Posts
Mbunge:Bobi Wine Amekataa Fedha Milioni 29 Alizohongwa
- Get link
- X
- Other Apps
Mwanamuziki Uganda, ambaye ni Mbunge Kyadondo East , Bobi Wine amekataa fedha milioni 29 za Uganda alizohongwa na serikali ili aweze kukubaliana na mapendekezo ya kufanyia marekebisho kipengele cha katiba na kuondoa ukomo wa miaka 75 kuongoza nchi. Bobi Wine ameiamuru benki ambayo amewekewa fedha hizo kuzirudisha kwa watu ambao wameziweka na kusema kutokana na taarifa ya mawasiliano wabunge wote wa Uganda 449 wamepewa fedha hizo ili waweze kukubaliana na hoja hiyo na kuoandoa ukomo wa miaka 75 ili kuweza kumpa nafasi tena Yoweri Kaguta Museveni (73) kugombea nafasi ya Urais tena kwa awamu ya sita 2021. “Oktoba 24, 2017 Milioni 29 wa Uganda ziliwekwa kwenye Account yangu ya benki, pesa hizo walipewa wabunge wote wa Uganda kwa mujibu wa taarifa rasmi pesa hizo walizopewa wabunge ni ili kukubaliana na pendekezo la kufanyia marekebisho kipengele cha 102 (b) cha Katiba ya Uganda na kuondoa ukomo wa miaka 75 kama sifa ya kusimama kama Rais wa Uganda” alisema Bobi W
ZARI THE BOSS LADY NA HAMISA MOBETTO MAPYA TENA,WAONYWA VIKALI,WAWEKWA KITI MOTO
- Get link
- X
- Other Apps
Warembo waliokuwa kwenye vita ya maneno, Hamisa Mobeto na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wamedaiwa kuwekwa kitimoto ili waache kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii. Risasi Jumamosi limeelezwa kuwa, kwa nyakati tofauti wawili hao waliwekwa kitimoto na ndugu wa msanii wa Mzazi Mwenzao na kutakiwa waache malumbano hayo mitandaoni kwani hayaleti picha nzuri kwao na ukizingatia kosa limeshafanyika na msanii kukiri hadharani. “Walichoelezwa tu ni kwamba, waache kutupiana vijembe mitandaoni maana wao sasa hata kama hawatakuwa wake wenza lakini tayari msanii ana damu yake kwa Mobeto. Amekiri kwamba aliteleza na kujikuta ameingia kwenye uhusiano naye hadi kufikia hatua ya kupata mtoto. Zarinah Hassan. “Mtoto ameshazaliwa na ni damu ya msanii na mwisho wa siku msanii atalazimika kumpa mahitaji yake kama mwanaye hata kama yeye hataendeleza uhusiano na mama wa mtoto. Zari ni mama wa watoto wake wawili, wamedumu muda mrefu hivyo yeye ataendelea tu kushikilia usuk
Mambo 10 Utayaona Leo Uwanja wa Uhuru…Simba vs Yanga
- Get link
- X
- Other Apps
Kikosi cha timu ya Simba. . YANGA na Simba zinakutana leo Jumamosi kila moja ikiwa imepania kushinda mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Pamoja na yote, watani wanapokutana kunakuwa na burudani nyingi sana ambazo zinatofautisha aliye uwanjani na atakayeangalia katika runinga. Kwenye Uwanja wa Uhuru, idadi ya mashabiki wanaotakiwa kuingia ni 23,000 tofauti na 60,000 kwenye Uwanja wa Taifa. Pia kumbuka mechi hii ya watani inarejea kwenye uwanja huo baada ya kipindi kirefu. Kutakuwa na mengi ambayo yatajitokeza ndani na nje ya uwanja, lakini nakupa 10 tu ambayo kwa asilimia 90 utayaona. Kikosi cha timu ya Yanga Wasio na tiketi: Watu watajitokeza wengi zaidi kuliko idadi ya wale walio na tiketi na watajazana nje ya uwanja na kusababisha kero kubwa nje ya uwanja. Bado kuna tabia ya watu kuamini kuwa wanapokwenda uwanjani kuna nafasi ya kuingia angalau kwa njia za mkato. Hivyo hawatakubali kuondoka mapema badala yake watae
SHAHIDI AELEZA WALIVYOAHIDIWA MAMILIONI KWAJILI YA KUMUUA BILIONEA MSUYA
- Get link
- X
- Other Apps
