Daktari Feki Aliyenaswa Muhimbili, Adakwa Tena Hospitali ya Amana



Daktari ‘feki’ Abdallah Juma akiwa chini ya ulinzi wa Askari Polisi waliofika katika hospitali hiyo mara baada ya kupata taarifa.
Mkazi  wa  jiji la Dar es Salaam, Abdallah Juma aliyewahi kukamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akidaiwa kujifanya daktari amenaswa tena katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa kufanya kazi katika hospitali hiyo wakati sifa za udaktari hana. Juma amenaswa leo ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari, baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo.
Kukamatwa kwa Juma  kunakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tokea Juni 19 mwaka huu alipo kamatwa katika hospitali ya Muhimbili kwa kujifanya daktari. Katika hospitali ya Muhimbili kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu  huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amana,Zainab Hoti akizungumza waandishi habari juu wananchi kuacha njia ya mkato katika kupata huduma katika hospitali ya Amana.picha na Emmanuel Massaka.
Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo. Daktari wa Kitengo cha Watu wanaoishi na Virusi  vya Ukimwi (WAVIU),    Shani Mwaruka alikiri kukamatwa kwa  kwa mtuhumiwa huyo.
Amesema, Juma alinaswa baada ya uongozi kupata malalamiko kutoka kwa  watu waliokuwa wakihitaji huduma  katika hospitalini hiyo. Amesema tayari hospitali hiyo iliweka mtego imara wa maofisa wake, ambapo Juma aliingia bila hofu yeyote na kukutana na watu ambao alitaka wampe fedha ili awahudumie ndipo aliponaswa.
Baadhi ya watu waliodaiwa kuombwa fedha na  daktari huyo feki, wamesema aliahidi kuwatafutia kazi mbalimbali katika hospitali hiyo.

Daktari wa Kitengo cha Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) wa Hospitali ya Amana, Shani Mwaruka akizungumza na waandishi wa habari juu ya kumnasa Daktari ‘feki’ katika hospitali hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Nae mwananchi aliyekwenda kupata huduma hospitali ya Amana Cecilia amesema  Agosti 9 mwaka huu, kijana  huyo aliwaeleza kuwa kuna kazi  katika hospitali ya Amana na yeye kama daktari bingwa anayefanya kazi hapo anaweza kuwasaidia.
“Alituambia kuwa  fomu zinatolewa katika  hospitali ya muhimbili sh. 150,000 lakini kwakuwa wao ni madakatari atatufanyia kwa sh. 100,000 tu. Tulichanga fedha hiyo na ilifikia 800,000 tukampatia,” alieza Cecilia. Ameongeza,Juni  19 mwaka huu aliwaita katika hospitali ya Amana ili kufanyiwa usahili lakini hakutokea na simu akawa hapokei.
“Tuliamua kuuliza kwa madakatari kama wanamfahamu lakini hakuna aliyemfahamu ndipo tulipobaini kwamba tumetapeliwa na kuamua kufanya mtego kwa kushirikiana na uongozi uliofanikisha kumnasa  leo ,” alieleza.

Comments

Popular posts from this blog