Posts

GAVANA SONKO AAMUA KUMUIGA RAIS MAGUFULI

Image
Gavana mteule wa jimbo la Nairobi nchini Kenya Mike Sonko, ameingia kitendo cha Rais Magufuli alichofanya baada ya kuingia madarakani cha kuingia mtaani na kufanya usafi, huku akiweka kampeni maalum ya usafi. Kwenye ukurasa wake wa instagram Mike Sonko ameweka picha na kuandika kuwa serikali yake itasimima suala hilo ili kuweka mji safi, ili kutunza mazingira na kujiepusha na magonjwa ya kumbukiza. “Ni muhimu kwetu kujua na kuweka mazingira safi kwani muhimu kwa maisha yetu, na serikali yangu itawezesha kila kinachohitajika ili kufanya usafi, ili kuonyesha dhamira yetu tumetoa mapipa ya kutunzia takataka 20, mikokoteni 10, koleo 10, reki 10, viatu, mipira ya mikono na vitu vingine kwa kila kata hapa Nairobi, kwa kazi za kawaida:”, aliandika Sonko. Sonko aliendelea kuandika “Tukitaka kuondokana na kipindu pindu a magonjwa mengine mabaya, tunahitaji kuweka mazingira yetu safi, nahimiza kuacha kutupa taka hovyo, tutumie hivi vifaa ipasavyo

SIMBA WAKUTANA KUMPA TIMU MO DEWJI

Image
Wanachama wa Klabu ya Simba wakijiandaa kwa ajili ya mkutano huo. Kwa mara nyingine tena, Wanachama wa Klabu ya Simba wamekutana kufanya Mkutano Mkuu wa Klabu leo Jumapili kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyarere International Conference Centre) jijini Dar es Salaam. Maanadalizi ya ya mkutano huo. Ukumbi huo wa kisasa kabisa nchini upo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM), utakuwa unatumiwa kwa mara ya pili na klabu hiyo baada ya kutumika Jumapili iliyopita. Wanachama wakijadiliana kabla ya mkutano huo. Mkutano huo ni mwendelezo wa maandalizi ya Klabu ya Simba kufanya mabadiliko ya kimfumo katika kuiongoza klabu hiyo. Msemaji wa Simba, Haji Manara akizungumza. Mmoja wa wanachama maarufu wa Simba, Mohamed Dewji ‘MO’ anatarajiwa kuwa mmoja wa wadau waliopanga kuwekeza baada ya mfumo wa uendeshaji kubadilishwa. Hali ilivyo ukumbini hapo.   Wanachama ni furaha kwenda mbele. PICHA NA MUSA

KENYA: Odinga Auawa, Mwili Wake Watupwa Sokoni

Image
Caroline Odinga enzi za uhai wake. JESHI la Polisi katika Kaunti ya Siaya linaendelea na upelelezi baada ya mwili wa mwalimu wa kike aliyetambulika kwa jina la Caroline Odinga ambaye alikuwa msimamizi msaidizi wa Tume ya Uchaguzi (IEBC) katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya wa Agosti 8 mwaka huu. Mwili wa mwalimu huyo wa Ugenya High School ulikutwa katika soko la Sega jana Jumamosi asubuhi na watu waliokuwa wakielekea katika mazishi ya Mkurugenzi wa TEHAMA wa IEBC, Chris Msando, Kijiji cha Lifunga. Soko ambapo mwili wake umekutwa. Mkuu wa Polisi katika Kaunti ya Siaya, Sarah Duncan amesema uchunguzi unaendelea na upelelezi wa awali unaonyesha kuwa marehemu alibakwa na watu wengi na sehemu zake za siri pamoja na sikio moja kukatwa vibaya. Familia yake inaeleza kuwa mara ya mwisho alitoka nyumbani siku ya Ijumaa na kwenda kudai malipo yake kwa kazi aliyofanya ya usimamizi wa Uchaguzi Mkuu uliomalizika.

