blog