Posts

MAJI YA MOTO YALIVYO NA FAIDA MWILINI

Image
KUNA tiba nyingi za kitabibu zilizogawanyika katika makundi mbalimbali. Kuna zile za hospitali ambazo ni lazima zinunuliwe, lakini kuna tiba ambazo kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila kutumia gharama kubwa. Moja ya tiba hizo ni kunywa maji ya moto. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, maji moto yanatibu magonjwa mengi ikiwemo figo, kutoa sumu mwilini na kuyeyusha mafuta tumboni. Pia hurahisisha mzunguko wa damu, huondoa sumu kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo. Kunywa maji ya moto kila unapotaka kwenda kufanya kazi ya nguvu au mazoezi iwe kama kinga na inashauriwa kila siku unywe glasi nane ili kutoa taka na kila kisichotakiwa kubaki mwilini, kupitia jasho. Wataalamu wa afya wanasema kuwa ni vyema pia kunywa maji ya moto yenye ndimu au limao kabla ya kifungua kinywa ili kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima. Mwinyimvua Pazi, Mtaalamu wa Chakula na Lishe kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa maji yanarahisisha uyeyushaji wa chakula...

Paparazzi Maarufu Akutwa Amejinyonga

Image
Mwili wa marehemu ukiondolewa eneo la tukio. Wakazi wa Chalinze na vitongoji vyake mkoani hapa, Jumatano iliyopita walikumbwa na simanzi baada ya paparazzi na mpiga picha wao maarufu, Mogela Msimbe kukutwa amejinyonga kwenye nyumba iliyokuwa ikiendelea kujengwa muda mfupi baada kuaga kuwa anakwenda kushuhudia tukio la wapenzi wawili waliodaiwa kunasiana wakizini ambalo nalo lilidaiwa kutokea siku hiyo. Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyekataa kutaja jina lake, alisema siku ya tukio marehemu ambaye alikuwa mpiga picha na mwandishi wa habari wa kujitegemea alionekana kuwa na mawazo mengi lakini ghafla zikasambaa taarifa kuwa kuna mwanaume na mwanamke ambao walizisaliti ndoa zao na kwenda kujivinjari gesti, walinasiana wakiwa katika tendo la usaliti. Uvumi huo ulisambaa kwa kasi eneo hilo na kusababisha umati kujazana Kituo cha Afya cha Chalinze, mkoani hapa ambapo watu hao walionasiana walidaiwa kupelekwa kwa ajili ya huduma ya ...

Mwili wa mwanaharakati wa Tembo kuagwa leo

Image
Wayne Lotter enzi za uhai wake. MWILI wa mwanaharakati wa kupinga ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo wa nchi za Afrika Wayne Lotter, aliyepigwa risasi na kuuawa jijini Dar es Salaam Jumatano iliyopita unatarajiwa kuagwa leo katika viwanja vya Baobao Villlge Masaki jijini Dar. Wayne ambaye alikuwa mwanzilishi wa PAMS Foundation, taasisi ambayo imekuwa katika mstari wa mbele kusaidia kupambana na uwindaji haramu na biashara ya pembe za ndovu nchini Tanzania aliuawa na watu wasiofahamika Agosti 16 mwaka huu wakati anatoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere akielekea nyumbani kwake Masaki. Akizungumza na wana habari kwa niaba ya wana familia, jana Krissie Clark alisema wanatarajia kuuaga mwili wa mwanaharakati huyo leo kisha kuusafirisha kwenda nyumbani kwao Afrika Kusini kwa maziko. Alisema kuuawa kwa Wayne hakutawafanya kurudisha nyuma mapambano dhidi ya ujangili na badala yake wameelekeza nguvu zao katika Afrika ili kutokomeza kabisa ujangili kama ili...

Daktari Feki Aliyenaswa Muhimbili, Adakwa Tena Hospitali ya Amana

Image
Daktari ‘feki’ Abdallah Juma akiwa chini ya ulinzi wa Askari Polisi waliofika katika hospitali hiyo mara baada ya kupata taarifa. Mkazi  wa  jiji la Dar es Salaam, Abdallah Juma aliyewahi kukamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akidaiwa kujifanya daktari amenaswa tena katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa kufanya kazi katika hospitali hiyo wakati sifa za udaktari hana. Juma amenaswa leo ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari, baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo. Kukamatwa kwa Juma  kunakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tokea Juni 19 mwaka huu alipo kamatwa katika hospitali ya Muhimbili kwa kujifanya daktari. Katika hospitali ya Muhimbili kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu  huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amana,Zainab Hoti akizungumza waa...

