Posts

TEF WAFUNGULIA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAULMAKONDA.

Image
Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) wakiondoa zuio la kutokutoa habari yoyote kwenye chanzo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye vyombo vya habari  sasa kuanzia leo habari za mkuu wa Mkoa wa Mkoa zitakuwa zikitoka kwenye vyombo vya habari. katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile  na kushoto ni  Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.   Kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akizungumza na waandishi wa  habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Jukwaa la wahariri kuondoa zuio kutotoa habari zamkuu wa ,Mkoa wa Dar Es Salaam leo.  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam kwaajili

Mwanamume apatikana akisafirisha mikono ya binadamu China

Image
Maafisa wa usalama kusini magharibi mwa China walipigwa na butwaa hivi majuzi walipogundua mwanamume mmoja alikuwa akisafirisha mikono miwili ya binadamu. Kwa mujibu wa Pear Video, mzee wa miaka 50 kwa jina Zheng alisimamishwa na maafisa wa polisi katika kituo cha mabasi cha Duyun, katika mkoa wa Guizhou baada ya mikono miwili ya binadamu kugunduliwa na mtambo wa kiusalama tarehe 31 Julai. "Nilimuuliza alikuwa amebeba nini kwenye mkoba wake, na akanijibu kwamba ulikuwa ni mkono," afisa wa usalama aliambia Pear Video. Kwa mujibu wa gazeti la South China Morning Post, alizuiliwa mara moja, wakimshuku kuwa huenda alikuwa amehusika katika mauaji. Hata hivyo, Bw Zheng aliwafafanulia kwamba alikuwa akisafirisha viungo hivyo kwa kakae, ambaye alikuwa amekatwa mikono baada ya kuhusika katika ajali ya mtambo wa umeme. Bw Zheng alisema kakake aliomba asaidiwe kusafirisha mikono hiyo hadi alikokuwa akiishi, ili atakapofariki, mwili wake na viungo hivyo, vi

PICHA MATUKIO YANAYOJIRI TAMASHA LA SIMBA Y UWANJA WA TAIFA

Image
Mashabiki wa Simba waliojitokeza kwenye Tamasha la Simba Day linalofanyika Kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salam .. Klabu ya Simba yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam ina utaratibu wake wa kuenzi vitu vyake vya klabu kwa kuanzisha siku maalumu ambayo wanasimba wote hukusanyika pamoja kujadiliana mambo mbalimbali.Agosti 8 ya kila mwaka huwa ndiyo siku hiyo iliyopewa jina la ‘Simba Day’, wameichagua wao Wanasimba kama sehemu ya kumbukumbu ambapo huchagizwa na mambo mengi ikiwemo kutoa misaada kwa jamii inayowazunguka, kubadilishana mawazo, na mwisho huchezwa mechi ambayo ndiyo huitimisha kila kitu.

UCHAGUZI KENYA: ODINGA, KENYATTA WAPIGA KURA

Image
Kenyatta akipiga kura LEO ni siku ya uchaguzi nchini Kenya na Wakenya wengi wamejitokeza kupiga kura. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa 11:00 asubuhi. Mpaka sasa, wagombea wanaochuana vikali, Odinga na Kenyatta, wamepiga kura katika maeneo tofauti. Odinga akipiga kura. Rais Uhuru Kenyatta amepiga kura kwenye shule ya msingi ya Mutomo na amesikika akiwaomba Wakenya wote wafanye uchaguzi huo kwa amani. Kenyatta akipiga kura. Upande mwingine, Odinga amepiga  kura katika  shule ya Kibra, Nairobi. Ikumbukwe kuwa Odinga anagombea kwa mara ya nne sasa.

Rais Museveni Abadilisha Tarehe Yake wa Kuzaliwa

Image
Rais Museveni akikagua nyaraka zake za Ubatizoa. Kwa muda mrefu sana kumekuwa na mijadala hasa katika mitandao ya kijamii nchini Uganda kuhusu umri halisi wa Rais wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta Museveni. Kwa mara kadhaa serikali ya Uganda imekuwa ikinukuliwa ikisema kwamba Rais Museveni alizaliwa mwaka 1944, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana vyama vya upinzani vilikuwa vikimkosoa Rais Museveni kwamba anadanganya kwa kusema ana miaka 71. Vyama hivyo vilidaiwa kuwa alikuwa na zaidi ya umri wa miaka 75 na asingeweza kugombea tena. …Akiwa na mkewe na viongozi wa kanisa. Lakini mjadala mpya umeibuka ambapo Ikulu ya Uganda imechapisha nyaraka kwenye ukurasa wake wa Facebook zinazoonyesha kwamba nyaraka za ubatizo wa Rais zimeandikwa tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni 3 Agosti 1947 na hivyo sasa ana miaka 70. Kwa minajili hiyo, Rais Museveni atakuwa na umri wa maika 74 wakati Uganda itakapofanya uchaguzi mwingine mwaka 2021 na hivyo ataweza kugombea ten

