KENYA: Odinga Auawa, Mwili Wake Watupwa Sokoni

Caroline Odinga enzi za uhai wake.
JESHI la Polisi katika Kaunti ya Siaya linaendelea na upelelezi baada ya mwili wa mwalimu wa kike aliyetambulika kwa jina la Caroline Odinga ambaye alikuwa msimamizi msaidizi wa Tume ya Uchaguzi (IEBC) katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya wa Agosti 8 mwaka huu.
Mwili wa mwalimu huyo wa Ugenya High School ulikutwa katika soko la Sega jana Jumamosi asubuhi na watu waliokuwa wakielekea katika mazishi ya Mkurugenzi wa TEHAMA wa IEBC, Chris Msando, Kijiji cha Lifunga.
Soko ambapo mwili wake umekutwa.

Mkuu wa Polisi katika Kaunti ya Siaya, Sarah Duncan amesema uchunguzi unaendelea na upelelezi wa awali unaonyesha kuwa marehemu alibakwa na watu wengi na sehemu zake za siri pamoja na sikio moja kukatwa vibaya.
Familia yake inaeleza kuwa mara ya mwisho alitoka nyumbani siku ya Ijumaa na kwenda kudai malipo yake kwa kazi aliyofanya ya usimamizi wa Uchaguzi Mkuu uliomalizika.

Comments

Popular posts from this blog