UCHAGUZI KENYA: Mahakama Kuu imefuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa nchi hiyo yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta. Imeamuru uchaguzi urudiwe ndani ya siku 60.
Mahaka Kuu ya Kenya. IDARA ya Mahakama imesema majaji wa Mahakama Kuu nchini Kenya wameanza kutoa uamuzi kuhusu kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyowasilishwa na Umoja wa Vyama vya Upinzani (NASA) saa 5:00, leo ambapo ndiyo siku ya mwisho kikatiba kwa mahakama hiyo kutoa uamuzi. Matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi Kulikuwa na wagombea wanane katika uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 8 Agosti mwaka huu. Matokeo ya uchaguzi huo yalitangazwa Ijumaa tarehe 12 Septemba na mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati. Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo: Ekuru Aukot 27,311 (0.18%) Abduba Dida 38,093 (0.25%) Cyrus Jirongo 11,705 (0.08%) Japheth Kaluyu 16,482 (0.11%) Uhuru Kenyatta 8,203,290 (54.27%) Michael Wainaina 13,257 (0.09%) Joseph Nyagah 42,259 (0.28%) Raila Odinga 6,762,224 (44.74%) Waliokuwa wamejiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo ni 19,611,423 lakini waliopiga kura walikuwa 15,073,662 ambao ni sawa na asilimia 78.91. Ma