Mobeto Ampukutisha Zari
Hamisa Mobeto.
DAR ES SALAAM: Mwanamitindo Hamisa
Mobeto amedaiwa kuwa sehemu ya kupungua mwili kwa mwanadada mjasiriamali
maarufu, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Kwa mujibu wa chanzo makini, tangu Mobeto aanze kuibua mjadala mtandaoni kuhusiana na mtoto wake kudaiwa kuwa ni wa bwana wa Zari, mjasiriamali huyo amejikuta akipungua mwili kutokana na mawazo aliyonayo.
“Zari kapungua mwili kweli jamani. Mobeto amemponza. Amemsababishia watu wamtukane sana Zari kiasi ambacho amekosa amani kabisa. Masikini mtoto wa watu kakonda kweli sasa hivi.
Zari.
Hata hivyo mwanahabari wetu aliingia kwenye ukurasa wa Instagram wa Zari na kujionea jinsi alivyopungua baada ya kuona picha zake mpya na kulinganisha na picha zake za zamani.
Licha ya yeye mwenyewe kutozungumzia suala hilo lakini mashabiki wake walisema amefanya vizuri kujipunguza unene kwani sasa ametokelezea tofauti na zamani.
Stori: Gladnes Mallya, AMANI
Comments
Post a Comment