MREMBO HAMISA MOBETO AJIFUNGUA AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME

Image
Hamisa enzi za ujauzito Mwanamitindo maarufu   ambaye pia ni muuza nyago kunako video za   wasanii Bongo ,   Hamisa Mobbeto, amejifungua mtoto wa kiume leo. Ubuyu wa Hamisa  kujifungua umezagaa mitandaoni baada ya mama yake  mzazi kuposti picha  ya mkono wa mtoto na kuandika maneno yafuatayo. “Alhamdullilah mume wangu miye peke yangu” Baada ya posti hiyo ya  mama yake mzazi , saa chache baadaye Hamisa alithibitisha taarifa hizo kwa kuposti picha ya mtoto wake na kuandika ujumbe ufuatao. “Ahsante Mungu, Karibu duniani mshindi” Hamisa ni mzazi mwenza  wa mfanyabiashara maarufu,  Majizzo , aliyezaa naye mtoto wa kwanza anayeitwa  Fantasy , ambapo mpaka sasa hajaweka wazi ni nani baba wa mtoto wake huyu wa pili.

Umesikia alichokisema Okwi?

Image
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi (katikati mwenye namba 7) akiwa na wachezaji wenzake. KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi amefunguka kuwa amejipanga kuonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa leo ili kuwathibitishia mashabiki ambao wana hofu na uwezo wake baada ya kushindwa kutamba alipokwenda nchini Denmark kabla ya kurudi kwao Uganda. Okwi aliyetua Simba akitokea SC Villa, ataungana na mastaa wengine wa Simba waliosajiliwa hivi karibuni kuonekana kwa mara ya kwanza wakikichezea kikosi hicho kwenye mchezo waSimba Day mbele ya Wanyarwanda,Rayon Sports. Mshambuliaji huyo ameliambia Championi Jumanne, kuwa atabadilisha mawazo ya mashabiki wengi leo ambao walimuona hana jipya baada ya kushindwa kutamba alipokwenda Denmark kwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu dhidi ya Rayon Sports. “Najua mashabiki wengi wana hofu na uwezo wangu kwa sababu muda mrefu umepita baada ya kuondoka hapa Tanzania, lakini niwaambie kwamb

Dokta Avamiwa Usiku, Achinjwa Babati

Image
Dk. Izack Daniel enzi za uhai wake. DUNIA haina huruma! Ndiyo kauli unayoweza kuitoa baada ya hivi karibuni mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Dk. Izack Daniel , mkazi wa Ngarenaro, Babati mkoani Manyara, kukutwa akiwa amechinjwa kama kuku chumbani kwake na watu wasiojulikana. Chanzo makini kililieleza Uwazi kuwa, siku ya tukio, dada wa kazi wa Dokta Izack alitaka kuingia chumbani kwa bosi wake huyo kwa ajili ya kufanya usafi asubuhi. Lakini tofauti na siku nyingine, ilielezwa kuwa, aligonga mlango kwa muda mrefu bila kufunguliwa hivyo aliamua kwenda kugonga dirishani. Ilidaiwa kuwa, hata dirishani nako hakukuwa na majibu ambapo baadaye familia ilipigwa na butwaa baada ya kuona damu zikichuruzika kutoka chumbani hadi sebuleni kupitia chini ya mlango. “Mkewe alikuwa amesafiri hivyo pale nyumbani Dokta Izack alikuwa na wafanyakazi tu na nyumba aliyokuwa amelala ni tofauti na ile wanayolala wafanyakazi. “Siku ya tukio, dada wa kazi alikwenda kwa aji

Rais Kagame Amjibu Rais Magufuli Twitter

Image
Rais wa Rwanda amejibu tweet ya dr John Pombe Magufuli , aliyomwandikia kwa ajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kwa awamu nyingine kuwa rais wa Rwanda. ANGALIZO; Inaonekana hawa viongozi wawili wametokea sana kuelewana mpaka kufikia hatua Paul Kagame kumwita rais Magufuli ndugu yangu, hongera sana Rwanda na Tanzania kwa mshikamano huu. Replying to @MagufuliJP Nakuahidi kuuendeleza Undugu na ushirikiano wetu katika nyanja zote kwa ajili ya maendeleo ya nchi zetu. Replying to @MagufuliJP Kwa niaba ya Wananchi wa Rwanda na kwa niaba yangu binafsi, nakushukuru sana Ndugu yangu Mheshimiwa Rais