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete afurahia mavuno Shambani Kwake Chalinze

Image
Rais mstaafu wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameendelea na kuwekeza nguvu zake katika kilimo wakati huu ambao amestaafu majukumu yake ya Urais. Rais Kikwete kutumia ukurasa wake wa instagram amepost picha nne akiwa shambani kwake Msoga Chalinze katika shamba la mahindi wakivuna, Rais mstaafu Kikwete alikuwa akivuna na mkewe Mama Salma Kikwete.

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES AT MOSHI CO-OPERATIVE UNIVERSITY (MoCU)

Image
The Moshi Co-operative University (MoCU) has its Mission of being the best provider of quality education, training, research and advisory services to enhance co-operative development. Applications are invited from qualified and highly motivated Tanzanians to fill the following vacancies for Academic and Administrative posts at the Moshi Co-operative University (MoCU) as follows: 1.0 ASSISTANT LECTURER (7 POSTS) (i) Law – (1 Post) (ii) Procurement – (1 Post) (iii) Banking – (1 Post) (iv) Communication Skills – (1 Post) (v) Cooperative Management and Accounting – (2 Posts) (vi) Statistics – (1 Post) 1.1 DUTIES AND RESPONSIBILITIES (i) To undergo an induction course in pedagogic skills for those who had none before; (ii) To carry out lectures, conduct tutorials, seminars and practicals, for undergraduate programmes; (iii) Preparing and present case studies; (iv) Conduct and publish /disseminate research results; (v) To recognize students having difficulties...

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA MAENDELEO LA JAPAN (JICA) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo  na Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida leo agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo  na  Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka aliyekutana na kufanya mazungumzo naye leo agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga na Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale kwa Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka aliyekutana naye leo agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.

Hofu maiti 15 zikikutwa kwenye viroba

Image
WAVUVI na wafanyabiashara katika masoko na minada ya samaki ya Kunduchi, Ununio na Feri jijini Dar es Salaam wanaishi kwa hofu baada ya kuwapo kwa taarifa za kuopolewa miili 15 ya watu baharini ikiwa imewekwa katika mifuko maalumu kama viroba, Bara na Zanzibar. Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kilichozungumza na Nipashe, miili hiyo iliokotwa kwa nyakati tofauti na wavuvi ambao waliwajulisha polisi, waliofika kuichukua. Kuwapo kwa idadi kubwa ya miili inayoopolewa kutoka baharini au kukutwa fukweni ikiwa imefungwa kama mzigo kumefanya wavuvi na wafanyabiashara wa samaki kuingiwa na hofu ya kuja kutakiwa kuisadia polisi katika uchunguzi wa mauaji hayo, pindi wanapogundua na kutoa taarifa za maiti hizo. Hofu hiyo imesababisha baadhi ya wavuvi kunyamaza wanapoona miili zaidi ikielea baharini. “Polisi tunawajulisha, wanakuja, wanabeba maiti, lakini hakuna siku wametueleza ni za kina nani," alisema mvuvi mmoja wa Kunduchi aliyezungumza na Nipashe kwa shart...

SERIKALI YAAMUA KUZIPIGA MNADA MALI ZA LUGUMI

Image
Moja ya nyumba ya Lugumi. Kampuni ya Lugumi Enterprises   Ltd  iliyotajwa katika sakata la zabuni ya Sh34 bilioni ya kuweka mashine za kielektroniki za kuchukua alama za vidole ya Jeshi la Polisi, iko hatarini kupoteza mali zake kutokana na kudaiwa kodi na  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Mnada wa maghorofa hayo utafanywa na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, kwa niaba ya TRA Mkoa wa Ilala. Maghorofa hayo yapo maeneo tofauti jijini Dar es Salaam; moja Mtaa wa Mazengo, Upanga na mawili yako Mbweni JKT wilayani Kinondoni. Kuuzwa kwa maghorofa hayo kumetangazwa jana katika gazeti la Serikali la Sunday News, tangazo hilo likieleza kwamba ghorofa la Upanga linafaa kwa ofisi wakati yale ya Mbweni JKT yanafaa kwa makazi. Mkurugenzi mtendaji wa Yono, Scolastica Kevela alisema mnada huo utafanyika Septemba 9, kuanzia saa 4:30 asubuhi kwenye maeneo yalipo maghorofa hayo. Kevela alisema Lugumi Enterprises imeshindwa kulipa kodi ya TRA kwa waka...

