Posts

Polisi: Tutamkamata na Kumhoji Askofu Kakobe kwa Uchochezi

Image
Licha  ya kutokiri moja kwa moja juu ya taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu kumkamata Askofu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGFC) lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam, Jeshi la Polisi limesema ni lazima litamhoji kiongozi huyo wa kiroho. Kuhojiwa huko kumetokana na kauli yake dhidi ya serikali aliyoitoa wakati wa ibada ya Krismasi. Jana, kulienea taarifa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kueleza kwamba askofu huyo alitiwa mbaroni jana asubuhi na askari wa Jeshi la Polisi huku sababu za kukamatwa zikielezwa kuwa ni ujumbe alioutoa wakati wa mahubiri yake ya ibada ya Krismasi. Akizungumza na Nipashe jana kuhusiana na ukweli wa taarifa za kutiwa mbaroni kwa Askofu Kakobe, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema kuwa ni kweli walishakuwa katika harakati za kumkamata. “Ametoa maneno ya kashfa katika mahubiri yake, lakini sina taarifa kama amekamatwa,”  Kamanda Mambosasa alisema na kuongeza: “Taarifa

BABA MZAZI ,ALIYENASWA GESTI NA, MWANAYE WA KUMZAA KIMENUKA!

Image
Fadhil Mshamu, mkazi wa Kibaha mkoani hapa anakula Krismasi na Mwaka Mpya wa 2018, akiwa na stresi kufuatia kusomewa shitaka la kumdhalilisha binti yake wa kumzaa jina linahidhiwa kwa sababu za kimaadili. Kesi hiyo ilitajwa wiki iliyopita ambapo itaanza rasmi kusikilizwa mapema Mwezi Januari, mwakani katika Mahakama ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani. Mshamu alikutwa na kasheshe hilo baada ya miezi kadhaa kunaswa akiwa na binti yake wa kumzaa kwenye nyumba moja ya kulala wageni (gesti) huko Kibaha huku kukiwa na madai ya kumtaka kingono. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Mshamu alinaswa akiwa na binti yake huyo baada ya kuwekewa mtego kufuatia taarifa za kumsumbua kwa muda mrefu akidaiwa kumtaka kimapenzi. Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka ndani ya familia ya Mshamu, baada ya kunaswa kwenye mtego huo uliowashirikisha polisi na ndugu wa familia hiyo, Juni 26, mwaka huu, Jeshi la Polisi lilimfungulia Mshamu jalada la uchunguzi ambalo lilipelekwa kwa Mwendesha Mas

Mkurugenzi Mtendaji CRDB Atangaza Kung’atuka

Image
MTENDAJI Mkuu wa CRDB Bank, Dr Charles Kimeo, leo ametangaza kustaaafu ifikapo Mei 2019. Dkt. Kimei aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba hatua hiyo ni kwa ajili ya kuanzisha mchakato wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo kupata mtu atakayeshika nafasi yake kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizopo. Kabla ya kujiunga na benki hiyo, Dk Kimei alifanya kazi Benki Kuu ya Tanzania kama Mkurugenzi Mfawidhi wa Shughuli za Benki, Mkurugenzi wa Sera, Uchumi na Utafiti, Meneja wa Idara ya Utafiti wa Uchumi na Sera na nyadhifa nyingine mbalimbali katika Idara ya Utafiti. Hivi sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki Mabenki nchini. Amewahi pia kufanya kazi katika bodi mbalimbali ikiwemo ya Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Mamlaka ya Elimu nchini, Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampuni ya Huduma za Mikopo Midogo ya CRDB na tawi la CRDB nchini Burundi. Dkt. Kimei ana Shahada ya Uzamivu katika Uchumi aliyoipata Chuo Kikuu cha

Ikulu Haina Taarifa ya JPM Kushinda Tuzo ya Mandela

Image
IKIWA ni siku moja baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ametunikiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) huko nchini Afrika Kusini, huku kukikosekana taarifa rasmi kutoka kwa waandaaji wa tuzo hizo. Leo Alhamisi, Desemba 28, 2017 kupitia kipindi cha Joto la Asubuhi cha Radio  E-FM, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa amesema kuwa hana taarifa yoyote juu ya tuzo hiyo. “Mimi sina taarifa zozote kwa sababu mtu anapotoa tuzo sio lazima awasiliane na mtu anayempa tuzo, wao wanakuwa na vigezo vyao kadri ya watu walivyowapima viongozi.“ amesema Msigwa. “Mimi sina information zozote kwa hiyo ni vizuri mngewatafuta hao Nelson Mandela wenyewe hicho chuo waweze kuwaeleza tuzo hizo taarifa wanakuwa nazo vyuo wenyewe,“ amesisitiza Msigwa. Hata hivyo tayari Wakfu wa Nelson Mandela nchini Afrika Kusini umebainisha kuwa haukuandaa, kusimamia wala kutoa tuzo

