Vijue Vyakula Hatari kwa Kupunguza Nguvu za Kiume

Mbegu za Flax (Flax seeds):  
Wanaume wanapaswa kufahamu aina ya vyakula ambavyo si rafiki kwao katika kuongeza kiwango cha homoni ya kiume iitwayo testosterone inayochochea sifa ya mwanaume yaani kuwa na nguvu za kiume. Baadhi ya vyakula visivyofaa kuliwa na mwanaume aliyetaka kuwa na nguvu za kiume ni vile vyenye asili ya homoni ya kike iitwayo estrogen. Hivyo sio kila vyakula vinafaa kwa mwanaume eti ilimradi tu vyakula hivyo vinasaidia kujenga mwili au kujaza tumbo wakati mtu akiwa na njaa.

Vyakula visivyofaa kabisa kuliwa na mwanaume kutokana na vyakula hivyo kupunguza homoni ya testosterone ni hivi vifuatavyo:

vyakula vinavyotengenezwa kutokana na unga wa mbegu za flax vimekuwa vikisifiwa kwa kuwa Omega-3 fats ambayo ni muhimu katika miili yetu. Hata hivyo mbegu za flax ni mbegu maarufu kwa kuwa na estrogen ambayo ni sawa kabisa na homoni ya estrogen iliyoko katika miili ya wanawake.

Flax seeds zina kiwango cha phytoestrogens mara tatu zaidi ya soya. Kama bado unafikiria kula vyakula vilivyo na mbegu za flax ili upate omega-3 achana na wazo hilo. Kama unataka kupata omega-3 kula samaki wenye mafuta mafuta (fish oils) utapata omega-3 ya kutosha.

Licorice: 
Huu ni mzizi ambao hutumika hasa kuondoa tatizo la msongo (stress) kwa watu wanaokumbwa na tatizo hilo. Pia mzizi huo hutumika kama sukari kwenye vinywaji kama chai au kahawa badala ya kutumia sukari ya kawaida.

Hata hivyo mzizi huu una estrogen ambayo hushusha kiwango cha homoni ya kiume ya testosterone kwa wanaume. Kuna utafiti ulifanywa ambapo wanaume 7 wenye afya walipewa gramu 7 za vidonge vya licorice kila mmoja kila siku.

Vidonge hivyo vilikuwa na kiasi cha gramu 0.5 za glycyrrhizic (kiambata kilichomo ndani ya licorice kinachopunguza testosterone kwa mwanaume). Baada ya siku 4 tu kiasi cha homoni ya testosterone kwa kila mwanaume aliyefanyiwa utafiti huo kilipungua kwa kiwango cha nusu ya kiasi cha homoni kwa kila mwanaume kilivyokuwa wakati wa kuanza utafiti.

Bia (Beer):
Sipendi kusema habari mbaya kwa wanywaji wa bia. Hata hivyo ni vema kusema ukweli kuhusu athari ya bia kwa wanaume. Bia imetengenezwa kwa humle (hops) ambayo kwa kiwango kikubwa inaleta hali ya homoni za kike kwa wanaume (highly estrogenic).

 Humle (Hops) ina kiasi cha 300,000 IU cha estrogen kwa kila gramu 100 za hops. Kabla ya mwaka 1487 bia ilikuwa ikitengenezwa kwa viambata (ingredients) ambazo zililenga kuifanya bia inaponywewa na mwanaume humfanya mwanaume awe na hali ya uanaume kweli kweli (more aggressive, horny, and socially dominant).


Hata hivyo baadaye Kanisa liliingilia uzalishaji wa bia na kutaka bia itengenezwe kwa viambata ambavyo vitamfanya mwanaume awe mpole au mtaratibu na sio mtu wa maguvu na ubabe ( to make men more feminine and sensitive). Hapo ndipo likazaliwa wazo la kutengeneza bia kwa kutumia humle (hops). Siku hizi bia hutengenezwa kwa viambata vitatu, hops, maji na malt.

Soya (Soy): 
Ina kiwango kikubwa cha Isoflavones ambayo ni kiuhalisia ni estrogen. Ulaji wa soya ni sawa na kula kidonge kimoja cha uzazi wa mpango (birth control pill). Kwa kuelewa zaidi madhara ya soya kwa wanaume soma hapa.

Spearmint:
Hutumiwa zaidi kama kiambata kwenye chewing gums, candies, na breath freshener au kwenye majani ya chai (herbal tea). Spearmint pia in akiwango kikubwa cha estrogen.

 Lima beans: 
Yana homoni za kike (estrogen) iitwayo inositol ambayo hupunguza kiwango cha homoni ya kiume (testosterone) kwa wanaume.

Whole grains:
 Ina gluten ambayo huongeza prolactin ambayo hupunguza kiasi cha testosterone.


 Soda: 
Unapenda kinywaji baridi yaani soda? Je unajua soda zimechangia sana tatizo la watu kuwa na unene au uzito uliopitiliza (obesity)? Tukiachana na suala la obesity hebu tuongelee kuhusu namna soda zinavyopunguza homoni za kiume (testosterone).

Chupa za plastiki ambazo hutumiwa na makampuni yanayotengeneza soda zimetengenezwa kwa phthalates ambayo hufanya plastiki ziweze kukunjwa katika umbo lolote (flexibility).

Phthalates ni estrogen! Kawaida ili kuondoa phthalates kwenye chupa za plastiki makampuni yanapaswa kuziacha chupa hizo zikae kwa mwaka mmoja bila kuweka soda ndani yake. Hata hivyo makampuni hayo mara tu baada ya kutengeneza chupa hizo huweka soda ndani yake na kuzipeleka sokoni kwa walaji.

Unajua nini kinatokea? Phthalates inaingia kwenye soda unayokunywa!!! Maana yake kama wewe ni mwanaume unaingiza homoni za kike mwilini mwako na matokeo yake unapunguza homoni za kiume!

Fast food: 
Wewe ni mwanaume unapenda kula chakula kwenye Mgahawa wa Fast Food? Ngoja nikupe maneno kwa nini usiwe na upungufu wa nguvu za kiume wakati unafakamia vyakula Fast Food. Ukienda Fast Food unaagiza vyakula vya nyama iwe ni beef au kuku au burger na unaagiza na soda then unaona mambo safi, sio? Haya hiyo nyama au kuku imetokana na wanyama waliofugwa na kulishwa junk grains na kupewa madawa kama antibiotics na homoni za kukuzia wanyama ambavyo vyote hivyo vina asili ya homoni za kike (estrogen).

Nyama hizo zinakaangwa au kupikwa kwa mafuta ya mimea kama vile soybean oil au sunflower oil ambayo yana estrogen! Baada ya hapo unashushia soda ambayo ina phthalates (homoni ya kike). Kwa ulaji huo unategemea kunako sita kwa sita uwe ‘super man’?!!

Comments

Popular posts from this blog