Mahakama Kuu Kanda ya Moshi imeelezwa kuwa washtakiwa katika kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya waliahidiwa kulipwa Sh17 milioni kila mmoja. Hayo yamo katika maelezo ya mshtakiwa wa saba, Ally Mussa Majeshi yaliyosomwa mahakamani na shahidi wa 10 wa upande wa mashtaka, Sajini Atway Omary baada ya kupokelewa kama kielelezo.Maelezo hayo yalisomwa baada ya Jaji Salma Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo, kutoa uamuzi mdogo wa kukataa pingamizi la upande wa utetezi kupinga maelezo hayo yasipokelewe kama kielelezo.Jopo la utetezi linaloundwa na mawakili Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emmanuel Safari na John Lundu walikuwa wakipinga wakisema mshtakiwa aliyatoa baada ya kuteswa na polisi. Baada ya kutupilia mbali pingamizi hilo na kuungana na hoja za mawakili wa Serikali, shahidi huyo wa 10 akatakiwa kuyasoma maelezo hayo neno kwa neno. Akisoma maelezo hayo, shahidi huyo ambaye ndiye aliyeyaandika katika Kituo cha Polisi Kigoma Oktoba 5, 2013, alisema mshtakiwa alimw
Jaji Warioba ashauri Viongozi wakutane na Wazungumze
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri Mkuu wa zamani, Joseph Warioba amewataka viongozi wa kisiasa kujenga utamaduni wa kukutana wanapogundua kuna matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani. Jaji Warioba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba amesema waasisi wa Taifa walijenga umoja na misingi ya maendeleo ambayo kuna dalili ya kutoweka. Amesema hayo leo Alhamisi Oktoba 26,2017 jijini Dar es Salaam akifungua mdahalo wa mashauriano juu ya kuhamasisha, kusisitiza, kulinda na kudumisha amani, umoja na maridhiano nchini. Amesema viongozi wa dini wamekuwa na kawaida ya kukutana wanapoona mambo hayaendi sawa jambo ambalo ni zuri na linapaswa kuendelea. Jaji Warioba amesema kuna viashiria vya kutoweka kwa amani na viongozi wa kiserikali na kisiasa wanapaswa kuiga kile wanachofanya wenzao wa dini. "Amani ikitoweka kuirudisha ni shida au kuiendeleza. Viongozi hasa hawa wa kisiasa wawe wepesi kukutana na kuzungumza, tuache malumbano na hasa viongozi wa kisiasa
MASKINI LULU,MANGE KIMAMBI AMSHAMBULIA MTANDAONI KUHUSU KESI YAKE
- Get link
- X
- Other Apps
Mnajua watanzania mna double standards sana! Juzi juzi a lot of you mlikuwa mnamsapoti Magu kuwafukuza shule watoto wanaopata mimba wakiwa shule, kina Mange tukawa tunawatetea kuwa wale ni Watoto hawaju wafanyalo nyinyi mkawa mnasema kama wameweza kuvua chupi sio watoto acha wafukuzwe ila leo kwa Lulu mnasema alikuwaga mtoto Kanumba alikuwaga anambaka. Mnaona jinsi mnachekesha? Watoto wa maskini kufukuzwa shule sababu ya mimba sio Watoto ila mtu maarufu kuuwa bila kukusudia mnasema ni mtoto, so stupid. . Anyways, let me be truthful why nimeshindwa kuwa na huruma na Lulu au upande wa Lulu. Sababu ni jinsi tu alivyoishi her life the last 5 years. Hakuonyesha hata chembe ya regret for what happened.Mostly hakuwa na huruma na familia ya marehemu. Lulu alitakiwa afikirie kuwa yeye ndio sababu Kanumba hayupo duniani leo, angeonyesha ubinadamu na utu kwa kumsaidia mama wa marehemu ambae alikuwa anamtegemea mwanae kwa kila kitu. Angalau angeonyesha remorse kwa kumjali yul
Mwakyembe Kuivaa Kampuni Iliyomdhurumu Mil.25 Mzee Majuto
- Get link
- X
- Other Apps