Mwanajeshi Apigwa Risasi na Mpenzi Wake, Afariki

Image
ASKARIwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Kikosi cha Makambako (KJ 514) ambaye amefahamika kwa jina la Neema Masanja amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mchumba wake ambaye ni askari wa Jeshi la Polisi Makambako mkoani Njombe. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Prudensiana Protas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo mapema jana na kusema kuwa Askari wa jeshi la polisi Makambako mkoani Njombe ambaye anafahamika kwa jina la Zakayo Dotto alifanya tukio hilo la mauaji kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa Zakayo Dotto ambaye baada ya kufanya tukio hilo la mauaji alikimbia kusikojulikana.

Wema: Tunajivunia Kumpata RC Mwenye Akili Nyingi

Image
QUEEN wa Bongo Movies, Wema Sepetu ambaye amerejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni akitokea CHADEMA , amefunguka ya moyoni kuhusu utendaji mzuri wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. Wema ambaye amekuwa karibu na RC Makonda tangu arejee CCM, amepost picha ya Makonda kupitia Instagram yake na kuandika ujumbe unaowataka wakazi wa Dar es Salaam kujivunia mkuu huyo kutokana na utendaji wake wa kazi. “Tanzania Kwanza. Katika vitu ambavyo Dar pia inatakiwa kujivunia ni kupata RC mwenye akili nyingi… Mungu akakutangulie katika kazi zako za lengo la kuijenga Tanzania yako izidi kuwa zaidi ya ilipo sasa,” aliandika Wema. Aliongeza, “Ipo siku wataelewa tu, The Man Himself… Call Him Mr Dar-es-salaam… Viva RC wangu…. Viva Rais wangu…. #UzalendoKwanza … cc @paulmakonda May everything you wish well for your Nation Be…. We support you fully,” Muigizaji huyo bado anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya baada ya kudaiwa kukutwa na msokoto wa bangi n

Angalia Picha Mwanamke Tajiri Zaidi Duniani kwa Sasa, Aliyechukua Mikoba ya Liliane Bettencourt

Image
Baada ya Mfaransa Liliane Bettencourt, 94, kufariki mwezi uliopita, ambaye alikuwa mmiliki wa maduka ya bidhaa za urembo L’Oreal, ambaye ndiye aliyekuwa mwanamke tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni 39.5, sawa na takriban Tshs trilioni 94, mikoba yake imepata mrithi. Mikoba hiyo imechukuliwa na Alice Walton, ambaye ana mali ya jumla ya Dola za Marekani bilioni 33.8. Kwa jumla, alishikilia nambari 17 katika orodha ya mabilionea wa Forbes waliotangazwa mapema mwaka huu. Hadi kufikia mwezi November mwaka huu Alice Walton ametajwa kuwa na utajiri wa Dola bilioni 45.9 sawa na Tsh za Tanzania trilioni 108. Watson ambaye ni binti pekee wa mwanzilishi wa maduka ya Wal-Mart Sam Walton, ndiye mwanamke tajiri zaidi Marekani na utajiri wake unatokana na hisa zake katika Wal-Mart pamoja na malipo ya mgawo wa faida.

I Miss My God! (Namkumbuka Mungu Wangu) – 01

Image
“ OH My God! It is a ruptured pregnancy!”(Mungu wangu! Kumbe mfuko wa uzazi umepasuka!) aliongea kwa sauti Dk. Namshitu Fundikira, bingwa wa upasuaji wa matatizo ya wanawake . “Kweli?” Daktari mwingine aliyekuwa karibu aliuliza. “Kabisa, tunachohitaji kufanya hivi sasa ni kumkimbiza haraka sana chumba cha upasuaji ili tujaribu kuokoa maisha ya mama na mtoto, tukizidi kuchelewa tutapoteza wote wawili au mmoja wao.” Yalikuwa ni maongezi ya kundi la madaktari ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Good Samaritan iliyopo eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam, mwanamke alikuwa amelala kitandani, ujauzito wake ukionekana bayana, mtu mwenye akili timamu hakuhitaji shahada yoyote kuelewa ukali wa maumivu aliyokuwa nayo, jasho jingi lilikuwa likimtoka na kulowanisha mashuka huku akitupa miguu yake huku na kule. “Ana CPD!” Dk. Fundikira alitamka maneno hayo akimaanisha Cephalo-Pelvic- Disproportion, yaani hapakuwa na uwiano kati ya kichwa cha mtoto