DAR: Wapigadebe 150 Watiwa Mbaroni

Image
Picha na maktaba. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza kukamata watu wapatao 150 kuanzia Agosti 14 hadi 17 mwaka huu, kwa makosa ya kuwabughuzi abiria katika maeneo mbalimbali ya jiji katika vituo vya mabasi. Wakati akizungumza na wanahabari jana  jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Lucas Mkondya, alisema watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia misako na operesheni kali iliyofanywa na polisi, na kwamba watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili. “Stendi ya mabasi ya Ubungo walikamatwa 39, Posta 12, Ferry 7, Tegeta 12, Tandika 16, Mnazimmoja 6, Stesheni 5, Manzese 12, Bunju 8 na Stereo 7,” amesema. Katika hatua nyingine, Kamanda Mkondya alisema Jeshi la Polisi katika nyakati tofauti ilikamata watuhumiwa 167 kwa makossa mbalimbali ya kihalifu ikiwemo kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, unyang’anyi wa kutumia sialaha na utapeli, kucheza kamali na kuuza pombe haramu ya gong

Rais Uhuru Kenyatta Aruhusu Maandamano ya Wanaopinga Ushindi Wake

Image
Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake, William Ruto. Rais Uhuru Kenyatta huenda akaingia katika vitabu vya kumbukumbu na historia kwa marais wa Afrika kwa kuamua kuruhusu maandamano ya amani kupinga ushindi wake alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8.   Kenyatta amewataka polisi kujizuia kutumia nguvu kubwa na badala yake wawape ulinzi wakati wa maandamano hayo ya amani na yanayoruhusiwa kisheria kwa watu ambao hawafurahii matokeo ya uchaguzi uliopita. Rais Kenyatta alisema hayo jana alipokuwa akitoa ujumbe kwa wagombea walioshindwa katika uchaguzi huo uliofanyika Jumanne iliyopita.  Kenyatta alisema hayo akiwa Jengo la Harambee alikokwenda kukutana na Kamati ya Maandalizi ya Hafla ya kuapishwa kwake. Katika ujumbe huo uliomlenga zaidi Raila Odinga aliyekuwa mgombea urais kupitia muungano wa Nasa, Kenyatta aliwataka wagombea wote ambao hawakuridhishwa na matokeo ya uchaguzi wachukue hatua zilizobainishwa na Katiba ili kupata wanachotaka.   “Marafiki

TAC WATANGAZA NAFASI YA KAZI KWA IT NA ACCOUNTS

Image
TAC ASSOCIATES is a well established Firm which provides a wide audit, tax and consulting services to both public and private sector entities. The firm is looking for energetic, self motivated individuals who can work in a friendly and dynamic environment. Apart from the qualifications stated below, the successful candidate will be an individual capable of working independently, and possess good communication skills in both spoken and written English and Kiswahili. Applications are invited from suitable qualified professionals for the following positions currently existing in TAC ASSOCIATES. Job Title: Financial Consultant Reporting to: Associate Partner-Financial Consultancy Duties and Responsibilities: • Assist the Associate Partner in the development of policies and procedures for the Division. • Assist the Associate Partner in the formulation of financial policy documents e.g. financial regulations, accounting manuals, and procurement procedures manuals for

NAFASI YA KAZI KUTOKA UONGOZI INSTITUTE

Image
Policy Analyst UONGOZl Institute seeks to inspire leaders and promote the recognition of the important role of leadership in sustainable development within Africa. . We are seeking dynamic persons with sound experience in Policy Analysis who would appreciate the opportunity to take their career to the next level. BASIC FUNCTION Undertaking policy related development work. MAJOR ACTIVITIES • Undertake high quality research and analysis in the area of leadership and governance; • Draft and co-ordinate the preparation of substantive reports on policy work carried out at UONGOZl lnstitute • Draft working papers, policy briefs, briefing notes, opinion editorial and blog articles; • Provide comments on analytical reports and policy documents • Organisation of Policy Events • Develop innovative and effective strategies and instruments to disseminate the findings and to convey the main messages from policy work to different audiences at workshops and conferences. • C

TANROADS YATANGAZA NAFASI 9 ZA KAZI

Image
TANZANIA NATIONAL ROADS AGENCY (TANROADS) is a Semi-Autonomous Agency under the Ministry of Works, Transport and Communication established on July 1, 2000 and is responsible for the day-to-day management of the Tanzania Mainland’s trunk and regional roads network. Its primary functions include the management of maintenance and development works, operations of the network and Axle Load Control, the implementation of road safety and environmental measures, provision of advice on the strategic framework, policies and plans for the road sector. Regional Manager, TAN ROADS – MOROGORO is looking for suitable qualified Tanzanian candidates for 9 available Posts at Morogoro Weigh Bridge stations. Applications are invited from suitable qualified and competent Tanzanians to apply for the following positions: 1. Position Title: Shift In Charge (5 – Posts) Successful applicants must be ready to work on ‘Shift’ basis including weekends and Public Holidays. He/ She should be w

SHUHUDIA LIVE MTI WA MAAJABU UNAOTOA ‘DAMU’, UPO HAPA HAPA BONGO!