RAIS DKT. MAGUFULI AREJEA JIJINI DAR ES SALAAM NA KUHUTUBIA WANANCHI WA BUNJU B

Image
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bunju wakati akirejea jioni ya leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano katika mkoa wa  Tanga.   Baadhi ya wananchi wa eneo la Bunju wakimsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza aliposimama eneo hilo kwa ajili ya kuwasalimia  wakati akirejea jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano katika mkoani    Tanga. PICHA NA IKULU

Rais Magufuli Agoma Kukaa Madarakani Miaka 20

Image
Rais John Magufuli akiwahutubia  wananchi. amesema hawezi kukaa madarakani kwa miaka 20 kwa kuwa anaheshimu Katiba na kwamba kazi ya urais ni ngumu. Magufuli amesema hayo leo Jumatatu, Agosti 7 katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga alipozungumza na wananchi na kuzindua stendi ya kisasa ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya siku tano mkoani humo. Kauli hiyo ya Rais imekuja baada ya Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani ‘Prof. Maji Marefu’ (CCM) kusema kwa kuwa Magufuli anafanya kazi nzuri na ingekuwa vizuri akiongezewa hata miaka 20. “Nadhani Profesa Maji Marefu unataka niishi miaka 20 zaidi na siyo kuwa rais kwa miaka 20, sitafanya hivyo kwa kuwa naheshimu Katiba,” alisema Magufuli.

Aveva, Kaburu hali tete

Image
Kesi inayowakabili Rais wa Simba Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange 'Kaburu' imehairishwa hadi Agosti 16 mwaka huu kutokana na kuwa upelelezi hujakamilika dhidi yao. Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Victoria Nongwa ambapo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ambayo mawili kati ya hayo ni ya utakatishaji fedha. Viongozi hao walikamatwa na TAKUKURU miezi miwili iliyopita kutoka sasa wakikabiliwa na mashitaka ya kutakatisha fedha mpaka kupelekea kunyimwa dhamana.

Waziri Mwijage Afunguka Baada JPM Kutoridhishwa na Utendaji Wake

Image
Waziri Mwijage (kulia) akiwa kwenye kipindi cha Clouds 360 kufafanua yaliyosemwa na rais Magufuli jana. Jana (August 6, 2017) Rais Magufuli  alitoa kauli ya kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji dhidi ya watu waliouziwa viwanda na kuvitelekeza ambapo alimtaka Waziri Mwijage kuwanyang’anya na kuwapatia wawekezaji watao viendeleza. Leo August 7, 2017 Waziri wa Viwanda Charles Mwijage amehojiwa kwenye Clouds 360 Clouds TV na kuelezea kuhusu hiyo kauli ya rais na kutoa hizi kauli. ”Kujenga viwanda sio mchezo, yapo maelekezo ya Rais viwanda vilivyo binafsishwa na havitumiki virudishwe, Rais alichokitegemea kwangu sio kile anachokiona sababu viwanda haviendi kwa kasi anayoiona na hii kuna sababu kadhaa.   “Hii sekta ya viwanda ni multi-sector maana kuna viwanda vipo chini ya Wizara ya Mifugo, vingine maliasili…. kuna viwanda vimechukuliwa lakini havipo kwenye orodha ya viwanda vilivyobinafsishwa, nahitaji Wakuu wa mik

RAIS DKT. MAGUFILI AZINDUA STENDI MPYA NA YA KISASA YA MABASI MJINI KOROGWE LEO

Image
 Taswira za Stendi mpya na ya kisasa ya mabasi mjini Korogowe mkoani Tanga ambayo imezinduliwa asubuhi hii na Rais Dkt. John Pombe Magufuli

PENZI LA GWAJIMA, FLORA JIPU PWAA!

Image
Askofu Gwajima. TAKRIBAN miaka miwili iliyopita kuliibuka sarakasi ya aina yake  katika ndoa ya waimba Injili wawili Bongo, Emmanuel Mbasha na Flora Mbasha ambazo zilisababisha mastaa hao kutalikiana mahakamani. Katika sakata hilo, Mbasha alishusha tuhuma nzito zisizobebeka kwamba Flora alikuwa na uhusiano wa kimapenzi (penzi la Gwajima Flora) na baba mchungaji wao ambaye ni Askofu wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church almaarufu Ufufuo na Uzima, Dk Josephat Gwajima. KIMYA KIREFU Baada ya tuhuma hizo palipita kimya kirefu bila ufafanuzi toshelezi wa skendo hiyo ‘hevi’ lakini kwa mara ya kwanza, Flora amepasua jipu pwaa juu ya ni nini kilichotokea. Kupitia kitabu chake ambacho Ijumaa Wikienda lina nakala yake kilichoingia sokoni wiki iliyopita, pamoja na mambo mengine yasiyoandikika gazetini, Flora alimtuhumu Mbasha kwa mambo mazito ikiwemo hilo la kumpa penzi Askofu Gwajima. TUJIUNGE NA FLORA “Wakati tatizo lile linatokea tulikuwa tunasali kwa As

Mzee wa Upako kumbadili dini Q-Chief?