Rais Mnangagwa amteua mkuu wa jeshi aliyeongoza mapinduzi ya kumng’oa Mugabe

Image
Jenerali wa Jeshi la Wananchi Zimbabwe ambaye aliongoza mapinduzi yaliyopelekea Robert Mugabe kung’olewa madarakani, ameteuliwa kuwa naibu kiongozi wa chama tawala cha ZANU-PF. Constantino Chiwenga ameteuliwa na Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa  ambapo hivi karibuni alistaafu kama mkuu wa jeshi, na kuenea kwa tetesi kuwa atapewa wadhifa wa kwenye serikali ya mpya ya Rais Mnangagwa. Uteuzi huo unaonekana kama hatua ya kuelekea kutajwa kuwa makamu wa Rais baada ya makamu wa Makamu wa sasa wa Zanu PF, Kembo Mohadi ambaye alikuwa waziri usalama chini ya Robert Mugabe kuonekana kuelemewa.

SPIKA NDUGAI AIKOSOA SERIKALI UPANGAJI WA VITUO VYA KAZI KWA WALIMU WAPYA

Image
DODOMA: Spika wa Bunge, Job Ndugai amekosoa mpango wa TAMISEMI kuwapangia walimu wapya vituo vya kazi moja kwa moja akisema kazi hiyo ni ya Halmashauri kwani ndizo zinazofahamu maeneo yenye uhaba wa walimu. Ndugai amesema hayo leo Jumamosi Desemba 23,2017 ikiwa ni siku moja baada Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo kutangaza majina ya walimu wapya 3,033 waliopangiwa vituo vya kazi. Katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Dodoma, Ndugai amehoji Tamisemi ni nani hata aweze kujua ikama ya walimu shuleni. Amesema wamekuwa wakijaza walimu maeneo yasiyo na mahitaji na kuyaach maeneo yenye uhitaji. “Jambo hili linakera, kila mahali sasa ni Tamisemi hadi napata shaka, hivi hii zana ya D by D (ugatuaji wa madaraka) ina maana haijatafsiriwa vyema au ndiyo kupoka madaraka kwa wengine?” alihoji Ndugai. Akitoa mfano wa Shule ya Banyibanyi wilayani Kongwa, Ndugai alisema ina wanafunzi wanaoingia kidato cha tatu lakini hawajawahi kusoma masomo ya sayan

Haji Manara; kitendo cha Klabu yangu kufungwa kwa penanti ni aibu ya mwaka

Image
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kusema kitendo cha klabu yake ya Simba jana kufungwa kwa njia ya penati na kuondolewa kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup ni aibu ya mwaka. Haji Manara alisema hayo jana baada ya waliokuwa mabingwa watetezi wa (Azam Sports Federation Cup) Simba kupigwa na Green Warriors na kuondolewa katika michuano hiyo kwa penati 4-3 "Shame!! Aibu!!!Fedheha!!! Haivumiliki!!!Tumewakera fans wetu zaidi ya twenty millions... nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba..Aibu ya mwaka" aliandika Haji Manara

Mwalimu atiwa mbaroni kwa kubaka wanafunzi wake

Image
Mwalimu mbaroni akidaiwa kubaka wanafunzi wake tisa MWALIMU wa Shule ya Msingi Itiryo, Samweli Bisendo (29),  amekamatwa na jeshi la polisi akituhumiwa kubaka wanafunzi tisa wa shule yake iliyopo wilayani Tarime. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe, alisema kuwa mwalimu huyo anadaiwa kutenda unyama huo kwa nyakati tofauti hadi alipobainika. "Jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mwalimu wa shule ya msingi Itiryo, Samweli Mariba Bisendo (29) kwa tuhuma ya kubaka watoto wapatao tisa ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi Itiryo,” alisema Kamanda Mwaibambe na kuongeza kuwa matukio hayo yalifanyika kati ya Novemba 30 na Desemba 6,mwaka huu. “Alikamatwa wakati akiwa anajiandaa kutorokea nchi jirani ya Kenya," alisema Mwaibambe. Aidha, Mwaibambe alipongeza ushirikiano kutoka kwa wananchi ambao ndiyo waliowezesha jitihada za polisi kuzaa matunda  katika  kumkamata mwalimu huyo.