VITA KUU YA MTOTO, MOBETO KICHEKO, ZARI KILIO

Image
HALI si shwari kati ya mwanamitindo matata wa Bongo, Hamisa Hassan Mobet o na mwanamama mjasiriamali wa Afrika Mashariki ambaye ni mzazi mwenza wa msanii wa Bongo Fleva, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ , kisa kikielezwa kuwa ni mtoto. Wakati mtoto huyo wa Mobeto aliyepewa jina la baba mzazi wa msanii huyo akitimiza siku 14 leo Jumatatu , uzao huo umesababisha Mobeto kuibuka na kicheko kwa kuungwa mkono na Wabongo huku Zari akidaiwa kuambulia kilio kutokana na kushambuliwa mitandaoni. Mtoto wa mobeto alipozaliwa. Mara tu baada ya Mobeto kujifungua mtoto huyo Agosti 8, mwaka huu, Zari alitokwa na povu ambalo siyo la nchi hii huku akipiga mkwara kuwa asihusishwe na mtoto huyo wa ‘bitch’ (malaya), kauli ambayo aliitoa kupitia ukurasa wake unaotambuliwa kwenye Mtandao wa Instagram. Kilichofuatia ni majibizano ya mashabiki wa Mobeto na wale wa Zari ambapo kila upande ulikuwa ukivutia upande wake, lakini pande zote zilichukizwa na neno ‘bitch’ ambalo ni tusi lililo...

Ester Bulaya Augua Ghafla Akiwa Rumande

Image
Bulaya akiwa amelazwa. MBUNGE wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya (Chadema) amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua ghafla akiwa rumande ambako alikuwa ameshikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda ya Tarime Rorya baada ya kumkamata akiwa hotelini kwa madai ya kutaka kufanya mkusanyiko usio halali. ..Hapa akiendelea kutibiwa. Taarifa za kulazwa kwa Bulaya zimethibitishwa na Katibu wa Mbunge Tarime Vijijini, John Heche (Chadema), Mrimi Zabron ambaye ameeleza kuwa Bulaya anasumbuliwa na kifua ambacho kimesababisha ashindwe kuzungumza lakini hata hivyo madaktari wanaendelea kumtibu. Aidha imeelezwa kuwa, Bulaya alianguka na kupoteza fahamu akiwa rumande hivyo kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

GAVANA SONKO AAMUA KUMUIGA RAIS MAGUFULI

Image
Gavana mteule wa jimbo la Nairobi nchini Kenya Mike Sonko, ameingia kitendo cha Rais Magufuli alichofanya baada ya kuingia madarakani cha kuingia mtaani na kufanya usafi, huku akiweka kampeni maalum ya usafi. Kwenye ukurasa wake wa instagram Mike Sonko ameweka picha na kuandika kuwa serikali yake itasimima suala hilo ili kuweka mji safi, ili kutunza mazingira na kujiepusha na magonjwa ya kumbukiza. “Ni muhimu kwetu kujua na kuweka mazingira safi kwani muhimu kwa maisha yetu, na serikali yangu itawezesha kila kinachohitajika ili kufanya usafi, ili kuonyesha dhamira yetu tumetoa mapipa ya kutunzia takataka 20, mikokoteni 10, koleo 10, reki 10, viatu, mipira ya mikono na vitu vingine kwa kila kata hapa Nairobi, kwa kazi za kawaida:”, aliandika Sonko. Sonko aliendelea kuandika “Tukitaka kuondokana na kipindu pindu a magonjwa mengine mabaya, tunahitaji kuweka mazingira yetu safi, nahimiza kuacha kutupa taka hovyo, tutumie hivi vifaa ipasavyo ...