Image
KAMA ada yetu, jukumu kubwa la  GLOBAL TV Online  ni kukusogezea matukio yote muhimu ambayo wewe mdau wetu una kiu ya kuyafahamu muda wowote na wakati wowote. Kwa mara nyingine tena,  Global TV  imefunga safari mpaka Mkoani Mbeya, Wilaya ya Rungwe, Kata ya Kisiba kijiji cha Lugombo ambapo kuna Himaya ya Chief Mwambuga. Eneo hilo kuna mti wa kustaajabisha. MAAJABU YA MTI KATEMBO, UPANDE UTOMVU MWEUPE, UPANDE DAMU! Mti huu ni aina ya Mvule maarufu kwa jina la Mti wa Katembo, unakadiriwa kuwa na umri wa miaka 600 au zaidi. Ukubwa wake wa duara unahitaji watu kuanzia wanane waliounganisha mikono. ukiupima una futi 39 katika kimo cha juu kidogo lakini una futi 43 chini kabisa. Inaelezwa kuwa Mnamo mwaka 1975 mti huu kwa mara ya kwanza ulidondosha tawi lake moja ambalo, hata ukifika leo panaonekana, inasemekana lilipoanguka ilikuwa kama tetemeko la ardhi kutokana na kishindo kilichotetemesha kijiji kile na vijiji jirani. GLOBAL TV ONLINE imefika eneo la tukio na kuongea na viongo

Vijue Vyakula Hatari kwa Kupunguza Nguvu za Kiume

Image
Mbegu za Flax (Flax seeds):   Wanaume wanapaswa kufahamu aina ya vyakula ambavyo si rafiki kwao katika kuongeza kiwango cha homoni ya kiume iitwayo testosterone inayochochea sifa ya mwanaume yaani kuwa na nguvu za kiume. Baadhi ya vyakula visivyofaa kuliwa na mwanaume aliyetaka kuwa na nguvu za kiume ni vile vyenye asili ya homoni ya kike iitwayo estrogen. Hivyo sio kila vyakula vinafaa kwa mwanaume eti ilimradi tu vyakula hivyo vinasaidia kujenga mwili au kujaza tumbo wakati mtu akiwa na njaa. Vyakula visivyofaa kabisa kuliwa na mwanaume kutokana na vyakula hivyo kupunguza homoni ya testosterone ni hivi vifuatavyo: vyakula vinavyotengenezwa kutokana na unga wa mbegu za flax vimekuwa vikisifiwa kwa kuwa Omega-3 fats ambayo ni muhimu katika miili yetu. Hata hivyo mbegu za flax ni mbegu maarufu kwa kuwa na estrogen ambayo ni sawa kabisa na homoni ya estrogen iliyoko katika miili ya wanawake. Flax seeds zina kiwango cha phytoestrogens mara tatu zaidi ya soya. Kama bado unafikiria kul

Gigy azidi kukonda, apima ngoma

Image
Gift Stanford ‘Gigy Money’. VIDEO Queen, Gift Stanford ‘ Gigy Money ’ ambaye mwili wake umepungua sana kiasi cha kuwapa wasiwasi mashabiki wake, amesema licha ya kupungua huko, lakini ni mzima kwani amepima ‘ngoma’ na kujikuta yuko fi ti. Akizungumza na Risasi Jumamosi juzikati, Gigy aliifungukia afya yake na kusema baada ya kujipunguza kwa mazoezi, baadaye aliamua kutumia dawa maalum za kujipunguza kwa makusudi kwani kuna mwili aliokuwa akiutafuta na sasa umekaa mahala pake. Gigy alisema hata hivyo, katika kuwahakikishia mashabiki kuwa kukonda kwake hakuna tatizo, ameamua kupima ngoma na majibu yamerudi yakimuonyesha yuko sawa kabisa. “Nimeamua kupima ngoma ili kuwaondoa wasiwasi mashabiki, kwani mwili huu si wa magonjwa kama watu wanavyodhani, nimejipunguza kwa kutumia dawa maalumu na nimefanikiwa nashukuru Mungu,” alisema Gigy. Katika hali ya kushtua, Gigy pia alifungukia maisha anayotaka kwa sasa ya kutokuwa na mpenzi ‘pamanenti’ wa kupika na kupakua, bada