WAZIRI wa Habari, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka na kusema kuwa Mzee Majuto amedhurumiwa pesa milioni 25 na kampuni ya filamu ambayo jina lake amelihifadhi na kudai atatumia hata mshahara wake kuhakikisha anawafunga watu hao. Mwakyembe amesema hayo leo Oktoba 27, 2017 alipokutana na wasanii mbalimbali kujadili changamoto za kazi ya sanaa nchini na kusema katika vitu ambavyo atapambana navyo ni pamoja na watu wanaowadhurumu wasanii haki yao na kuwaibia kazi zao za sanaa. “Nilipopita Tanga nilikutana msanii nguli wa filamu Mzee Majuto nilikwenda kumjulia hali na bahati nzuri saizi anaendelea vizuri, Mzee Majuto akaniomba kitu kimoja na kuniambia naumwa nahitaji pesa lakini nimeshafanya kazi na kampuni hii akanionyesha na kuwa ameshatengeneza filamu zaidi ya 100 na kampuni hiyo kwa mkataba wa kulipwa fedha ndogo tu shilingi milioni 25. “Lakini huu ni mwaka wa pili hajalipwa hata senti tano sasa hayo ndiyo mambo ambayo sifurahii, nimeshapeleka taarifa kwa
WANAWAKE MIL 14 HUUGUA SARATANI YA MATITI KILA MWAKA DUNIANI
- Get link
- X
- Other Apps
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt Julius Mwaiselage Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt Julius Mwaiselage amesema kuwa tatizo la saratani limekuwa likiongezeka siku hadi siku duniani kote na takwimu zinazotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni [WHO] zinaonyesha kwamba kila mwaka wagonjwa wapya milioni 14.1 hugundulika na wagonjwa milioni 8.8 hufariki dunia. Ugonjwa wa Saratani ya Matiti Unavyoonekana Ameyasema wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akizungumzia matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi mapema wa saratani ya matiti inayotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu. Ameongeza kuwa taasisi yao kwa kushirikiana na Hoteli ya Kunduchi Beach na Hospitali ya Aga Khan ndiyo imeandaa matembezi yatakayoanzia Ocean Road saa 12.30 asubuhi na kuhitimishwa saa 4.00 katika taasisi hiyo ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.
JPM Abadili Maamuzi kwa Wakuu wa Mikoa Wawili Baada tu ya Kuwaapisha
- Get link
- X
- Other Apps
RAIS John Magufuli amewataka Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliyeapishwa leo, Bi. Christine Mndeme ahame kituo na kwenda kufanya kazi kama Mkoa wa Ruvuma huku akimtaka Mkuu wa Mkoa Ruvuma, Mahenge ahamie Mkoa wa Dodoma. Rais ametoa agizo hilo mara baada ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu wa Wizara na Manaibu katibu wakuu aliowateua jana baada ya kufanya mabadiliko machache katika safu yake ya uongozi. “Mkuu wa Mkoa wa Dodoma mpya, Christine Mdemi atakuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma badala na Dkt. Binilith Mahenge atakwenda Dodoma,” alisema Magufuli. Aidha Rais amewataka Wakuu wa Mikoa wapya, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu wapya wakashirikiane na viongozi wengine kwenye maeneo yao kutatua shida za wananchi na kutengeneza mikakati ya kukuza uchumi katikamaeneo yao ya kazi. “Kila mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya akaangalie matatizo yaliyopo na kitu gani anaweza kufanya kuongeza uchumi wa eneo lake,” alisisitiza Rai Magufuli. Pia ametoa onyokwa watendaji watakao
Mganga Mkuu Afunguka Kuhusu Vifo vya Watoto Wachanga 9
- Get link
- X
- Other Apps
Mganga Mkuu Mkoa wa Arusha Dkt. Wonanji Timoth amekanusha taarifa za kufariki kwa watoto 9 waliokuwa kwenye Incubator kutokana na katizo la umeme hapo jana hospitali ya Mt. Meru, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote. Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Dkt. Timoth amesema kwamba watoto waliofariki walikuwa wanne na sio 9 kama inavyoelezwa kwenye taarifa iliyosambaa mitandaoni, na wamefariki kwa matatizo mengine lakini sio kukatika kwa umeme. Dkt. Timoth ameendelea kwa kueleza kwamba moja ya sababu iliyofanya watoto hao kufariki ni mama kuchelewa kufika hospitali kujifungua kwa kuwa alijifungulia nyumbani, pamoja na hatari kubwa wanazopata watoto njiti.