SIMBA WAKUTANA KUMPA TIMU MO DEWJI

Image
Wanachama wa Klabu ya Simba wakijiandaa kwa ajili ya mkutano huo. Kwa mara nyingine tena, Wanachama wa Klabu ya Simba wamekutana kufanya Mkutano Mkuu wa Klabu leo Jumapili kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyarere International Conference Centre) jijini Dar es Salaam. Maanadalizi ya ya mkutano huo. Ukumbi huo wa kisasa kabisa nchini upo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM), utakuwa unatumiwa kwa mara ya pili na klabu hiyo baada ya kutumika Jumapili iliyopita. Wanachama wakijadiliana kabla ya mkutano huo. Mkutano huo ni mwendelezo wa maandalizi ya Klabu ya Simba kufanya mabadiliko ya kimfumo katika kuiongoza klabu hiyo. Msemaji wa Simba, Haji Manara akizungumza. Mmoja wa wanachama maarufu wa Simba, Mohamed Dewji ‘MO’ anatarajiwa kuwa mmoja wa wadau waliopanga kuwekeza baada ya mfumo wa uendeshaji kubadilishwa. Hali ilivyo ukumbini hapo.   Wanachama ni furaha kwenda mbele. PICHA NA M...

KENYA: Odinga Auawa, Mwili Wake Watupwa Sokoni

Image
Caroline Odinga enzi za uhai wake. JESHI la Polisi katika Kaunti ya Siaya linaendelea na upelelezi baada ya mwili wa mwalimu wa kike aliyetambulika kwa jina la Caroline Odinga ambaye alikuwa msimamizi msaidizi wa Tume ya Uchaguzi (IEBC) katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya wa Agosti 8 mwaka huu. Mwili wa mwalimu huyo wa Ugenya High School ulikutwa katika soko la Sega jana Jumamosi asubuhi na watu waliokuwa wakielekea katika mazishi ya Mkurugenzi wa TEHAMA wa IEBC, Chris Msando, Kijiji cha Lifunga. Soko ambapo mwili wake umekutwa. Mkuu wa Polisi katika Kaunti ya Siaya, Sarah Duncan amesema uchunguzi unaendelea na upelelezi wa awali unaonyesha kuwa marehemu alibakwa na watu wengi na sehemu zake za siri pamoja na sikio moja kukatwa vibaya. Familia yake inaeleza kuwa mara ya mwisho alitoka nyumbani siku ya Ijumaa na kwenda kudai malipo yake kwa kazi aliyofanya ya usimamizi wa Uchaguzi Mkuu uliomalizika.

DAR: Wapigadebe 150 Watiwa Mbaroni

Image
Picha na maktaba. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza kukamata watu wapatao 150 kuanzia Agosti 14 hadi 17 mwaka huu, kwa makosa ya kuwabughuzi abiria katika maeneo mbalimbali ya jiji katika vituo vya mabasi. Wakati akizungumza na wanahabari jana  jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Lucas Mkondya, alisema watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia misako na operesheni kali iliyofanywa na polisi, na kwamba watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili. “Stendi ya mabasi ya Ubungo walikamatwa 39, Posta 12, Ferry 7, Tegeta 12, Tandika 16, Mnazimmoja 6, Stesheni 5, Manzese 12, Bunju 8 na Stereo 7,” amesema. Katika hatua nyingine, Kamanda Mkondya alisema Jeshi la Polisi katika nyakati tofauti ilikamata watuhumiwa 167 kwa makossa mbalimbali ya kihalifu ikiwemo kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, unyang’anyi wa kutumia sialaha na utapeli, kucheza kamali na kuuza pombe haramu ya ...

Rais Uhuru Kenyatta Aruhusu Maandamano ya Wanaopinga Ushindi Wake

Image
Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake, William Ruto. Rais Uhuru Kenyatta huenda akaingia katika vitabu vya kumbukumbu na historia kwa marais wa Afrika kwa kuamua kuruhusu maandamano ya amani kupinga ushindi wake alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8.   Kenyatta amewataka polisi kujizuia kutumia nguvu kubwa na badala yake wawape ulinzi wakati wa maandamano hayo ya amani na yanayoruhusiwa kisheria kwa watu ambao hawafurahii matokeo ya uchaguzi uliopita. Rais Kenyatta alisema hayo jana alipokuwa akitoa ujumbe kwa wagombea walioshindwa katika uchaguzi huo uliofanyika Jumanne iliyopita.  Kenyatta alisema hayo akiwa Jengo la Harambee alikokwenda kukutana na Kamati ya Maandalizi ya Hafla ya kuapishwa kwake. Katika ujumbe huo uliomlenga zaidi Raila Odinga aliyekuwa mgombea urais kupitia muungano wa Nasa, Kenyatta aliwataka wagombea wote ambao hawakuridhishwa na matokeo ya uchaguzi wachukue hatua zilizobainishwa na Katiba ili kupata wanachotaka. ...