Image
Msanii wa muziki wa bongo fleva Q Chief ambaye hivi karibuni ameachia ngoma yake mpya ya 'Naogopa', amezungumzia suala la kubadili dini na kuingia kwenye dini nyingine, baada ya kuwa karibu na mchungaji Anthony Lusekelo. Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Q Chief amezungumzia suala hilo na kusema huwa familia yake upande wa mama ni Wakristo na ana amini katika Mungu, lakini sio rahisi kwake kubadilisha imani yake. "Familia yangu upande wa mama wengi ni wakristo, lakini wamegawanyika kutoka kwenye uislam kwenda ukristo, baba yangu ni muislam, babu yangu ana msikiti kwa hiyo sio jambo jepesi kutoka kwenye dini yangu imani yangu kwenda kwenye imani nyingine, naamini Mungu ndiye jibu sahihi, lakini huwa nachukua ushauri wa viongozi wa dini tofauti tofauti", alisema Q Chief Q Chief aliendelea kwa kuzungumzia kitendo chake cha kuwa karibu na Mchungaji Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako', na kusema Mchungaji huyo ni sawa na ka

Rais Magufuli Amaliza Bifu la Makonda na Ruge Jukwaani

Image
Paul Makonda akishikana mkono na Ruge Mutahaba. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli , amemaliza bifu kubwa lililokuwepo kati ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kuwakutanisha wawili hao jukwaani na kuwataka washikane mikono. Tukio hilo la aina yake, limetokea kwenye Kijiji cha Chongoleani, Tanga ambapo kulikuwa na tukio kubwa la uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda mpaka kwenye Bandari ya Tanga.

SOL CAMPBELL WA ARSENAL ANATUA DAR LEO

Image
Beki wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell. BEKI wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell anatarajiwa kutua nchini leo Jumamosi mchana kwa mwaliko wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa.Campbell ambaye pia amewahi kuichezea Tottenham Hotspur ya England, akiwa nchini kesho atajumuika na baadhi ya wadau wa soka kutazama mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Arsenal na Chelsea.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba, akiwa nchini Campbellpia atafanya mafunzo kwa timu ya Magnet kwenye Uwanja wa Gymkhana na kutembelea timu ya Muungano. “Huyu ni nyota wa pili wa zamani wa soka baada ya Leon Osman wa Everton, tunajua bado watu wanakumbuka ujio wa Everton huu ni muendelezo wa kampuni yetu kuleta hamasa ya soka nchini,” alisema Tarimba.Tarimba alisema SportPesa inaendelea kuwapa hamasa ya soka Watanzania kwa ujio wa nyota huyo ukiachana na udhamini iliyoutoa kwa Simba, Yanga na Singida United.

Povu la Ndikumana kwa Uwoya Lachafua Hali ya Hewa

Image
Ndikumana na Uwoya. Mwanasoka wa Kimataifa kutoka Rwanda, Hamad Ndikumana ambaye ni mume wa ndoa wa staa wa filamu za Bongo, Irene Uwoya , amekubali kumpa talaka Irene ili andelee na maisha yake baada ya kutengana muda mrefu huku akieleza kuchoshwa na skendo chafu za mke wake huyo. Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Ndikumana ameandika ujumbe akisema amekubali kumpa Irene talaka, hivyo asisubiri hadi afe ili aolewe, ili ampe uhuru anaouhitaji aweze kufanya mambo yake bila yeye kuhusishwa. “Ulilia muda kwamba unataka talaka ili uolewe, sina kipingamizi tafuta kila utakacho ulete nitakusainia, usisubiri nife ili uolewe maana naweza kuishi zaidi ya unavyofikiria, Mungu akusimamie”, aliandika Ndikumana. Wanandoa hao wakitambo wakiwa pamoja. (Picha na Maktaba) Pia Ndikumana amesema kitendo cha Irene kumnyima kuzungumza na mwanae tangu watengane, ni kitendo kinachomuumiza sana, lakini yote anamuachia Mungu. “Ungekuwa na roho ya kibinadamu u