Matukio yaliyojiri ikiwa ni pamoja na babu abebwa mgongoni kwenda kupiga kura kenya
- Get link
- X
- Other Apps
Leo tarehe 26 Oktoba, 2017 Taifa la Kenya limefanya uchaguzi wa Rais, ambapo kiongozi wa vyama vya upinzani nchini humo, Raila Odinga amesusia uchaguzi huo. Rais Uhuru Kenyatta akipiga kura mapema leo jijini Nairobi katika Shule ya Msingi Mutomo Hadi sasa taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari nchini humo zinaeleza kuwa mtu mmoja amshauawa kwenye vurugu zilizotokea mjini Kisumu na wengine 20 wakijeruhiwa kwenye vurugu zilizoongozwa na wafuasi wa vyama vya upinzani. Misururu mirefu ya wapiga kura, katika shule ya msingi ya Kayole One, Embakasi Central jijini Nairobi Wafuasi wa upinzani wakiweka magogo katikati ya barabara mjini Migori Jaji Mkuu nchini Kenya, George Maraga akipiga kura mapema leo katika shule ya msingi ya Bosose, Nyamira Rais wa zamani wa Kenya, Mwai Kibaki akipiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Munaini, Othaya. Mpiga kura akiwa na Babu yake mgongoni akimpeleka kupiga kura katika kituo cha shule ya msingi Kaare Kaunti ya Thar
RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI WA NAFASI MBALIMBALI ZA WAKUU WA MIKOA,MABALOZI NA MAKATIBU WAKUU
- Get link
- X
- Other Apps
Rais Magufuli Uteuzi wa Rais Magufuli, uliotangazwa leo Alhamisi Oktoba 26,2017 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi uliwahusu pia, makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu na wakuu wa mikoa ambao wataapishwa kesho Ijumaa Oktoba 27,2017 mchana Ikulu jijini Dar es Salaam. Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa Mkoa wa Manyara – Mkuu wa Mkoa ni Alexandar Pastor Mnyeti (Alikuwa DC wa Arumeru) Mkoa wa Rukwa – Mkuu wa Mkoa ni Joachim Leonard Wangabo (alikuwa DC wa Nanyumbu) Mkoa wa Geita – Mkuu wa Mkoa ni Bwana Robert Gabriel Lughumbi (alikuwa DC wa Korogwe) Mkoa wa Mara – Mkuu wa Mkoa ni Adam Kigoba Ally Malima (aliwahi kuwa kwenye baraza la mawaziri awamu ya nne) Mkoa wa Dodoma – Mkuu wa mkoa ni Bi. Christine Solomoni Mndeme (alikuwa DC wa Dodoma Mjini) Mkuu wa Mtwara – Gelasius Gasper Byakanwa (alikuwa DC wa Hai) Uteuzi wa Mabalozi Dr. Aziz P. Mlima – Amekuwa Balozi (alikuwa Katibu Mkuu wizara mambo ya nje) IGP Mtaafu Ernest Mangu – Amekuwa Balozi Hawa Vituo vyao vya k
Kangi Lugola: Kwa Nini Kasri la Mama Rwakatare Halijabomolewa?
