MVUA ZASABABISHA HUDUMA ZA USAFIRI BARABARA YA MOROGORO KUFUNGWA
Mvua ya inayoendelea kunyesha kwa siku mbili mfululizo katika jiji la
Dar es salaam, imesababisha mafuriko makubwa katika maeneo mbalimbali
Jijini humo, ikiwemo eneo la Jangwani ambapo maji hayo yamefunga
mawasiliano ya barabara ya Morogoro, Hakuna gari inayokwenda wala kurudi
mjini.
Mpaka sasa umeripotiwa kuokotwa katika mto kenge uliopo Tabata jijini humo, mwili wa mtu mmoja mwenye jinsia ya kiume.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema
amefika katika eneo hilo nakuwataka wananchi kuondoka katika maeneo hayo
kwasasa kwakuwa maji yanaendelea kuongezeka.
Kituo cha mabasi ya mwendo kasi cha Fire kikiwa kimesimama kutoa huduma kwa abiria baada kujaa maji kwa bonde la Jangwani na kufunika barabara kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam leo Oktoba 26, 2017.
Mbunge wa Jimbo la Ilala Iddi Azan Zungu akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufika eneo la Jangwani lilolokumbwa na mafuriko na kusababisha barabara ya Morogoro kufungwa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha leo Oktoba 26, 2017 Jijini Dar es salaam.
Eneo la bonde la Jangwani likiwa limefurika na kuziba barabara ya Morogoro kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam.
Barabara ya Morogoro ikiwa imefungwa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es salaam.
Gari za mwendokasi zikiwa zimesitisha huduma kwa sasa kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha leo Oktoba 26, 2017 Jijini Dar es salaam.
Comments
Post a Comment