Nabii Amnunulia Binti Yake wa Miaka 4 Gari la Mil. 926

Image
Mtoto Israella Bushiri. NABII wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering, Shepherd Bushiri, amemfanyia sapraizi mwanayae wa kike, Israella Bushiri mwenye umri wa miaka 4, baada ya kumnunulia gari aina ya Maserati Levante lenye thamani ya Sh milioni 926, kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa. Gari alilonunuliwa na baba yake. Bushiri alitumia ukurasa wake wa Facebook ku-share picha na kuandika maneno ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya pekee aliyomjalia kumpata binti yake huyo. Gari lenyewe. Nabii huyo ambaye mara nyingi anafanya kazi zake za uinjilishaji nchini Afrika Kusini aliandika: “Ninaona baraka zako Mungu kwa zawadi hii ya pekee uliyonipa katika maisha yangu. Ninasherehekea kuzaliwa kwa Mungu wangu na mwokozi wangu Yesu Kristo, na kuzaliwa kwa binti yangu wa kwanza, Israella Bushiri. “Ninaona ni kama jana tu wakati mtoto huyu alipozaliwa na kumbeba mikononi mwangu, lakini leo naweza kumweka mabegani mwangu na akatulia mwenyewe pasipo kushikiliwa, nit

Hamisa Mobetto: “Ungejiamini Wako angetulia”

Image
Kutokana na kile ambacho kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii kati ya Zari the bosslady  na Hamisa Mobetto ambao wanadaiwa kuwa wanarushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii kutokana na who wawili kuhost party usiku wa December 21,2017 Kampala Uganda na kusemekana kuwa Zari alijaza watu wengi kuliko Hamisa Mobetto. Hamisa Mobetto aonyesha kuendelea kurusha vijembe kwa Zari kupitia mtandao wake wa snapchat ambapo Hamisa ameandika “Tembo gani anang’olewa pembe kila siku” na Zari kumjibu “vikatuni kumi wanakusanya michango ya kusaidia watoto, vinyago kwenye mitandao ya kijamii,walioshindwa na maisha wakajikusanya kumshusha mtu mmoja,lakini mkashindwa#TheGeneral”

SIMBA KAMA MANCHESTER UNITED, WAVULIWA UBINGWA WA KOMBE LA FA

Image
Kikosi cha timu ya Simba SC. Siku mbili baada ya Manchester United ya England kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Ligi dhidi ya Bristol City inayoshiriki Ligi Daraja la Pili, mabingwa wa Kombe la FA nchini Tanzania, Simba nao wamevuliwa ubingwa wa michuano hiyo kwa kufungwa na Green Warious. Simba imevuliwa ubingwa huo usiku huu wa Ijumaa kwenye Uwanja wa Azam Complex ulipo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa njia ya penati 4-3. Hatua hiyo ilifika baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida, ndipo mwamuzi Israel Nkono akaamuru zipigwe penati. Kipa wa Green, Shaban Dihile ndiye aliyekuwa shujaa kutokana na kuonekana kuwa imara langoni huku wachezaji wa Simba, Mzamiru Yassin, Mohamed Hussein ‘Zimbwe JR na Jonas Mkude wakikosa penati na kuchangia timu hiyo ya Ligi Daraja la Pili kusonga mbele dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom. Waliopata penati za Simba ni Erasto Nyoni, Shiza Kichuya na John Bocco.

BREAKING NEWS : ASKARI MWINGINE WA JWT ALIYESHAMBULIWA DRC AFARIKI DUNIA

Image
ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) aliyekuwa katika Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amefariki dunia nchini Uganda wakati akipatiwa matibabu. Askari huyo ni miongoni mwa askari 44 wa Tanzania waliojeruhiwa katika shambulio lililofanywa Desemba 7 mwaka huu na waasi wa The Allied Democratic Forces (ADF) katika kambi ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa (MONUSCO), na kusababisha vifo vya wanajeshi 14 wa Tanzania na watano wa DRC. Msemaji wa Katibu wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, alitangaza taarifa hiyo ya kusikitisha katika Makao Makuu wa UN, Mjini New York jana Desemba 22, 2017 usiku. Katika taarifa iliyotolewa na MONUSCO leo, imeeleza kwamba mwanajeshi wa 15 wa Tanzania amefariki dunia akipatiwa matibabu mjini Kampala. Umoja wa Mataifa umetuma salamu za pole kwa wanajeshi, familia, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na serikali ya Tanzania kutokana na msiba