TAC WATANGAZA NAFASI YA KAZI KWA IT NA ACCOUNTS

Image
TAC ASSOCIATES is a well established Firm which provides a wide audit, tax and consulting services to both public and private sector entities. The firm is looking for energetic, self motivated individuals who can work in a friendly and dynamic environment. Apart from the qualifications stated below, the successful candidate will be an individual capable of working independently, and possess good communication skills in both spoken and written English and Kiswahili. Applications are invited from suitable qualified professionals for the following positions currently existing in TAC ASSOCIATES. Job Title: Financial Consultant Reporting to: Associate Partner-Financial Consultancy Duties and Responsibilities: • Assist the Associate Partner in the development of policies and procedures for the Division. • Assist the Associate Partner in the formulation of financial policy documents e.g. financial regulations, accounting manuals, and procurement procedures manuals for ...

NAFASI YA KAZI KUTOKA UONGOZI INSTITUTE

Image
Policy Analyst UONGOZl Institute seeks to inspire leaders and promote the recognition of the important role of leadership in sustainable development within Africa. . We are seeking dynamic persons with sound experience in Policy Analysis who would appreciate the opportunity to take their career to the next level. BASIC FUNCTION Undertaking policy related development work. MAJOR ACTIVITIES • Undertake high quality research and analysis in the area of leadership and governance; • Draft and co-ordinate the preparation of substantive reports on policy work carried out at UONGOZl lnstitute • Draft working papers, policy briefs, briefing notes, opinion editorial and blog articles; • Provide comments on analytical reports and policy documents • Organisation of Policy Events • Develop innovative and effective strategies and instruments to disseminate the findings and to convey the main messages from policy work to different audiences at workshops and conferences. • C...

TANROADS YATANGAZA NAFASI 9 ZA KAZI

Image
TANZANIA NATIONAL ROADS AGENCY (TANROADS) is a Semi-Autonomous Agency under the Ministry of Works, Transport and Communication established on July 1, 2000 and is responsible for the day-to-day management of the Tanzania Mainland’s trunk and regional roads network. Its primary functions include the management of maintenance and development works, operations of the network and Axle Load Control, the implementation of road safety and environmental measures, provision of advice on the strategic framework, policies and plans for the road sector. Regional Manager, TAN ROADS – MOROGORO is looking for suitable qualified Tanzanian candidates for 9 available Posts at Morogoro Weigh Bridge stations. Applications are invited from suitable qualified and competent Tanzanians to apply for the following positions: 1. Position Title: Shift In Charge (5 – Posts) Successful applicants must be ready to work on ‘Shift’ basis including weekends and Public Holidays. He/ She should be w...

SHUHUDIA LIVE MTI WA MAAJABU UNAOTOA ‘DAMU’, UPO HAPA HAPA BONGO!

Image
KAMA ada yetu, jukumu kubwa la  GLOBAL TV Online  ni kukusogezea matukio yote muhimu ambayo wewe mdau wetu una kiu ya kuyafahamu muda wowote na wakati wowote. Kwa mara nyingine tena,  Global TV  imefunga safari mpaka Mkoani Mbeya, Wilaya ya Rungwe, Kata ya Kisiba kijiji cha Lugombo ambapo kuna Himaya ya Chief Mwambuga. Eneo hilo kuna mti wa kustaajabisha. MAAJABU YA MTI KATEMBO, UPANDE UTOMVU MWEUPE, UPANDE DAMU! Mti huu ni aina ya Mvule maarufu kwa jina la Mti wa Katembo, unakadiriwa kuwa na umri wa miaka 600 au zaidi. Ukubwa wake wa duara unahitaji watu kuanzia wanane waliounganisha mikono. ukiupima una futi 39 katika kimo cha juu kidogo lakini una futi 43 chini kabisa. Inaelezwa kuwa Mnamo mwaka 1975 mti huu kwa mara ya kwanza ulidondosha tawi lake moja ambalo, hata ukifika leo panaonekana, inasemekana lilipoanguka ilikuwa kama tetemeko la ardhi kutokana na kishindo kilichotetemesha kijiji kile na vijiji jirani. GLOBAL TV ONLINE imefika eneo la tukio n...