
Bulaya akiwa amelazwa.
MBUNGE wa Bunda Mjini,
Ester Amos Bulaya (Chadema)
amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara usiku wa
kuamkia leo baada ya kuugua ghafla akiwa rumande ambako alikuwa
ameshikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda ya Tarime Rorya baada ya kumkamata
akiwa hotelini kwa madai ya kutaka kufanya mkusanyiko usio halali.

..Hapa akiendelea kutibiwa.
Taarifa za kulazwa kwa Bulaya zimethibitishwa na Katibu wa Mbunge Tarime Vijijini,
John Heche (Chadema), Mrimi Zabron ambaye ameeleza kuwa
Bulaya anasumbuliwa na kifua ambacho kimesababisha ashindwe kuzungumza lakini hata hivyo madaktari wanaendelea kumtibu.
Aidha imeelezwa kuwa, Bulaya alianguka na kupoteza fahamu akiwa rumande hivyo kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
Comments
Post a Comment