Mbaroni kwa Kukutwa na Magamba ya Kakakuona na Nyama ya Simba

Image
JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Ngerezya Chamukaga mkazi wa Kijiji cha Kanyara wilaya ya Sengerema kwa kukutwa na nyara mbalimbali za serikali, yakiwemo magamba 40 ya Kakakuona na vipande vitatu vya nyama ya Simba. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi Ahmed Msangi amesema Chamukaga alikamatwa Desemba 21 mwaka huu majira ya saa 1 usiku akiwa na nyara hizo za serikali. Katika tukio jinine, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mukadam Mukadamu ameongoza oparesheni ya ukaguzi wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi za jirani katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Nyegezi, ambapo mabasi matatu yanayosafirisha abiria kuelekea jijini Dar es Salaam yamezuiliwa baada ya kubaini kuwa hayajakidhi vigezo. Baadhi ya madereva wa mabasi yaliyofanyiwa ukaguzi wa leseni na kuwapima kilevi, wameupongeza utaratibu huo na kuomba uwe endelevu, huku abiria pamoja na wadau wengine wa usafiri wakisema ukaguzi h

MWENYEKITI UVCCM APOKELEWA KWA KISHINDO DAR

Image
Mwenyekiti mpya Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),Kheri James akizungumza nawaandishi wa habari ukumbi wa Vijana Kinondoni, Dar es Salaam Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Kilakala (kushoto) akiteta jambo na Kheri James. Baadhi ya vijana wa UVCCM waliohudhuria katika hafla hiyo. MWENYEKITI mpya Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amepokelewa kwa kishindo na vijana wa UVCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati akitokea mkoani Dodoma. Hafla hiyo imefanyika jana katika ukumbi wa Vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam. Kheri alichaguliwa rasmi kuwa mwenyekiti Desemba 13 mwaka huu katika uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma na kuibuka mshindi kwa kupata kura 319. Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo, Kheri alisema ni wakati wa vijana wa jumuiya hiyo kuwa ngangari katika kupambana na rushwa inayoharibu taswira ya nchi kwani rushwa haijengi bali itawafanya vijana kuwa wasindikizaji tu kati

Zitto Akutana na Kufanya Mazungumzo na Mbowe

Image
Zitto na Mbowe. Katika kikao chake cha juzi, ambacho kiliamua kugomea ushiriki wa uchaguzi wa marudio, Kamati Kuu ya ACT Wazalendo iliuagiza Uongozi wa Taifa wa Chama kuwafikia wadau wote wa Demokrasia nchini na kuweka mikakati ya pamoja ya hatua za ziada za kuchukua ili kuboresha mazingira ya chaguzi za haki nchini kwetu, kwa kuanzisha mazungumzo na vyama vyote vya Upinzani nchini ili kuona njia bora zaidi ya mapambano ya pamoja ya kukabiliana na vitendo vya chama tawala cha kuvuruga chaguzi huru na za haki nchini. Wakati Katibu Mkuu wa chama chetu, ndugu Dorothy Semu, anaendelea na utaratibu rasmi wa kulitekeleza hilo, nilipewa wajibu wa kuanzisha mazungumzo ya Viongozi wa Juu wa vyama hivyo. Jana, nimezungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi, ndugu James Mbatia aliye hospitalini KCMC baada ya ajali (namuomba Mola ampe afya njema), pamoja na kukutana na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, ndugu Freeman Mbowe. Nafurahi kwamba mazungumzo yetu yameanza vizuri.

Fanya Haya, Hisia Za Mapenzi Ziendelee!

Image
TUNAISHI kwenye ulimwengu unaoenda kasi sana kiasi kwamba usipokuwa makini, unaweza kujikuta ukimpoteza mtu uliyempenda sana maishani kwa sababu tu ya kujua namna ya kwenda naye sawa wakati ukiendelea na mchakamchaka wa kukimbizana na maisha! Inafahamika kwamba mapenzi ni hisia lakini ni wachache wanaoweza kueleza jinsi ya kufanya hisia za mapenzi ziendelee kuwa hai. Siku hizi ndoa nyingi zinaendelea kuwepo kwa sababu ya kudra tu, unakuta mume na mke wanaishi kwa sababu ya mazoea tu lakini si kwa sababu ya mapenzi! Wengine wanakwambia kabisa, ‘mapenzi yalikuwa wakati tunaanzana’! Wanaishi tu ilimradi siku zinaenda, ilimradi wanawalea watoto lakini si kwa sababu ya upendo kati yao. Wengine wanafikia hatua hata ya kulala mzungu wa nne au kutengana vyumba kabisa! Kwa nje mnawaona kama wanapendana lakini kumbe ndani kuna ufa mkubwa kati yao, hakuna tena mapenzi kati yao. Cha ajabu, utakuta watu hawahawa ambao leo wanaishi kimazoea, wakati wanaanzana walikuwa w