Dk Slaa, JPM wakutana kwa mara ya kwanza Ikulu
Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi mteule, Dk Willibrod Slaa, Ikulu Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 29, mwaka 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema Dk Slaa amemshukuru Rais kwa kumteua kuwa Balozi na kuahidi kuwa yupo tayari kutekeleza majukumu atakayopangiwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa. Imeeleza kuwa Dk Slaa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa uongozi bora na kutekeleza mambo makubwa ikiwemo miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa daraja la juu katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, mradi wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto rufiji na mapambano dhidi ya rushwa. “Kwa kweli naona faraja, ninafurahi Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza hatua kwa hatua karibu yote tuliyokuwa tunayapigania kwa miaka takribani 20 ya huko nyuma, mimi Dk Slaa nilikuwa napiga kelele kwa sababu nilikuwa naon