- Get link
- X
- Other Apps
NAIBU Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola ameagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc) kufikisha mezani kwake maelezo ni kwa nini nyumba ‘kasri’ ya mbunge wa Viti Maalumu, Mchungaji Getrude Rwakatare (CCM) haijabomolewa. Lugola ametoa muda kwa Nemc hadi kesho Alhamisi Oktoba 26,2017 saa 10:00 jioni awe amepata taarifa ya maandishi ili aweze kutoa uamuzi iwapo ibomolewe au la. Naibu waziri ametoa agizo hilo leo Jumatano Oktoba 25,2017 wakati Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ilipokutana na watendaji wa Nemc. Lugola amefikia uamuzi huo baada ya Nemc katika taarifa yake kueleza serikali imeshindwa kuivunja nyumba hiyo kutokana na zuio lililopelekwa mahakamani na Mchungaji Rwakatare tangu mwaka 2012. Nemc imesema kesi ikiisha na uamuzi kutolewa hakutakuwa na shaka wala kigugumizi katika kuivunja nyumba hiyo. Kwa kauli hiyo, Naibu Waziri Lugola amesema hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba,
BREAKING NEWS:Mwenyekiti wa IEBC Aahirisha Uchaguzi Kenya
- Get link
- X
- Other Apps
Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati. Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati aahirisha uchaguzi kwa baadhi ya maeneo nchini Kenya mpaka siku ya Jumamosi Oktoba 28, 2017 kwa kile kilichoelezwa kuwa baadhi ya maeneo kumekuwa na changamoto mbalimbali kama vile mvua kubwa. Wafula Chebukati ametaja maeneo ambayo uchaguzi umeiarishwa kuwa ni pamoja na Kisumu Migori, Siaya na Homabay na kuwa katika maeneo hayo uchaguzi utafanyika siku ya Jumamosi, Oktoba 28. Chebukati amesema wamefikia maamuzi hayo kutokana na maeneo hayo kuwa na changamoto mbalimbali ikiwepo masuala ya usalama pamoja na mvua jambo ambalo limefanya zoezi la kupiga kura kuwa changamoto ka wapigaji kura.
Mama Aolewa Na Mwanaye Baada Ya Kumpa Ujauzito
- Get link
- X
- Other Apps
Betty Mbereko na mwanaye, Farai Mbereko. BETTY MBEREKO (40) mwanamke anayeishi Mwenezi huko Masvingo, Zimbabwe, ameolewa na mwanaye wa kumzaa aitwaye Farai Mbereko mwenye umri wa miaka 23. Katika hali hiyo ambayo ilitokea mwanzoni mwa mwezi huu wa Oktoba, mama huyo anategemea kupata mwanaye ambaye pia ni mjukuu wake. Mwanamke huyo amekuwa mjane kwa miaka 12 iliyopita ambapo amekuwa akiishi na mwanaye huyo. Alithibitisha hivi karibuni kuwa ana ujauzito wa miezi sita na hivyo akaona afadhali “aolewe” na mwanaye kwani hakutaka kuolewa na mmoja wa wadogo wa marehemu mumewe, aliosema wanamtamani. Betty aliishangaza mahakama ya kijijini kwake aliposema alianza kuzini na mwanaye miaka mitatu iliyopita. Alisema baada ya kutumia fedha nyingi kumsomesha Farai baada ya kifo cha mumewe, aliona ana haki ya kufaidi fedha ya mwanaye na si mwanamke mwingine. “Tazama, nilihangaika kumsomesha mwanangu na hakuna aliyenisaidia. Sasa mwanangu anafanya kazi na watu wanas
MVUA ZASABABISHA HUDUMA ZA USAFIRI BARABARA YA MOROGORO KUFUNGWA
- Get link
- X
- Other Apps
Mvua ya inayoendelea kunyesha kwa siku mbili mfululizo katika jiji la Dar es salaam, imesababisha mafuriko makubwa katika maeneo mbalimbali Jijini humo, ikiwemo eneo la Jangwani ambapo maji hayo yamefunga mawasiliano ya barabara ya Morogoro, Hakuna gari inayokwenda wala kurudi mjini. Mpaka sasa umeripotiwa kuokotwa katika mto kenge uliopo Tabata jijini humo, mwili wa mtu mmoja mwenye jinsia ya kiume. Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amefika katika eneo hilo nakuwataka wananchi kuondoka katika maeneo hayo kwasasa kwakuwa maji yanaendelea kuongezeka. Kituo cha mabasi ya mwendo kasi cha Fire kikiwa kimesimama kutoa huduma kwa abiria baada kujaa maji kwa bonde la Jangwani na kufunika barabara kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam leo Oktoba 26, 2017. Mbunge wa Jimbo la Ilala Iddi Azan Zungu akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufika eneo la Jangwani lilolokumbwa na mafuriko na kusababisha barabara ya Morogoro kufungwa kufuat