BREAKING NEWS: MZEE KILOMONI ASIMAMISHWA UANACHAMA, AFUTWA UONGOZI WA BARAZA

Image
Aliyekuwa mdhamini wa Simba, Hamisi Kilomani. Klabu ya Simba imetangaza kumtoa mzee Hamisi Kilomani kwenye Baraza la Wadhamini kwa kosa la kuvunja katiba ya klabu hiyo. Pia, wanatarajia kumpekelea barua ya kumfuta uanachama na ikiwa hatafuta kesi na kushindwa kujitetea watamfukuza uanachama moja kwa moja. Aidha, profesa Juma Kapuya ameteuliwa kuziba pengo la Ally Sykes ambaye kwa sasa ni marehemu katika baraza hilo, nafasi ya mzee Kilomoni imejazwa na Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Alhaj Adam Mgoyi.

IGP Sirro awaaga askari na maofisa wanaokwenda Sudani

Image
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwakabidhi bendera ya taifa askari kumi (10) waliopata uteuzi wa kwenda kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye kazi ya Ulinzi wa Amani nchini Sudani ya Kusini (UNMISS) IGP Sirro, amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi. Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa kwenye picha ya pamoja na askari waliopata uteuzi wa kwenda kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye kazi ya Ulinzi wa Amani nchini Sudani ya Kusini (UNMISS) IGP Sirro, amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA:SERIKALI KULIPA MADENI YA WATUMISHI

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali italipa madeni yote ya Watumishi ambayo yamehakikiwa na kukutwa kuwa ni halali.  Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kwenye mkutano uliyofanyika kata ya Goweko, wilayani Uyui mkoani Tabora na Rais Pombe Magufuli alisitisha malipo kwa sababu ya zoezi la kubaini watumishi hewa, sasa kazi hiyo imeshakamilika na yale yaliyobainika kuwa halali yatalipwa huku akiwataka Watumishi hao wafanye kazi ya kuwadumia wananchi kwa bidii. "Hivi sasa tunadhibiti uzalishaji wa madeni mapya ya watumishi, hakuna madeni ya matibabu, ya likizo au ya masomo. Kila mtumishi anaruhusiwa kujiendeleza, lakini ni lazima kwanza aandike barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuelezea nia yake na akikubaliwa, ndipo aanze kutuma maombi kwenye vyuo. Mtumishi akiamua kuomba chuoni moja kwa moja ndipo alete madai yale, hatapewa chochote kwa sababu ni nje ya utaratibu,"  alisema Ma

Shamba jingine la Sumaye lachukuliwa

Image
WAKATI machungu ya kupoteza shamba lake lenye ukubwa wa ekari 33 lililokuwa Mabwepande yakiwa hayajatuliwa, aliyekuwa Waziri Mkuu Katika serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye amepoteza shamba jingine mkoani Morogoro baada ya serikali kulichukua. Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imelitwaa shamba la Sumaye lenye ukubwa wa ekari 326 baada ya kupata kibali kutoka kwa Rais Magufuli kwa madai kuwa hajaliendeza licha ya kupewa notisi ya kufanya hivyo. Shamba la Sumaye la Mabwepande lilichukuliwa Novemba mwaka jana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akifikia uamuzi huo baada ya mmiliki wa shamba hilo kutoliendeleza kama notisi ya siku 90 aliyopewa ilivyokuwa ikimtaka. Oktoba 28 Rais Magufuli alibatilisha umiliki wa shamba hilo namba 3,074 lililopo Mabwepande. Shamba hilo lilikuwa na hati namba 53086 na jina la umiliki lilikuwa ni Frankline Sumaye. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Florent Kyombo jana alisema kuwa Rais Magufuli amekubali ku

