Wema Aingia Matatani Kisa Mashoga
Mrembo wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu. Mrembo wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amejikuta akiingia matatani kwa kudaiwa ‘kuwafuga’ wanaume wanaodaiwa ‘si riziki’ (mashoga) nyumbani kwake, Salasala. Kwa mujibu wa chanzo makini, mrembo huyo amekuwa akiishi na wanaume hao tata kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likiwakera majirani wanaomzunguka na kuwafanya wamshitaki serikalini. “Unajua hii tabia yake si ya leo, ameanza muda mrefu na amekuwa akiwakera majirani zake kwani wanahofia kuharibiwa watoto wao wa kiume kwa kufuata matendo yao,” kilidai chanzo. Kikizidi kushusha madai hayo chanzo hicho kilienda mbali zaidi kwa kusema mrembo huyo ni sikio la kufa kwani alikuwa akiishi na mashoga hao tangu alipokuwa anaishi maeneo ya Ununio jijini Dar hadi kumsababishia matatizo pia. “Kule Ununio alikuwa nao hawa mashoga, sijui ni marafiki zake au ni watu wa aina gani kwake. Watu wengi wanajiuliza kwanini anawakumbatia, wanakosa majibu. “Kama mnakumbuka vizuri hat