Aliyekuwa mke wa Barnaba afunguka alichokuwa anakikosa

Image
 Aliyekuwa mke na mama mtoto wa mwanamuziki Barnaba Elias, Zuu Namela, ametoa kile kinachoitwa la moyoni, na huenda ndio sababu iliyomtoa kwa mzazi mwenzake na kuanzisha mahusiano mapya. Kwenye ukurasa wake wa instagram Zuu Namela ameandika ujumbe kuwa kwa miaka mitano (ambayo ilikuwa ndani ya mahusiano na Barnaba) alikuwa anakosa furaha ya kweli na amani ya moyo, lakini sasa ameipata furaha hiyo baada ya kuachana. "Ni watu wachache sana wanaojua nikitu gani nilikua nakosa katika maisha yangu! Unaweza ukapata kila kitu kwenye maisha ila ukakosa furaha,amani,heshima......kwa zaidi ya miaka mitano ichi ndo nilicho kuwa nakitafuta #AMANIyaMOYO " aliandika Zuu Namela. Hivi karibuni Zuu Namela ameonekana akimpost mwanaume mwengine kwenye ukurasa wake, huku akiandika jumbe mbali mbali za mapenzi, na kuacha mashabiki wake kuwa ndiye mbadala wa Barnaba ambaye ni baba mtoto wake.

RAIS MAGUFULI AMPONGEZA UHURU KENYATTA BAADA YAKUTANGAZWA MSHINDI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Agosti, 2017 amempongeza Rais Mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta baada ya jana kutangazwa mshindi wa nafasi ya Urais na Tume Huru Ya Uchaguzi Kenya ( IEBC). Tume Huru ya Uchaguzi Kenya ilitangaza Kenyatta kuwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 (54.27%) dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga 6,762,224 (44.74%), kufuatia matokeo hayo Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametoa pongezi kwa Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine tena.  "Nakupongeza Ndg.Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema"  alisema Rais Magufuli kupitia mtandao wake wa Twitter  Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) ilisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki na kudai kuwa umekuwa ni uchaguzi wa kipekee kwa Kenya kwani watu waliojitokeza kujiandikisha na kupiga kura ni wengi zaidi ukilinganisha na chaguzi zilizofanyika ki

BILIONEA BILL GATES AFUNGUA AKAUNTI YA ISTARAM TANZANIA NA KUANDIKA UJUME HUU

Image
  F

DC amchapa viboko Mzazi kisa gari kupigwa mawe

Image
MKUU wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amemcharaza viboko mzazi wa mmoja wa watoto walioshambulia gari lake kwa mawe na kuvunja kioo cha nyuma jana. Gari hilo lenye namba za usajili STL 669, lilishambuliwa na watoto watatu katika barabara kuu ya Kondoa-Dodoma, kwenye kijiji cha Paranga wilayani Chemba. Kufuatia kupasuliwa kwa kioo hicho, DC alisimamisha gari hilo na kuwakimbiza watoto waliolipiga mawe, hali iliyozua purupushani kwa muda. DC huyo aliwakimbiza watoto hao kwa lengo la kuwakamata na kuwaadhibu lakini hakuweza kuwakamata baada ya kumzidi mbio. Hata hivyo, wananchi walioshuhudia tukio hilo walimtajia DC majina na sehemu wanakoishi watoto hao ili awafuate majumbani kwao. Ndipo mmoja wa wazazi wa watoto waliohusika na shambulio hilo alikutwa nyumbani akiendelea na shughuli zake na alipohojiwa na DC kuhusu malezi ya mtoto wake, aliingia katika majibizano yaliyomkera DC Odunga. "Malezi? Malezi gani unataka kwangu? Mtoto ametoka shule, mimi nitajuaje an

Mbunge wa CCM Atiwa Mbaroni Akidaiwa Kugonga na Kuua Mwanafunzi

Image
Mbunge Daniel Mtuka. Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia Mbunge Manyoni(CCM), Daniel Mtuka (51) kwa tuhuma ya kumgonga kwa gari mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Sukamahela, Salome Paschal (10) na kusababisha kifo chake papo hapo. Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa, debora Magilingimba alisema tukio hilo limetokea jana katika Kijiji cha Sukamahela tarafa ya Kilimatinde Wilaya ya Manyoni. Alisema siku ya tukio mbunge huyo akitokea Dodoma mjini akiwa njiani kurundi jimboni kwake akiendekesha gari lake aina ya Toyota Prado alimgonga mwanafunzi huyo aliyekuwa  akijaribu kuvuka kutoka upande wa kulia kwenda kushoto mwa barabara. Kamanda huyo alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva Mtuka, kushindwa kuchukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara. “Mtuhumiwa mbunge Mtuka  anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano na baada ya mahojiano, atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili